Nikiweka fixed deposit 10M naweza kulipwa kiasi gani na bank kila mwezi?

Wataalamu wa bank, je naweza kuweka deposit kiasi cha hela kama 10m halafu kila mwezi bank inanilipa riba? Na je watanilipa kiasi gani kila mwezi? Wakati huo hela yangu ipo tu bank?
weka pesa kwa treasury bills 364 day
 
Hii ni DCB Lamba kwanza 12% kuanzia 100m na 10% kuanzia 50m mpk 99m lakin miaka 4 nyuma walitoa offer ya 14% wajanja wakawapa ela zote wakae nazo.
 
ACCESS BANK 14% offer ukiweka kuanzia 100m kwa mwaka unavuta 12.6m net faida ukishatoa kodi bila kunyanyua kidole unalipia ada za watoto.
 

Huyu mwamba ana shida sehemu! Ameambiwa ukweli lakini hapa anaanza kuweka uongo eti imeeanza mwaka huu. Mimi baada ya kuona biashara ni changamoto pesa nyingi nimeweka fixed bank tofauti tofauti na wanangu pia nimewafungulia fixed. Hii ya TCB nimemwekea mwanangu mwenye week 2 tu hivyo ataanza kuramba >450K kila mwezi. Nitacheki hii ya DCB ya 14%. Shukrani sana mkuu.
 

Kiungwana sasa inabidi uniombe msamaha kwa matusi yako.
 
DCB offer imesitishwa wanatoa 12% tu kwa sasa kuanzia 100m ila Access wanatoa 14% kila la kheri mkuu" mapambano lazima yaendelee"
 
Biashara zinachangamoto sana mpk unaona heri nusu shari niweke fixed nipate kidogo kuliko kuchoma ela usikilizie upepo unaendaje
 
Watanzania wanataka hela zinazokuja kimaajabu yaani sio kwa kuzitengeneza kwa akili au mbinu za kijasiliamali. Mtu anataka aweke tu milioni 10 somewhere then awe anapokea hela kila mwisho wa mwezi. Na milioni kumi yake iwe available kuipata muda wowote.

Kimsingi wabongo ni wavivu and they hate working or projects hawataki wanapenda kulipwa for nothing so they can spend without caution.

Umemshauri vema lakini mimi nimekuelewa.
 
Hakuna biashara mzuri na inalipa kama ya kwenye makaratasi ha ha ha

Yan hapo ni very smooth, sasa nenda kafanye uone balaa lake
But ni muhimu kuwa na projection ya kibiashara ili uweze kujua unaelekea wapi.
 
Haya saww na yale niliwahi kuandika humu ya wale mnaita ___speaker kwenye events huko, sijui kuku mmoja na mayai.

But ingia field alafu uje na uhalisia ndo utajua kwa nini?.
 

Watu wengine hua mnafurahisha sana. Jiulize hiyo Milioni 10 anayotaka kuiweka benki ili awe anapata gawio bila kufanya kazi ameitoa wapi? Yani 10 Milioni ameitoa wapi? Ameiokota? Ujue sometimes muwe mnfkr pande zote. Lengo la jamaa kuweka huko itakua Kuna mchongo anausoma. Mm nimeweka UTT lengo ni kusoma game maana biashara niliyokua naifanya ikanipa hiyo 10m kwa sasa haisomeki so nimeamua niweke UTT ili niwe napata hela nikisubiri mambo yakae sawa. Je hili ni kosa? Tufikiri kwa mapana na marefu kabla ya kutoa maoni
 

Hawa ndo wanakwambia walianza mgahawa na punje moja ya Mchele na sasa wanapika wali zaidi ya kilo 5[emoji23]
 
Mchongo gani huo mkuu...Tupe Nondo.
 
Haya saww na yale niliwahi kuandika humu ya wale mnaita ___speaker kwenye events huko, sijui kuku mmoja na mayai.

But ingia field alafu uje na uhalisia ndo utajua kwa nini?.
Kwahio nisisome chuo kisa wanachuo wengi wapo mitaani?

Nimeandika kwenye maneno ya mwisho atumie akili yake ili azalishe hela. Hio ya bodaboda ni kamfano tu. Sijui umenielewa?.
 
Kitu kimoja nakijua binafsi watanzania wengi waoga wa kujaribu, wengi wao wana akili ya kuajiriwa na utajiri wa haraka.

Nimetembea nchi nyingi duniani watanzania wengi wao wanatumwa tu, hawana vision ya kujitoa wenyewe kimaisha.

Ndio maana mimi huwa karibu na waNigeria na waKenya hawa jamaa wao kujituma ndio kwao.

Mfano hapa jamaa ana 10M anafikiria kuwekeza bank apate laki 1. Wakati bank wao ukiomba mkopo 10M riba yake 10% hio ni 1M. Sasa nani kanufaika hapo?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…