Mwanamke akishakuwa Wife material (MKE Bora/Mwema) hicho ndio kigezo kikubwa cha kumfanya Aolewe.
Umaskini wa kwao haumhusu na hauhusu ndoa yenu ikiwa hauathiri U-wife material wake.
Sidhani kama Mtoa mada anazungumzia tukio halisi. Ila anachojaribu kukifanya ni kuwaambia Wanawake waache Tabia ya kuangalia wanaume Kwa kigezo cha Mali na utajiri wa nyumbani kwao.
Bali waangalie kama Mwanaume anavigezo vya kuwa Mume Bora(husband material) basi waolewe naye.
Mtoa mada anajaribu kueleza kuwa hata Sisi wanaume tunaouwezo wa Kutumia kigezo cha umaskini na kukosa Pesa Kwa Wanawake kuwabagua na kutokuwafanya kuwa Wake zetu. Kama vile baadhi ya Wanawake wanavyobagua wanaume Maskini.
Na hili likifanyika na tayari siku hizi linafanyika, basi Wanawake wengi watajikuta kwenye Wakati Mgumu kwani kiasili Wanawake hawakuumbwa kuwa watafutaji.
Msimamo wangu;
Sisi wote ni binadamu, tuna makundi yetu yanayotutofautisha, kimaumbile, kifikra, kiuchumi, kivipaombele, kiutamaduni n.k
Kila MTU atafute wakufanana naye linapokuja suala la Ndoa. Hiyo ndio huitwa Familia.
Maskini Kwa Maskini
Matajiri Kwa matajiri
Wazuri Kwa wazuri
Wabaya Kwa wabaya
Watawala Kwa Watawala
Watawaliwa Kwa watawaliwa.
Waovu Kwa waovu
Wema Kwa Wema.
Werevu Kwa Werevu
Wajinga Kwa wajinga
Kama MTU anataka kuvunja boundaries basi awe na chaku-offer
Mfano, MTU ni masikini anataka kuolewa na Tajiri. Basi itampasa awe Mzuri au mwenye Akili Sana.
Lakini tofauti na hapo ni kutafuta machafuko, kunyanyasana, na kubaguliwa.
Mwanaume anaoa Mwanamke anayefanana naye. Ukiona mwanaume anafanya uchaguzi katika kuoa, akapata Mwanamke vile umuonavyo Mwanamke huyo ndivyo alivyo Mumewe bila kujali yupoje.
Sasa hapo ndipo kipengele kilipo
Mwanzo 2:24
18 BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. . 20Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye.
Mambo ya Walawi 19:19 SRUV
Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa mfugo wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja; wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja