Niko Uganda, timu yao imefuzu AFCON ila sijasikia Mseveni akisifiwa wala kuongelewa

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Uganda wamekuwa wa kwanza kwa EAC kufuzu Afcon Ila cha kunishangaza huku Uganda sioni Mseveni akitajwa polote pale. Na raia wako kimya kana kwamba hakuna kilicho tokea. Nikajisemea sasa ingekuwa kule kwetu, nahisi mida hii tusingelala kungekuwa kuna Jam kwenye TV na radio za kuabudu na kusifia, TShirt zenye picha ya Mama zingetengenezwa.
faster

TFA wangekuja na taarifa rasimi ya kusifu na kuabudu.

UVCCM wangeisha andaa maandamano maalumu ya kumpongeza Mama.

 
Waganda wanadharau sana ni muhimu kutambua mchango wa serikali ya mseveni katika kuwafanya wao kuingia afcon
 
Unasema?
 

Attachments

  • downloadfile-13.jpg
    73.3 KB · Views: 3
Basi sifa kwetu tunawazidi Uganda kusifu!!

Lazima ujifunze kuona positive kwenye kila jambo kijana
 
Kwenye msiba wao King Kikii kuna picha yake
 
Ile ni Uganda na hii ni Tanzania hiyo tu inatofautisha
 
Huyo yupo madarakani tangu 1980's; wamemsidia mpaka maneno ya kumsifia yamekwisha na Sasa wanabaki kumuangalia tu maana hata mwenyewe uelewa unaanza kuisha......haelewi chochote kinachosemwa: ukisema sawa na usiposema sawa.

Hata hivyo, kwani tunalazimika kuwa kama wao?!!! Mama Samia mitano (5) tena.
 
Watamani tuwaige Uganda.
Basi na sisi Samia na Familia yake watawale miongo kadhaa kama alivyo Museveni na family yake
 
Tanzania kodi za wananchi tunatumika kwenye mpira kutoa zawadi kama za binafsi
 
Wangekuwa Waganda wanajitambua wasingekubali kutawaliwa na familia moja ya Museveni kuanzia mwaka 1986 hadi leo.
Kuna tofauti gani kutawaliwa na chama kimoja CCM tangu uhuru na kutawaliwa na chama kimoja NRM na raisi moja tangu 1986.......mbona ni yale yale tena ya uganda kuna unafuu bidii za kumuondoa zipa ila hapa sioni CCM inaondolewa hata iwe miaka 50 ijao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…