Nilichekwa sana Style yangu ya malezi ila leo hii watu wanatamani kuniiga

Mkuu nimechukua notsi, nakubaliana sana na malezi yako hasa hasa vipengele viwili:

Shule na marafiki na Electronics

Watu wengi hawajui kwamba hizi electronic zimeundwa kuwa addictive

Mtoto, tofauti na mtu mzima, hana uwezo wa kujizuia

Michezo kama mpira, akicheza huwa anachoka; ila sim na playstation hauwezi kuchoka

Anaweza kucheza siku nzima


Pia mkuu usisahahu kumlinda dhidi ya matumizi ya internet bila uangalizi na kikomo.

Sim za mkononi ni nzuri ila ukiwa umekomaa ubongo; lasivyo porn addiction ni risk kubwa saaana.

Hongera kwa malezi mazuri
 
kukulia kijijini ndio kuyajua maisha,
 
Hii ni experience ya kujiProud kweli, nothing to offer in our future just a wild life.
 
Waafrika huwa wanajiandaa kuishi maisha duni. Mtoto akipelekwa shule nzuri kila mtu anashangaa... roho ya umaskini.
Kuna rafiki yangu alishawahi niambia - kuna umuhimu wa kuinvest kwenye elimu ya watoto wako hata kama ni shule nzuri ukiweza kama Aga Khan etc. hata kwa kujinyima. Nikamuuliza kwa nini...alinielezea vizuri sana.. shule hizi zina watoto wa influencers na tukubali tukatae ni muhimu kuinvest kwenye social networking(ambayo inatofauti kubwa na socializing) maana mtoto wako anaanza kujijengea hazina ya watu muhimu akiwa mdogo. Na kumbuka lasting friendships and connections zinaanzia huko siyo chuo kikuu ambako ni too artificial.
 
Hii ni experience ya kujiProud kweli, nothing to offer in our future just a wild life.
Punguani.
Kwa kipande hiki cha childhood unafikiri ndio kimeaksi maisha yangu yote.
 
Ndio yeye ni low class inawezekana wewe high class unakojoa soda na kunya keki hongera mkuu.
 
Uko sahihi nina jirani nilikuwa nakaa alikuwa na binti mmoja tu akampeleka international school ada mamilioni nikauliza kwa nini na yeye mbona anaishi mtaani maisha ya kawaida akasema wanataka mwanae mbeleni aolewe na watoto wa matajiri sio vidume vya mtaani ni kweli alifanikiwa mwanae kaolewa uswisi na mswisi waliyesoma wote international school kule kuna watoto wa decision makers kwenye society hata mtoto Mara ingine kukosa kazi sio rahisi unakuta ni rafiki wa mtoto wa bakhreesa , mtoto wa bosi fulani nk tofauti na mtaani hao watoto wa decision makers hawapatikani shule za kawaida ndio maana wazazi wengine hujinyima sana ili watoto wao wasogee jaribu wakae na kufanya urafiki na watoto wa decision makers kwenye society
 
Kwanza hapa Tanzania kuna eneo lolote la kuitwa high class? 😂
Mmm kuna ukweli fulani mfano Dar unakuta mbezi beach au msasani au Masaki kote huko kuna watu wana mabanda ya kufuga kuku,ngombe na nguruwe kwenye makazi na watu wana magenge ya kuuza mboga na karanga za shilingi 100
 
Utotoni sisi Kama hujavunjika mkono kwa sarakasi basi wewe wa kishua
 
Aibu nimeona. Mimi
 

Mkuu unaongea as if wewe mwenyewe umekulia kwenye jamii tofauti na tuliyokulia sisi. Hiyo jamii unayoiponda hapa ndio ambayo imetukuza na kutu shape wengi wetu tuliopo humu leo. Hayo malezi unayoyakandia, ndio tuliyolelewa sisi na wewe, na mpaka leo tumeweza kujitambua na kuendesha maisha yetu! Kama yangekua mabovu kiasi hicho unachosema basi wengi wetu leo wala tusingekua humu jf tukijadili hii mada.

Hauwezi kuishi hapa duniani kama vile upo kwenye kisiwa, yaani ni wewe na watoto wako tu baas.. hayo yatakua maisha gani? Na je utaendelea kuishi kwenye hicho kisiwa mpaka lini? Kimaisha lazima uchangamane na watu wanaokuzunguka upende usipende na hao watu wata kuinfluence kwa njia moja ama nyingine.

Na mwisho, sisi wazazi tunafanya kile tunachoona kwamba ni bora kwa watoto wetu kulingana na uwezo wetu na uelewa wetu. Hakuna anaejua outcome ya malezi tunayowapa watoto itakuaje anaejua ni Mungu tu maana hakuna anaeweza kutamba kwamba yeye ni gwiji la malezi.
 

