Niliamua kumuacha huyu 'wife material' sababu ya umasikini wa kwao

Niliamua kumuacha huyu 'wife material' sababu ya umasikini wa kwao

Nimekuja kujifunza na kugundua kuwa familia maskini na duni huendelea kuwa hivyo sababu ya uchawi na ushirikina.

Yani akiibuka mwenye Neema kidogo watampiga vita huyo watamroga kila mtu lwake!

Yaani naona wanajisemea moyoni kuwa “sisi tunaganga njaa yeye afurahie maisha kama nani?!

Umaskini ni laana!

I’m humbled to say this!

Laana maana yake ni kutokufanikiwa.

Unakuta mababu na mabibi waliua watu kwa uchawi au wazazi wewe mtoto na mjukuu lazima mta-suffer the consequences.

Mtalipa gharama ni swala la muda tu.
"Nimekuja kujifunza na kugundua kuwa familia maskini na duni huendelea kuwa hivyo sababu ya uchawi na ushirikina."

[emoji115][emoji115]

Mimi pia nimeng'amua hili hivi karibuni. Na hawapo tayari kuuachilia. Ni jambo la kumshukuru Mungu sana kama hutokei ukoo wa kichawi/kishirikina.

Kifupi tu ni kuwa masikini wengi wameridhika na hali zao hata hawawazi, ila tu hawaridhiki na kupiga hatua chanya kwa familia zingine. Hapo ndipo penye tatizo.
 
Wanawake tafuteni hela mtakosa wachumba.

Nilikutana na huyu mwanamke miaka ya nyuma huko.

Akawa abakuja gheto anapika, anafua, usafi anafanya na moto nampelekea.

Hakuwa na makuu kivile ila alikuwa na simu kali kuliko yangu, akivaa anapendeza sana nikasema mke ndio huyu twende kwenu.

Tukaenda kwao Singida, kutoka Singida mjini hadi kwao ni masaa sita, kata inaitwaje sijui ila ni kabila la Wanyisanzu.

Nilichokiona sikuamini, kwanza kijiji hakina mtandao wa simu mpaka upande kichuguuni, maji ya kunywa yana rangi ya chai ya maziwa, choo cha shimo hakina mlango ukisikia mtu anakuja unakohoa ili ageuze

Kitanda cha kamba, kajumba kenyewe ukipiga teke kanadondoka.

Baada ya kurudi mjini nilifuta namba yake palepale.

Mimi ninaamini umasikini kama sio laana basi ni kitu fulani hivi cha kurithi

Wanaume masikini kuachwa ruksa ila wanawake masikini kuacha utaambiwa ni kukufuru Mungu...

Wanawake tafuteni hela. Na nyie makamanda mnaoa watoto masikini mbinguni moja kwa moja
Chief upo sahihi kabisa kwa dini yet ya kiislam ishaeleza tuoe familia yenye dini au yenye uwezo yan pesa hata mtume wetu Muhammad kipenzi alimuoa bi aisha alikuwa tajiri sana siyo maskini kwaiyo upo sahihi sana tuoe familia zenye uwezo wa pesa
 
Yesu ana pepo!?

"Amin amin nakuambia mimi hamnami siku zote lakini maskini watakuwepo hata ukamilifu wa dahari"

Maskini WAPO watakuwepo Hadi Mwisho wa Dunia!

CHUKUA hiyo itakusaidia!

Halafu kuna HUU ujinga unaitwa "tafuta pesa" kana kwamba ukipata pesa utapata ridhiko la nafsi na Roho ni ujinga sana mkuu!!

Unajisikiaje unapotambua Kuwa huyo mwenzi ulienae alikupendea pesa au uwezo fulani!unajisikiaje!?kwani we ni roboti la kuchapisha noti!?yaani WEWE huna cha maana ulichomvutia huyo ulienae ni pesa tu,yaani pesa ina thamani kuliko muonekano na utu wako!?

Binafsi huwa nahisi mnyonge Sana nikigundua Kuwa nakubalika kwasababu ya materials badala ya my uniqueness!

Naumia sana mkuu, SIPATI ridhiko kwa mvuto wa materials!
Washamba ndio wanahisi mapenzi ni kuwa na pesa. Wanaishia kuumia vibaya sababu wanakosa real ass partners.
 
We mwenyewe sikujui ila nina uhakika kuna wanawake uliwatamani ukawakisa sababu walikuona hauna uwezo,sijui lakini nahisi tu
That was the problem, mwanamke asipokukubali jinsi ulivyo wewe ndio una faida zaidi kwa sababu yeye ameamua kuchagua fake path.Atapata ambaye ana hela ila hampendi anamuigizia.
 
Mungu aliyekupa utajiri,ndio aliyewapa umaskini wengine. As long as tupo duniani,huwa tunalia kwa kupokezana. Kwa kufuru hizo,ipo siku....me nna mke,mke wangu kwao ni masikini lkn tunafurahia maisha na tunakaribia utajiri sasa alihamndulilah...na kwao tunasaidia naamini ndio maana Mungu anatubariki. Utubu ndugu,ni bora ukae kimya.
Mungu hampangii mtu kuwa tajiri au masikini
 
Hiyo Ni tabia tu ya kupenda kitonga na uoga wa majukumu ambao Ni janga la hiki kizazi.....yaani mwanaume kabisa unajinadi lazima nioe mtoto wa kishua ili iweje wajomba wakuendeshee familia kwa Mali za baba mkwe??Kitawakuta kitu Shauri zenu
Kwamba kuoa ni lazima uoe familia nzima?
 
Nyie wenyewe hamuwezi kuolewa na mwanaume mwenye background ya umaskini kwao

Mnatumia neno "Kitonga " kama defence mechanism kwenu

Ku oa mwanamke mwenye background nzuri haimaanishi usaidiwe majukumu
Shida ya wanawake wa hivyo ukimleta mjini akapata exposure anakuona wewe kidampa. Wanakuwaga na ulimbukeni wa kishamba sana na kama ni pisi basi lazma vijana wa mjini watapiga tu.
 
Na ikitokea ndani ya wiki ukapata ajali ukavunjika mikono au miguu, utaanza kulialia?,hakuna anayependa kuzaliwa kwenye hali ya chini inatokea tu.

Kama bado upo duniani usikufuru Kwa lolote shukuru Mungu kwa hali uliyonayo, halafu unaonekana na wewe ni maskini tu. Watoto wa kishua huwa hawana akili za kipumbavu kama hizi zako.

Una uhakika ni mtu anayeamini uwepo mungu huyu?
Maana sidhani kama angefanya au kuandika hayo aliyoyafanya
 
Shida ya wanawake wa hivyo ukimleta mjini akapata exposure anakuona wewe kidampa. Wanakuwaga na ulimbukeni wa kishamba sana na kama ni pisi basi lazma vijana wa mjini watapiga tu.
Akishakua hivyo unapiga chini una download mwingine..kuishi kwa hofu ya kuwaza mabaya nao ni umaskini wa akili.

Mimi familia pekee ambayo siwezi kuoa bwana ni yenye mambo ya kichawi. Mamaye hizo naogopa kama moto wa jehanamu.
 
Back
Top Bottom