Nikisikiliza hii clip nazidi kuelewa kwanini hayati Magufuli na sasa Rais Ruto anakutana na ugumu katika kuongoza nchi

Nikisikiliza hii clip nazidi kuelewa kwanini hayati Magufuli na sasa Rais Ruto anakutana na ugumu katika kuongoza nchi

Huwezi kumweka Mwendazake kundi moja na Mwl Nyerere. Muulize zile fedha alizowenda kuficha China zilikuwa kwaajili ya shughuli gani ?.
Hizi story za "hear say" huwa mnazitoa wapi?! Unajua kuna uvumi mwingi sana umefanya kipindi cha magufuri. Hata alipokuwa anafanya mambo yake kimya kimya watu walitafsiri anapiga hela. Uzuri wa magufuri hata kama alikuwa anapiga hela alikuwa anaifanyia inchi mazuri zaidi kuliko mabaya.

Ila ninyi watoto wa "anko kasema " huwa mna kasumba ya kutojiridhisha mnatumia zaidi maneno ya watu kujenga hoja. Bakini hivyo.
 
Mwendazake ni zaidi ya mwalimu Julius Kambarage Nyerere,
Mwalimu alitawala enzi za ujima na analog,,low populations


Magufuli ametawala zama hizi za imperialism , digital+high populations
Kwa kitu gani kichaa Magufuli umlinganishe na Nyerere? Huku ni KUMTUKANISHA Baba wa Taifa.

Vijana tatizo hamsomi historia ya Tanzania ndiyo maana unamlinganisha huyo mwendawazimu wa Chato na Nyerere
 
Kwa kitu gani kichaa Magufuli umlinganishe na Nyerere? Huku ni KUMTUKANISHA Baba wa Taifa.

Vijana tatizo hamsomi historia ya Tanzania ndiyo maana unamlinganisha huyo mwenfawazimu wa Chato na Nyerere
Bwana mdogo kuna vitu vingi sana huvijui kuhusu utawala wa Magu na Nyerere so kuna muda jitahidi kuficha ujinga wako .
 
Kutawala nchi za Kiafrika inahitajika mtu makini anayewajua haswa hawa mabeberur wazungu si watu wa mchezo mchezo, wanaweza kukupa tabasamu na furaha tele lakini mioyoni mwao wanajua wamelamba jackop la atu mzuka... ni wachache sana watanielewa ila mfano mdogo ni pale tu wapokuita kwenye usaili wa kazi - job interview... munafurahi sana , munasemezana, munaagan kwa furaha na unajaa matumaini kwamba baada ya week 2, nitaanza kazi... baada ya week 2 kuisha, unapokea barua ya kusema, asante kwa kuja kwenye interview lakini baada ya kufikiria mar 2 mbili , tumeamua kwamba hii kazi huiwezi... ni wanafiki sana wazungu- ni maslahi tu.. hawana urafiki hata maadui but wana kamsemomkao- the end justfies the means... tuwe nao chonjo sana...
 


Hiyo nchi inayoomba mkopo wa $3 billion na condition juu; wao wenyewe wana export mafuta yenye thamani $3.5 billion mwaka jana.

Katika miaka kumi ya kuuza mafuta thamani yake ni $32 billion, katika kipindi hiko nchi impeta $6.5 billion; zilizobaki zimeenda kwenye kulipa madeni ya mwekezaji na kumpa faida yake.

That’s africa for you

Watanzania wanaambiwa uwekezaji wa $42 dollar, wala hawana habari; mpaka siku watakapoanza kuona gas yenyewe aina faida yoyote kwao.
 
Hizo zilikuwa enzi za miaka ya 60-70. Ilikuwa dunia tofauti kabisa na leo hii. Marekani na Ulaya Magharibi (mabeberu) walikuwa katika vita baridi (Cold War) na nchi za kikomunisti zikiongozwa na Urusi (NATO vs Warsaw Pact). Enzi hizo kiongozi yeyote wa dunia ya tatu akionyesha dalili za kujinasibisha na ukomunisti alikuwa akitambuliwa kama adui. CIA walikuwa wakimuweka kwenye watchlist yao.

Wazalendo kama lumumba, Sekou Toure, Ruben Nyobe (Cameroon), Mandela, Rene, n.k. walionekana kama magaidi tu na kuwekewa mazingira magumu.

