Nikiona wanafunzi wa Sekondari na Vyuo wanaenda shule, naona kama wanaenda kupoteza muda na pesa

Nikiona wanafunzi wa Sekondari na Vyuo wanaenda shule, naona kama wanaenda kupoteza muda na pesa

Hao waliopo kwenye ajira wanaishi milele?

Hao waliopo kwenye ajira Hawatostafu?

Makampuni mapya yanaanzishwa
yatafanywa na hao hao waliopo sasa?...
Nondo hatari, we jamaa ni wale wanaoanza kusali na kuomba kabla hujainuka kukaa kitandani,si wale wanaomfumbata faru John ile hatimiliki ya mh.mwenyekiti!!
 
Hao waliopo kwenye ajira wanaishi milele?

Hao waliopo kwenye ajira Hawatostafu?

Makampuni mapya yanaanzishwa
yatafanywa na hao hao waliopo sasa?

Kwahiyo Daktari anatakuwa yule aliyemaliza form four tu?

Hakimu yuleyule Form four ?

Muuguzi yule yule form four?

Nataka kujua tu Hivi umeacha kufanya mapenzi?kama bado unaendelea unataka mtoto anayezaliwa kutoka kwako akafundishwe na nani shuleni kama hutaki watu waende Chuo?

Hivi umeacha kutumia Internet? Unategemea tukifuata ushauri wako nani atatoa huduma kwenye field ya Network.

Umesahau kuwa bado Nchi inahitaji sana Uzalishaji katika kilimo ? Au unataka tutumie technolojia dhaifu katika uzalishaji nakukumbusha kuwa kwenye kilimo wakemia wanahitajika,Waandisi, na taaluma mbalimbali.Kwenye kilimo bado fursa ipo wazi kabisa tatizo lako umekariri kuwa lazima Uajiriwe.Nakukumbusha tu kuwa Baada ya kumaliza Chuo akili yako ikilala mambo yatalala Ukichangamka na kutumia vizuri field yako Utatoboa haraka sana.Kila taaluma unaweza kufanya shughuli binafsi au kwa kuajiliwa.Acha Julia lia Peleka mtoto Shule.





Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo umezungumzia kilimo, sasa umeenda shule umeona wanafundishwa hicho kilimo??
Nenda kaulize utakuta wanafundishwa vita ya majimaji sasa itawasidia nn??
 
nchi bila wasomi yaan wasomi wa tija sio wale waliosomea vyeti yaan inakuwa kama dumu lenye hewa ndani bila kitu..
 
Elimu ni muhimu tatizo la wasomi wetu wa nchi zetu uwa wanaelimika lakin bado wajinga hawana msaada wowote na mazingira yao. unakuta kiongozi mkubwa wa serikali anaongea pumba kama bado ananyonya. Elimu zetu hazitusaidii kitu kwanza hazijatutoa gizan ata kidogo kiteknolojia bado tegemez.. heri tu uwe mfanya biashara
 
Tatizo utaratibu wa ajira umebanwa sana kipindi hiki sambamba na maslahi ya wale ambao wapo kwenye ajira tayari, hii ishu ya korona nayo imeyumbisha sana mapato ya nchi hasa kwenye sekta ya utalii.

Lakini hii haizuii wale wenye ndoto ya kusaka elimu kuendelea kufanya hivyo, maana elimu kwa vyovyote vile haitolewi ili kumpa mtu uwezo wa kuajiriwa bali kupambana na changamoto za kimazingira.
 
Elimu ni muhimu, tena sana... Hata huko kujiajiri kama huna elimu na hujitambui utaishia kupata tu hasara na biashara itakufa.
Usije tu ukawanyima watoto wako haki yao ya kusoma kwa kuogopa kupoteza hela mkuu.

Wewe unaongea kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu (Kwa sauti ya nabii Ayubu) , kupata hasara kwenye biashara na kufa kwa biashara hakuhusiani na kutokuwa na elimu na kutokujitambua, kama that's the case, bhasi maprofesa wa economics pale udsm ndo wangekuwa na biashara kubwa hapa nchini, wao si ndo wana elimu kubwa ya uchumi??? au wale wanafunzi bora kitaifa top 10 ndo wangekuwa vijana matajiri zaidi.

