Nilianza kujitambua kuwa ni mgonjwa wa akili tangu mwaka 2021(msongo)

Nilianza kujitambua kuwa ni mgonjwa wa akili tangu mwaka 2021(msongo)

Ambao hamna?
😄
Life is spiritual by default Kwa yyt uwe unataka au hutaki, unaamini au huamini ,ndo ilivyo ....
Kila unachoona ni Cha kiroho kabla hakijawa Cha kimwili.....yote tunayoyaona mwilini ni manifestation ya yaliyoko rohoni huko...
Km hujapitia shida shukuru Mungu tu, ila ukipitia utakuja kunielewa .
Acha niishie hapa...
Hongereni sana wenye roho, binafsi sina roho wala hiyo kiroho siishi na wala sijawahi kuihakiki naona kila mtu yupo kivyake madam ila Hongereni mno
 
Chief kama una uwezo basi jaribu kufanya carnivores diet,hizo changamoto zako zote zitatosha. Mungu akusaidie katika hii safari yako.
 
Habari wanajamiiforum.

Muda huu ninaona ni vyema nitoe dukuduku langu ili nipate msaada na ushauri nasaha

Nilianza kujitambua kuwa ni mgonjwa wa akili tangu mwaka 2021(msongo).kipindi hicho nilikuwa mdogo kiasi lakini nilikuwa naona vitendo vya hali ya kunyenyekewa sana

Pale ninapoghafirika,baada ya kujitambua nilianza mchakato wa kutafuta vidhawishi ambavyo vinaweza kupelekea kupunguza au kuondoa kabisa tatizo hili kwa kujichanganya mara kwa mara na jamii,kushiriki mazoezi na kuzingatia mlo.

Kwa kifupi niliendelea vizuri kwa wakatu huo.Lakini ilipofika mwaka 2019 kutokana na mazingira niliyokuwa ninashi,hali ilirejea tena na ilikuwa ni hatari sana,nilijaribu kutafuta washauri wabobezi na niliwapata akiwemo shool mate wangu ambaye alikuwa akihudumu UDSM,pamoja na mtaalamu wa human brain enginear kutoka sweeden.

Walinisaidia sana na nikajaribu kuacha vishawishi nilivyokuwa nikifanya kupunguza maumivu makali ya kichwa(kwa nilivyo amini)ikiwemo pombe,madawa tofautitofauti ambayo yalichangia pia ukosefu wa umakini kazini.mwaka 2024 mwezi wa 8 hali ile ilirudi kwa kasi kiasi kwamba ilichangia matatizo na kuibua magonywa mengine kama vidonda vya tumbo,bawasili,kukosa hamu ya kula,kulewa sana,na mengine mengi...

Mungu mkubwa nilipatana na mtu ambaye alinisaidia kupata tiba ya bawasili ambayo nimegundua mabadiliko chanya mwezi may mwaka huu.licha ya kuwa kwa sasa kichwa kinaniuma sana hadi machozi na mafua yananitoka bila mpangilio haswa ninapo kuwa peke yangu isitoshe kwa sasa pia ninatumia madawa sana bila ya kujali mlo,nimejitahidi kutumia vidonge vingi sana badala yake ni hakuna dawa hakuna mabadiliko na wakati mwingine hata nikitumia zile dawa mambo ni yaleyale.

Usingizi kwangu ni kama sherehe kiasi kwamba umechangi kuporomoka uimara na nguvu ya mwili.madawa ya kulevya yamekuwa ni kama maisha yangu.
WAKUU NAOMBENI MSAADA WENU
Pole mkuu
 
tafuta kanisa linalokemea roho chafu na uweke mpangilio wa maombi kwa siku mwenyewe usisahau na nyimbo za kuabudu kama kuna watu walikuwa kikwazo katika maisha yako futa kabisa uhusiano nao ikiwezekana badirisha mazingira ya kuishi.

Ishi na watu wengine ambao hawata kupeleka nyuma tena utajikuta umekuwa mpya na mwenye nguvu ya roho na akili.
 
Back
Top Bottom