Nadhani tatizo lipo kwenye tafsiri ya neno SHIDA uliyoitumia. Sisi kilichotusaidia sio shida, ni mfumo wa maisha tuliyoishi wakati tukiwa wadogo, ambao kwa kipindi hicho wala hatukua tunaona kama ni shida ila ni maisha ya kawaida. Wewe ndio unaona kama hizo ni shida kwavile pengine wewe hukukulia mazingira hayo.

Na tunachosema sio kwamba mtoto apate shida, bali mtoto akuzwe kwenye mazingira halisi ya kitanzania. Lengo likiwa ni kumu expose mtoto kwenye mazingira yote ili incase ikija kutokea amejikuta katika mazingira ya aina hiyo asipate tabu ku cope.
 
Ningeshangaa kama huo mtaala wa primary ungekupig chenga.
Huu mtaala wa primary umemshinda dada angu kwa watoto wake wawili mpaka wanafika form two mdogo na form four mkubwa wa kiume. Dogo la kiume ni jeuri na dharau nyingi mpaka kufikia hatua ya kuwaambia walimu kuwa hawajui kiingereza sahihi kisa yeye na dada ake wamesoma international primary school baada ya kufauru Std. Seven na kupangiwa shule za serikali.
Kuna siku akiwa likizo alileta za kuleta nikamchapa bakora, baada ya hapo akaenda kunishtaki polisi kuwa eti mjomba kanichapa so waje kunikamata hapo akiwa form two😆. Polisi wakamwambia haya tangulia nyumbani sisi tunakuja.
Sasa wanaelekea elekea maana kila wakiwa nyumbani likizo lazima niwatembelee nakuwalizimisha wafanye baadhi ya kazi na si kumuachia mfanyakazi wa ndani kila kitu mpaka kufua nguo za hili dume. Wananichukia sana nikienda pale lakini hawana jinsi kwasababu kwasasa wako chini ya uangalizi wangu maana dada hayupo nchini kikazi.
Na watanyooka tu
 
Asante sana mkuu kwa huu uzi, nimescreenshot baadhi ya sehemu na kumtumia sister yuko ughaibuni na watoto wake wapo hapa nchini. Wakati yupo aliwalea kama mayai, Ila sasa wapo chini ya uangalizi wangu. Sijawahi ona eti Kuna tv ya sitting room alafu unanunua tv nyingine inakaa chumbani kwa mtoto wa kiume kwaajili yakuchezea PlayStation games akiwa likizo toka shuleni😬
Nimefungia laptop zao na PS now ni mwendo kumsaidia mfanyakazi baadhi ya kazi wakiwa likizo. Kuna siku niligombana na sister baada ya kusikia nimemchapa mwanae wa kiume tena vibakora vitatu tu😆. Alininunia the whole week, nikamwambia mimi siwalei Kama wewe ulivyokuwa unawalea bali nitawalea Kama sisi tulivyolelewa na wazazi wetu. Ilimchukua muda kukubaliana nami.
 
Kuna siku akiwa likizo alileta za kuleta nikamchapa bakora, baada ya hapo akaenda kunishtaki polisi kuwa eti mjomba kanichapa so waje kunikamata hapo akiwa form two😆. Polisi wakamwambia haya tangulia nyumbani sisi tunakuja.
Ingekuwa Ulaya au Marekani polisi wangekubeba kule viboko na vibao marufuku kwa mke au mtoto

Kule mtoto au mke kumtuma kitu mfano afue au kuosha vyombo kama wewe kidume unatakiwa kusema Sorry my sweetest honey I beg you I am under your feet can you wash vyombo tulivyolia chakula? Vinginevyo haoshi

Ma Mura wa Kikurya mupoooo?
 
Na sister yuko Finland sasa asitake watoto wake niwalee katika mazingira hayo. Kwanza ameshaanza kunielewa maana kazi wanafanya ila stage ya kuwapiga tangia nilipomchapa bakora akiwa form two huyu mkubwa wa kiume imewajengea hofu juu yangu kwahiyo nikiagiza kitu wanatekeleza ingawa sometimes naona kabisa wanafanya kwa shingo upande. Ni aibu mtoto wa kikeyupo form three now hata kusonga ugali hajui na kuandaa chakula mezani anaona ni usumbufu. Muda wote wakiwa home wanataka wakae mbele ya tv, wataangalia hapo mpaka jioni. Sasa maisha hayo sisi wenyewe hatujakulia, kwanini tuwaharibu Hawa watoto? Baadae mama yao asipokuwepo au uwezo alionao sasa ukapungua itakuwaje?
 
Safi sana,
Lakini rohoni wanakulaani kinoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…