Kujiajiri/ biashara haiangalii uprofesa wako wala digrii yako, wala ww ni mtoto wa nani, wala ulipata division 1 ya ngapi, au una IQ kubwa kiasi gani, kujiajiri kunaangalia kujituma kwako, uzoefu wako kwenye biashara, na elimu sahihi uliyo nayo kuhusu pesa na kukuza biashara, na bahati yako, pia kujiajiri hakuangalii unajua nini kuhusu mfecane war, au world war 2, au polynomial function, Bali kutaangalia uwezo wako wa kusoma na kuhesabu (kujumlisha, kutoa, kuzidisha na kugawanya)

Soma post yangu vizuri, sijaipinga elimu, ila nataka elimu sahihi inayoendana na mazingira ya sasa, itolewe kwa muda sahihi Lenie
 
Kwa mfano ajira zikianza kumwagika na toto lako hujalipa elimu itakuwaje?
au akija prezoo wa kumwaga ajira kama njugu na elimu uliikacha hapo utafanyaje?
 
Hiyo elimu ya form four unayosema ndio itakuletea madaktari, walimu wa kuwafundisha wengine, maengineer, na wataalamu wengine?? Unahisi wote wanahitaji kuishi kwa kufanya biashara tu???

Ili nchi iendelee inahitaji wataalamu wa fani mbalimbali pia, hii ndio point uliyoisahau.

Acha vijana wetu wasome, hizo changamoto za ajira sio kigezo cha kusema watu wasisome.
 
Elimu ni muhimu, tena sana... Hata huko kujiajiri kama huna elimu na hujitambui utaishia kupata tu hasara na biashara itakufa.
Usije tu ukawanyima watoto wako haki yao ya kusoma kwa kuogopa kupoteza hela mkuu.
Elimu ya kujiajiri siyo zao la elimu ya darasani.

Mtu anahitaji cheti cha elimu ili aajiriwe ila hahitaji hicho cheti ili ajiajiri.
 
Ili Nchi Iendelee Inahitaji:-
1 . Watu
2 . Siasa Safi & Uongozi Bora
3 . Ardhi

Maadui Wa Tanzania Ni:-
...
Maadui Wa Tanzania Ni:-
1 . Umasikini
2 . Ujinga
3 . Maradhi
4.Ufisadi
 
Mfumo wetu wa elimu na malezi unamuandaa msomi kuja kuajiriwa badala ya kumpa uwezo wa kupambana na changamoto za maisha,hapo ndipo kwenye tatizo.

Miaka minne iliyopita niliacha ajira ya Serikali na kujiari mwenyewe familia yangu yote iliona nimerogwa,na kwa bahati utawala huu umevuraga kabisa sekta binafsi hapo ndiyo naonekana nimelaaniwa kabisa 😥😥😥.
 
Elimu ya kujiajiri siyo zao la elimu ya darasani.
Inategemea unajiajiri kwenye nini. Fani zingine lazima uingie darasani mkuu.... Ukitaka anzisha mfano kampuni za Civil/Financial Consultancy/Auditing Firms/IT bila shule haiwezekani
 
Inategemea unajiajiri kwenye nini. Fani zingine lazima uingie darasani mkuu.... Ukitaka anzisha mfano kampuni za Civil/Financial Consultancy/Auditing Firms/IT bila shule haiwezekani
Hiyo taaluma kiasi kikubwa itatumika pale unapotoa huduma kwa wateja wako tu lakini connection za kupata wateja, innovation za kuboresha huduma na ujanja ujanja mwingine ambao ni muhimu zaidi kwenye biashara husika cheti hakitakuwa na msaada wowote.
 
Hii hali ya watu kuona elimu ya juu haina maana imeshamiri kwa kiasi kikubwa hata Japan. Watoto na vijana wengi hawaoni tena umuhimu wa elimu ya juu .Nilisoma tafiti moja ya nchini Japan takribabini vijana laki mbili wamebainika kukimbia shule hasa elimu ya kati na ya juu.
 
Utaratibu wa serikali katika mambo mengi ni mbovu sana na hatarishi.
 
Back
Top Bottom