Niliamua kumuacha huyu 'wife material' sababu ya umasikini wa kwao

Niliamua kumuacha huyu 'wife material' sababu ya umasikini wa kwao

Wanawake tafuteni hela mtakosa wachumba.

Nilikutana na huyu mwanamke miaka ya nyuma huko.

Akawa abakuja gheto anapika, anafua, usafi anafanya na moto nampelekea.

Hakuwa na makuu kivile ila alikuwa na simu kali kuliko yangu, akivaa anapendeza sana nikasema mke ndio huyu twende kwenu.

Tukaenda kwao Singida, kutoka Singida mjini hadi kwao ni masaa sita, kata inaitwaje sijui ila ni kabila la Wanyisanzu.

Nilichokiona sikuamini, kwanza kijiji hakina mtandao wa simu mpaka upande kichuguuni, maji ya kunywa yana rangi ya chai ya maziwa, choo cha shimo hakina mlango ukisikia mtu anakuja unakohoa ili ageuze

Kitanda cha kamba, kajumba kenyewe ukipiga teke kanadondoka.

Baada ya kurudi mjini nilifuta namba yake palepale.

Mimi ninaamini umasikini kama sio laana basi ni kitu fulani hivi cha kurithi

Wanaume masikini kuachwa ruksa ila wanawake masikini kuacha utaambiwa ni kukufuru Mungu...

Wanawake tafuteni hela. Na nyie makamanda mnaoa watoto masikini mbinguni moja kwa moja
📌📌📌🔨
 
ila singida kuna umasikini sana wakuu sijui hawa ndugu walikosea wapi. Singida sio ajabu kukuta binti wa miaka 25 ana watoto sita au tano. Kule miaka 14 mtu ana mimba tayari, wako mbio mbio sana.
Singida na dodoma ni jangwani ,ndio kisa cha umasikini wao,ukipita kiangazi ni sawa na uko afghanistan
 
Kwani ulitaka kuoa familia yote au mke? Umesahau dhahabu hupatikana mbali na pagumu kuifikia? Ukimpata wa familia bora wanaweza kukudharau pia kwa ulivyo. Anyway ni maono yako na misimamo hatukuingilii.
 
Mwamba kaongea ukweli usiotakiwa kusikika. Japo kiukweli kupanga ni kuchagua ila usioe sehemu ambayo mnapishana sana hali ya maisha. Sio umaskini au utajiri lazima pazingue tu maana mna mifumo tofauti ya maisha na malezi.
Ukweli mchungu 😃
Kuna mwamba alishafanya kitu kama hiki
Demu alikuwa mzuri ila jamaa alipopata file anapotoka akarudi nyuma ila msichana hakujua sabb kwann jamaa kachomoa
 
Back
Top Bottom