Niko Kigoma, kweli sura siyo roho

Kuna mgombea mmoja wa urais mwaka 2010 alituahidi kuigeuza Kigoma kuwa Dubai. Mpaka leo huwa nikimuona, huwa natamani kunywa pombe, maana huwa najicheka sana. Niliamini sana alichokuwa akisema. Hata sasa hivi najipiga kifua na ninasema mimi FALA kwa kuamini wanasiasa! 😅😅😅😅
 
Gharama za maisha ziko chini ukilinganisha na wapi? Maskini gani anaweza kulipia migebuka kwa 25000 hotelini? Nguo dukani ziko juu sana tofauti na kwingine. Kifupi,gharama za maisha Kigoma ziko juu sana isipokuwa nauli za treni daraja la tatu C
 
Kigoma kuna mama alijifungua kifaranga cha kuku
Watu waliokufa na kuzikwa kurudi nyumbani baada ya muda au kuonekana tena mtaani hayo ndiyo mambo kigoma
Sijawahi kuupenda uwo kwa namna yoyote.
Mhhh! Taratibu mkuu. Ya kweli hayo? Au ndie zile story za wakina Juma Njemba ?
 
Hizo bei ulizozishangaa, kwa mfano, juisi ya muwa, hiyo 1,000/- ni kwa lita ngapi?
 
Vp kuhusu mipalangee
 
Jiandae vema,si pazuri sana kama tunavyosimuliwa. Nilikaa siku nne tu Mwitongo Hotel nikakimbilia zangu Mwanza kumalizia mapumziko yangu
Nitafikia huko kwa masister, huwa sina mambo mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…