Nyerere alitambuliwa kama “communist sympathizer”. Hivyo alikuwa akitazamwa kwa tahadhari. Bahati yake alikuwa na marafiki wengi nchi za Scandinavia, Labour Party ya Uingereza na Democrats wa Marekani.

Vita baridi ilipokwisha 1990 na nchi zetu kukumbatia ubepari na multiparty politics, hao mabeberu hawahangaiki na sisi tena. Kwanza viongozi wetu wenyewe wanawapelekea dili za kujichotea rasilimali zetu. Km Barrick na migodi ya dhahabu. Mpambanaji Lissu alipoingilia kudai haki ya Watz, serikali ya Mkapa ilimteremshia kipigo. Tulipolanguliwa rada na ndege ya serikali, mawaziri wa Uingereza mama Clare Short na Robin Cook walijitosa kutupigania dhidi ya BAE systems na dhidi ya Tony Blair, Waziri Mkuu wao (dalali wa BAE). Serikali yetu ya JK ilisimama kidete na walanguzi eti hatujapigwa. Halafu tuliporejeshewa cha juu, bado wakakipiga juu kwa juu! Majuzi hapa tumepeleka cash Marekani na Canada kununua ndege kwa bei za “kuruka”. Mifano ni mingi jinsi sisi wenyewe tunavyouza nchi kwa mabeberu na Wachina kwa vipande vya shekeli!

Halafu tunataka kujifananisha na kipindi cha kina JKN, wazalendo wa kweli wakipigania uhuru wa mwafrika? Eti na sisi tunapambana na mabeberu! Wtf!
 
Na nina hakika bila shaka JPM aliuwawa na USA na bi tozo akapachikwa kwa ajili ya maslahi ya US. Na taarifa alipewa ya kujiandaa kuwa rais akiwa Tanga kutoka ubalozi wa US akatetemeka sana, hakujua mambo haya yanafanyika hivyo. Na shida yote ya Sumu mzee baba alilishwa Morogoro kwenye ufunguzi wa kiwanda cha Rostam. Janeth hakuruhusiwa hata kumuona pale Mzena. Anyway Jiwe hatunae na leo hii hata ufunguzi wa Ikulu ni maagizo ya US kutomtaja kabisa JPM. Ila haepukiki inabidi familia ipokee tu tuzo.
Janet alizuiliwa kumuona pale Mzena na wamarekani?

Kwenye uzinduzi wa kiwanda cha RA, alilishwa hiyo sumu kwa njia gani? Alikula chakula kwenye uzinduzi? Au ni maji?

Unafahamu protokali za rais kula na kunywa sehemu kama hizo?

Kwa maneno yako, ni kwamba walinzi wake walishirikiana na wamarekani kumlisha hiyo sumu?
 
Janet alizuiliwa kumuona pale Mzena na wamarekani?

Kwenye uzinduzi wa kiwanda cha RA, alilishwa hiyo sumu kwa njia gani? Alikula chakula kwenye uzinduzi? Au ni maji?

Unafahamu protokali za rais kula na kunywa sehemu kama hizo?

Kwa maneno yako, ni kwamba walinzi wake walishirikiana na wamarekani kumlisha hiyo sumu?
Kwa mwenye akili ya kiupepelezi ndio hint ushapewa anzia hapo. Ukiniuliza zaidi ntakuona poyoyo anaejitia mwenyenazo mbele ya umma.
 
Yaani mwendazake aliyejenga uwanja wa ndege wa kimataifa Chato kijini kwake unamlinganisha na Mwalimu Nyerere?
Kwani Chato ni DRC hapakutakiwa kupelekewa maendeleo au kwenye katiba ilishasema msipeleke maendeleo Chato? Mbona kapeleka maendeleo dodoma mpaka ikulu kajenga hamlalamiki wanajisifu kujenga ikulu ni wengine mbona kajenga Dar mafyover na stendi hamlalamiki mbona kajenga hospital kubwa ya mwalimu Nyerere memories mbona kaweka mradi wa maji Arusha hamlalamiki ila ajenda yenu Chato Chato kwahiyo mlitaka mwili wake ungepelekwa na Lori hadi chato?
 
Usimlinganishe Nyerere na magufuli, nyerere was a charismatic, intellectual, visionary,
Diplomatic,
Hotuba zake zimeandikwa, zinaishi,
Magu alikuwa na staili yake, alikuwa hapendi kukosolewa, hataki upinzani, neno lake ni sheria.
Kwani Nyerere enzi zake alikuwa na upinzani?
 
Back
Top Bottom