Nilichojifunza kuhusu wanaume
Utakuwa Mama mzuri sama, nimeamka kwa shida sana leo kwenda kazini, ni kama umeniongelea, isingekuwa mke na watoto ningeacha kazi week iliyopita.
Mungu akutie nguvu. Katika kila gumu Mungu akakupe kulishinda. Pamoja na yote..tunawaombea. Mkafanikiwe
 
Wanawake wengi tumekuwa ni wazuri kwa upokeaji lakini ni wachache wa kushukuru.
Kwa mara ya kwanza nimeona mwanamke ameusema ukweli wa wanawake wote, sio kwamba mmekua wazuri wa kupokea wanawake mmeumbwa kupokea mnapokea mpaka mbegu kutoka kwetu wanaume ili mzae watoto bila mbegu hamuwezi kua wanawake maana ili mwanamke aitwe mwanamke inambidi azae, anazaaje? Anapokea mbegu kutoka kwa mwanaume,

Barikiwa kwa kujitambua na kulielewa hilo
 
Inawezekana dear ndio maana nikasema nlpamoja na madhaifu Yao lakini Bado wanamchango katika ustaw wa familia
Wapo wachache wanaojua kwamba hata ule ukorofi na mikiki-mikiki ya baba katika familia inasaidia sana kuifanya Familia iwe active (Ichangamke), iwe macho(awake) na muda wote familia hiyo ikae mkao wa tahadhari na kujihami kwani endapo mmoja wapo katika familia atajisahau na kuwa duwanzi au mzembe, atapambana na mkono wa baba.

Baba asipokuwepo Familia inakuwa ya baridi, imepoa, wanafamilia kuwa wanyonge n.k. na maadui wa familia (kutoka nje au ndani ) huibuka na kuanza kuinyanyapaa familia, kuwaonea na hata kuwadhulumu baadhi ya mali na haki zao. Lakini akiwepo Baba hawatothubutu kufanya ushenzi kama huo kwani wanajua ni nini kitatokea.
 
Maisha yalikuwa tofuti sana na kipindi baba yangu yuko hai nikaona ni kiasi gani mzee aliteseka kuhakikisha tunaishi vizuri na tunakuwa salama sisi na mama yetu nimejisikia kuwasemea leo.
Kuna wakati wanaume wanapitia mambo mengi magumu kwaajili ya familia zao ama watu wanaowapenda hasa katika utafutaji wa riziki. Kuna walio na kazi za halali, kuna wengine wahatarisha hata maisha yao Ili kuhakikisha mambo yankuwa sawa lakini kitu kizuri ni kwamba sio wasimualiaji wazuri wa mahangaiko na mateso yao wakati wanafnya hayo.[emoji1545][emoji818][emoji817][emoji2827]
Ni Bonge la insha
 
FB_IMG_16735423308032642.jpg

sophy27 wetu huyoo😘😘
 
Back
Top Bottom