Nikiona wanafunzi wa Sekondari na Vyuo wanaenda shule, naona kama wanaenda kupoteza muda na pesa

Nikiona wanafunzi wa Sekondari na Vyuo wanaenda shule, naona kama wanaenda kupoteza muda na pesa

Elimu ni muhimi sana hata bila ajira,
Elimu ni zaidi ya kuajiriwa.

Tatizo sio mfumo wa Elimu,tatizo ni mtazamo na utamaduni wetu ulivyotujenga juu ya elimu
Kwamba ukisoma lazima uje kuajiriwa imefika wakati sasa tuanze kuitazama elimu kama chachu ya kukujengea uwezo wa akili kufikiri nje ya box ( Logic and problems solving skills)...

Elimu ni kupata uelewa na maarifa ambayo mtu anaweza kupata pasipo hata kwenda shule.

Nimeshangaa pale ulipotoa mfano wa Hp, Amazon, na Microsoft... Elewa kwamba hao hawakusoma huku shit hole countries.. labda ungesema vijana wanaomaliza SUa wanajiajiri ktk kilimo na ufugaji wa kisasa hapo ningekuelewa.

Elimu ya tz ni kupoteza muda. Miaka 7+4+2+3=16 jumlisha na miaka ya kuzaliwa + miaka ile ya kupotezea muda.
 
kuna mabilionea kibao wa darasa la saba.unaweza usisome na ukatoboa
Hilo linawezekana pia ila ukifatilia vizuri utakuta wengi wamezaliwa kwenye familia bora na wanaendeleza family business so alisoma tu kutoa ujinga ila tangia mdogo aliandaliwa kuendeleza biashara.
 
Mtoa mada ww ni kenge kwel kwel.......kuna tofauti kati ya kusoma na kusoma ukose namna sahihi ya kutumia elimu uliyoipata (kujiajiri au kuajiriwa).......NASEMA KAKAE CHINI UTAFAKARI NDIPO ULETE UZI WENYE MANTIKI KENGEEEEEE
 
Tunahitaji engineers,doctors,nurses,teachers,wataalamu wa kilimo na mifugo na wengine kila sekta duniani kutokana na na ww kusoma na kukosa ajira,mazingira mabovu ya kujiajiri au kuajiriwa,wataalamu kulipwa mshahara mdogo ndio unaona elimu haina maana ......
 
Na ukipata bahati ya kuajiriwa unaishi maisha ya full stress na wengi mshahara haufiki hata 700,000 (take home )
 
[emoji16][emoji16][emoji16]bhana we kila MTU na fungu lake,,,education for self reliance
 
Kuna tofauti ya kusoma na kupata maarifa.

Kwa bahati mbaya elimu ya Tanzania mpaka chuo wanafunzi wanaopata maarifa ni wachache mnooo. Naongea hili nikiwa na ushhidi halisi. Maarifa ndio humfanya mtu ajiamini. Wasomi zaidi ya asilimia 90 kwa Tanzania hawajiamini ndio maana mtu ni daktari ila anakimbilia kugombea ubunge badala ya kuwa mbunifu aje na kitu gani kwenye taaluma yake. Kuna taasisi nyingi wewe kama daktri unaweza kuandika andiko wakaweka hela zao hususani kwenye nchi Kama tanzania ambayo bado ina changamoto nyingi za huduma za afya.

Ndio maana nasema tunaosoma ni wengi ila wanaotoka na maarifa ni wachache sana. Mtu anaetoka na maarifa ni yule ambae anaweza kuyatumia mazingira yanayomzunguka kujisaidia kabla ya yeye kusaidiwa na mazingira yanayomzunguka.

Ili tufikie huko lazima tukubali kubadili mfumo mzima wa elimu lakini pia wazazi Wana nafasi kubwa ya kubadili huu mfumo kwa kuanza kuwalea watoto katika mazingira ya kuwa na maarifa ya maisha kuliko kuwaachia wapate maarifa ya maisha kwa kupitia darasani.

Kusema kweli maisha ya Sasa ukisoma kwa kutegemea kuajiriwa utakuwa unajidanganya. Na tunakoelekea karri ya Maendeleo ya sayansi na teknolojia Hali itakuwa mbaya.
 
Ukiwa kitaa mwambie kijana aliyemaliza kidato cha 4 akuandikie 540,000 au 1mln kama ataweza uje pm nikupe zawadi.
 
Back
Top Bottom