Nilichelewa sana kujua kwamba Mungu Baba ni huyu Baba yangu mzazi aliyenizaa na kunilea. Mzee nisamehe kwa kuabudu miungu wengine

Yani hapo unataka kutumia kitabu cha hadithi ,kunifundisha kuamini kitu kisicho kuwepo kwa vitisho na ahadi.
 
Adam alipotenda dhambi Mungu alimwambia umetoka mavumbini na utarudi mavumbini. Maana yake atakufa. Na pia
Hakusema atampeleka Mbingun au Motoni.
 
Adam alipotenda dhambi Mungu alimwambia umetoka mavumbini na utarudi mavumbini. Maana yake atakufa. Na pia
Hakusema atampeleka Mbingun au Motoni.
Adamu ni hadithi ya kubuni tuliletewa na wakoloni miaka ya majuzi tu , tena babu zako wengine walikatwa mikono ili waziamini
 
Mkuu mpaka hapo nadhani umeelewa.
Hivyo vitabu vyenu vya sayansi vinasemaje kuhusu uumbaji wa Viumbe au ndio story zenu za volcano na matetemeko
Bado haithibitisha uwepo wa Mungu zaidi ya maneno ya kiimani ambayo bado yapo kwenye box la hayo mapokeo yako , akija pia wa imani nyingne nae atasema ya kwake.

Binafsi sina sababu ya kuamni hizo habari za Mungu , habari ya sayansi sijaizungumzia mimi.
 
Siku ukijua kuwa shetani pia ni huyo huyo baba yako uje kutuambia pia
 
Pamoja na yote unayopitia, nakusihi sana kwa neema ya Mungu shika sana ulichonacho asije muovu akakupotosha! Ulikuwa vizuri sana hapo mwanzo huku unakoelekea siko! Unapotea. Rudi kwa Yesu!
 
UGORO UKICHANGANYA NA BANANA LAZMA UWE MWEHU
 
Haya yote ni wewe unajaribu kumwelezea huyo Mungu kwa vile Hayupo na hajawahi kuwepo kujiongelea mwenyewe na kujielezea mwenyewe.
 
Viumbe vyote vilivyo hai vina DNA zinazofanana, ile “lugha ya kompyuta” au mfumo unaoongoza umbo na utendaji wa chembe.
Swali: Je, kufanana huko hakuwezi kuwa si kwa sababu vinatokana na mzazi mmoja, bali kwa sababu vina Mbuni mmoja?
Kwamba DNA yako na ya mbuzi zinafanana kwa vile pia mbuzi ni kiumbe hai?
 
Mungu hakukuumba kama robot, una uhuru wa kuchagua jema au baya.
Kama tuna uhuru wa kufanya jema au baya. Pia huyo Mungu ni Mbaya vilevile kwa kuruhusu watu kuwa huru kuweza kufanya mabaya.
Hiyo adhabu ya siku ya mwisho ni ipi?
Kulingana na maandiko yenu ya kidini ya Biblia. Adhabu ya siku ya mwisho ni moto wa milele.
 
Pamoja na yote unayopitia, nakusihi sana kwa neema ya Mungu shika sana ulichonacho asije muovu akakupotosha! Ulikuwa vizuri sana hapo mwanzo huku unakoelekea siko! Unapotea. Rudi kwa Yesu!
Yesu wa wapi?
 
Siku ukijua kuwa shetani pia ni huyo huyo baba yako uje kutuambia pia
Shetani hayupo, kama vile ambavyo Mungu hayupo. Ni hadithi tu za kubuni ili kumfunga au kumdhibiti binadamu asiweze kufikiria ipasavyo, awe mtumwa daima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…