Nilichekwa sana Style yangu ya malezi ila leo hii watu wanatamani kuniiga

Hongera kwa namna unavyomlea mwanao, mwanzoni nilipokua nikisoma maelezo yako nilifikiri uliamua kumuhamisha mwanao kwa sababu ya ukata.
Wazazi tuliowengi tunafikiri nkija sahihi ya kuonesha upendo kwa mtoto ni kumdekeza, kumchekea hata anapokosea.

Mtoto ili awe ni mwenye nidhamu akemewe, afundishwe stadi za Maisha na inapobidi aadhibiwe kwa fimbo au namna yeyote ilosahihi
 
Ni vizuri pia
Ongera kwa kujiongeza kumtengenezea mazingira ya kukuza mahusiano yake na jamii
Kuna mambo mabaya anaweza kujifunza njia anazopita, you can't believe.Don't trust neighbour.
 
Bora umngangalishe mapema mkuu maana Ukimlea kimayai akipata tabu kidogo tayari anakua "Mali ya Wenye Mali" [emoji2]
 
safi sana...mkuu
 

Wazazi wengi utasikia tukisema "sitaki mwanangu apate shida nilizopata mimi". Au "mimi natafuta hela ili mwanangu asiteseke" Hapo ndio tunadhani kwamba tunamsaidia huyo mtoto, na ndio tunaonyesha upendo. Tunasahau kwamba hizo shida tulizopata sisi ndio zimetufanya tukawa wapambanaji mpaka tumeweza kufikia hapa tulipo!

Matokeo yake sasa tunatengeneza kizazi cha watu nyoronyoro wasioweza kufanya kitu chochote.
 
1

Kizazi cha ajabu kabisa, walaini kama mlenda. Mtoto ana miaka 35 anaishi nyumbani. Anasema hakuna ajira.

Kulikuwa na ajira miaka ya 1950's hadi 1970's.

Wanaume, vijana hawakukaa nyumbani wakilalamika,kupinga, kutukana mitandaoni?

Nyerere alikuwa na ajira ya kuungaunga mwazoni (Mwalimu). Baadaye akasaidiwa.

Pamoja na matatizo yetu Tanzania bado ina fursa kibao.

Muhimu kuziona, kuchacharika. Hakuna kitu chochote muhimu kimekuja kirahisi.
 
Hongera mkuu kwa kuanza safari ila safari bado sana akiweza kupita salama kwenye changamoto akiwa sekondary then chuo na mahusiano basi umempata.

Tuleee kwa kumuomba Mungu aweke baraka zake
 
Hilo swala la kutembea miguu kuna raha yake nalikubali kabisa 100%...nakumbuka kipindi npo o level niliwahi nunuliwa baiskel na mshua lakini nilkuwa naiacha home ili mradi tu nitembee na wenzangu tupige story njian
Vuta picha mshua angekulipia schoolbus
 

Kuna vitu ambavyo logically havi make sense kama hilo la kusomea vibatari maana kwa sasa hata hivyo vibatari havipo. Lakini pia "generation wealth" haimaanishi kuachana na kila kitu tulichokua tunafanya (hata vile vizuri) na kuanza kufanya vitu vingine in the name of maendeleo. Wealth inajengwa juu ya kile kilichopo, haijengwi hewani.

Mfano, kwani kutembea kuna ubaya gani? Kama shule haiko mbali, ni walking distance, mtoto sio mdogo, kuna ubaya gani akatembea badala ya kupanda schoolbus au kupelekwa na gari? Mtoto kusaidia kazi ndogondogo za nyumbani kuna ubaya gani? Sasa hapo ndio mtu anakuambia "sitaki mwanangu apate shida, mimi nilifanya sana hizi kazi sitaki mwanangu apitie hayo!"

Na kingine, haya mambo ya maadili, heshima nk hayajengwi na mzazi peke yake! Ni ngumu sana kwa mzazi kujifungia na mtoto wako useme unamfundisha maadili. Hayo yanajengwa partly na mzazi, partly na jamii inayomzunguka kwa kuona, kusikia na kujifunza kwa wengine. Sasa inapotokea mtoto muda wote yupo kwenye gari ya shule, au ya mzazi kupelekwa na kurudishwa, na nyumbani ni geti kali, automatically anakua isolated kutoka kwenye community, matokeo yake anaona wa kuheshimiwa ni baba yake na mama tu, wengine ni vikaragosi tuu.
 

Common sense is kind of difficult kwa binadamu wa leo kuifuata. Yeye anatafuta likes.

Mfundishe mapema sana kujitegemea despite all dangers. Ikiwezekana ajifunze kupigana mapema sana. Hata pen knive inaweza kusaidia kutembea nayo.

Tembelea naye hospitalini, watoto yatima, omba omba mtaani, wagonjwa wa Cancer, HIV kila mwezi na kutoa misaadaa.

Atajifunza kitu kitachomsaidia kwenye maisha yake.
 
Ndiyo mkae na upuuzi wenu namuendelee kuzalisha mashoga kwenye hizo shule zenu
 
Hii ndio nyungu iliyo sahihi...

Hongera sana mkuu, pia Ahsante sana kwa hili somo zuri la malezi!
 
Mmmm kukaa porin wik nzima?
 
Very deep thoughts mkuu, kweli tuna watu walioelimika humu jf, umegongea nyundo points nyingi sana,
 
Kuna mambo mabaya anaweza kujifunza njia anazopita, you can't believe.Don't trust neighbour.
uwangalizi wa karibu na kumfatilia mara kwa mara yupo wap, anacheza na nan na ni mchezo gan anaocheza. Hii itasaidia pia
 
Waafrika huwa wanajiandaa kuishi maisha duni. Mtoto akipelekwa shule nzuri kila mtu anashangaa... roho ya umaskini.
 
Ni vizuri kumpa elimu sahihi katika mazingira sahihi; kuna mzee mmoja yeye ni mfanya biashara ameweza kumiliki asset mbalimbali ikiwamo viwanda , hotel, shule, usafirishaji n.k Na watoto wake wote watano amewasomesha nje, kuanzia chekechea mpaka masters. Cha ajabu mpaka leo hii, huyo mzee anapambana tu, watoto wamekuwa sio wazalishaji zaidi ya kutumia tu. Nadhani njia unayotumia ni sahihi, na inamjengea mtoto kuishi mazingira halisi ya kitanzania kwa sababu hutegemei akawe Director IMF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…