Niko njia panda yenye maumivu moyoni: Biashara yangu imelala sana je, niende kwa mganga?

Kumbe wee Ni kiaz HV unasema mganga anaomba kwa Nani Mbna una majibu ya kipuuz HV kama wee na familia yenu Ni washirikina nenda huko Kama unaona watakuokoa kwenye biashara zako


Je lini umewahi kufanya tour kwenye maduka mengine au wale wateja wako wanauzaje kwa Sasa HV na Ni Wapi wanapata mzigo hujawi wee uko hapa kuomba uungwaji mkono juu ya uganga


Na Bado itadorora Hadi umtafute mwamposa alipo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Huna haja ya kukata tamaa mwezi mmoja tu unawaza wataalam, huu mwezi ni mgumu wengine hapa unaenda kupambana unarudi kama ulivyoenda ndio biashara waulize wateja wako mnaoshibana kama wanauza kama zamani kabla haujaenda kuharibu,pesa za masharti hazina Raha muda zinaisha.
 

Cool down buddy..!!
"Kiazi" stop attacking people personally..!!

Halafu mwamposa hivi analipa kodi na ile biashara yake ya Mafuta ya upako?

#YNWA
 
Kwa kukufahamisha mwanadamu hapati janga lolote isipokuwa kutokana na chumo la mikono yake.

Sasa mbona watu wa dini mnatuchanganya..
Wachungaji husema, biblia inasema "Mapito hayapaswi kuja ......" Yaani Mungu karuhusu majanga kutupima.

Wewe Mzee wa Quran unasema "Tunayaleta"

Kwahiyo wa Ukraine wamefanya nini kustahili machumo Yale wapitiayo sasa?

#YNWA
 
Mimi ni mtumishi wa umma Ila pia nina ndoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa sanaa...
Hivyo vitu mara nyingi haviendi Pamoja.

USHAURI

Watengenezee Ofa ya Valentine mwezi huu. Punguza kidogo faida yako wape Offer. Hii pia iwe mbinu ya kuzungumza na Wateja wako(Yaani upate cha kuanzia kuongea na Mteja wako kwenye Simu). Jaribu hili kwa Wiki hii then uone Mwitikio wa Wateja wako. Wajulishe hii Offfer wale wateja wako WAKUBWA wengi kuliko wadogo.

Hakuna mganga zaidi ya MUNGU. Usidanganywe na hao Washikaji zako.

Mwisho kabisa Mkuu Liverpool VPN , Magumu huyapitii peke yako kaka, na hakuna ambaye hajatoka mbali. Just Relax hizo ni changamoto za kawaida saaaaaana katika Biashara. Ulitakiwa uanze kuwa na Mashaka endapo hio hali itaendelea for 3 months consecutive.
 
Umempatia wazk zuri sema naona tayari Imani yake iko rigid akadai kuwa Ana masters amesoma vitabu vya robati kiyosaki as if ni guarantee ukivisoma unatoka
 
Unakosa Business psychology due to lack of experience. Business almost zote huwa na uptrend, down trend and sometimes huwa na consolidations za kutosha. Kuna biashara nyingine, miezi kadhaa huwa na faida ndogo sana lakini hapo unatakiwa uwe na subira maana unaweza kuwa na mauzo machache mwezi mmoja au miwili ila miezi mingine ukapiga pesa ambayo itafidia miezi yote uliyokuwa chini. Achana na mambo ya waganga.
 

Najua ajira na biashara haviendi pamoja ila sikua na njia ya kupata mtaji zaidi ya mshahara.

Na kwa hii biashara nathibitisha Asilimia 100 mtaji umetoka kazini.

Kwahiyo bila huu Utumishi wa umma NISINGEKUWA HAPA.

#YNWA
 
yaani january ambayo kila mtu analia pesa zote zimeenda mashuleni hata wenye mabasi ya abiria wamepunguza mabasi barabarani kwa sababu abiria ni wachache, hilo umeshindwa kuliona, umeanza kulia na kutamani kwenda kwa wachawi. Pole sana.....watu kama wewe ndiyo mnaamini ushirikina kuliko uhalisia.
 
Ni kweli kuna jamaa yangu ana biashara ya usafirishaji kwasasa kayasimamisha. Ni kipindi tu
 
Acha imani potofu wewe! Hata mimi pia ni mdundulizaji, natokea Tanga! Lakini sijatanguliza hizo imani za kishirikina. Huko ukienda utaishia tu kupigwa, na kupotea mazima.

Biashara kuna wakati inapooza kidogo! Halafu kuna wakati inachangamka. Hivyo jitahidi kuwa mpole. Na usisahau hii miezi ya mwanzoni mwa mwaka, watu wako busy na ada. Hivyo baadhi wanapunguza matumizi yasiyo ya lazima, yakiwemo hayo ya vinywaji.

Mambo yakitengemaa utaendelea kulaza hizo milioni zako 2-3 kwa siku.


Ila binadamu tunatofautiana! Mimi kwenye kijiwe changu nikilaza laki, basi ujue siku hiyo mambo yameenda vizuri. Sasa wewe laki 5 unataka kwenda mpaka kwa mganga wa kienyeji! 🤔
 
MKuu pole kwa kipindi unachopitia kibiashara.
Kwa ufupi tambua biashara ina kupanda na kushuka kwahiyo ukiona imeshuka unapaswa kuangalia je wakati huo biashara huwa zinakuwa chini?
Kuna nyakati ambazo biashara inakuwa mbaya tuu si kuwa unakosea mahali ila ni kipindi ambacho watu hawali na hawanywi.

Ukiona kuwa ni kipindi ambacho biashara inatakiwa kuwa juu na unafanya vibaya basi inafaa ujitathimini wapi unakosea.
Kunakipindi kwenye biashara hata ufanye matangazo huwezi ongeza kitu maana ni kipindi za mzoroto wa biashara mkuu

Ushauri wangu kwako. Tuliza kichwa na anza kupitia jambo moja moja katka nlokwandikia.

Mganga achana naeee atakuondoa kwenye mstari wako milele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…