PostGE2025 Nilichokiona Jana Kimeniogopesha. Watanzania Wamebadilika Sana!

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Sitakuumiza Kamwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2025
Posts
466
Reaction score
1,457
Jana mida ya saa tisa hivi mchana. Wapasua matofali wetu wakawa wanafanya doria na lihelikopta lao moja kuukuu limechoka choka hivi. Wanapita kwa chini chini mpaka wanaonekana makomandoo wao wamekaa milangoni na mabunduki yao makubwa makubwa...

Ilikuwa ni maeneo ya soko; na watu wakawa wametoka nje ya soko wakawa wanawaangalia. Mara watu wakaanza kuzomea. Tena wengine akina mama watu wazima. Hamtutishi kwa lo lote! Wapuuzi nyie. Kama kweli wanaume shukeni hapa wasaliti wakubwa nyinyi.... Vijana ndiyo kabisasaa. Wakawa wanaporomosha matusi. Lihelikopta likaendelea kuzunguka!

Nilipoingia barabarani mara paap nikakutana na mtiti wa CDF nadhani. Landcruisers 4 zina namba za JW vioo tinted vimulimuli kama vyote na bendera zinapepea. Mbele na nyuma kuna open Defenders wamekaa wapasua matofali wamevaa full kivita mpaka nyuso wamefunika. Na penyewe mambo yakawa ni yale yale. Watu wakaanza kupiga miluzi na kuzomea. Haooo wakatokomea zao.

Nilitoka pale nikiwa na mawazo tele. Watanzania hawa wamekuwaje hawa? Ina maana hawaogopi tena? Kwa nini uhusiano kati ya raia na wapasua matofali umezorota namna hii? Wanetu wapendwa hawa. Walinzi wa mipaka na uhai wetu. Mashujaa wetu. Majuzi tu hapa walikuwa admired na kupendwa sana lakini sasa wakipita huku mitaani watu ni kusonya tu na kutema mate. Je, D9 watasimama katika zamu yao kama walinzi wa amani na raia au watawatelekeza tena raia wauwawe kama kondoo pamoja na kuahidi maandamano ya amani?

Naam! Mambo yamebadilika . Hawa ni Watanzania wapya . Hawaogopi tena wala hawatishwi na nywi nywi nywi wala nywa nywa nywa. Viongozi wetu inabidi walitambue hili na watumie dialogue na ushawishi badala ya vitisho na maguvu tu (kama ambavyo askofu Bagonza amekuwa akishauri mara Kwa mara). Kwa hakika hizi ni zama mpya! Hata Mzee Kenyatta aliyewahi kusema kuwa eti Watanzania ni sawa na maiti akifufuka leo atashangaa sana!
 
Hao wanajeshi nimewadharau sana, wanaleta mahelikopta yaloyochakaa, wakati watu walikuwa wanatekwa na hawajawahi kukemea wala kukataza. Watu wameuwawa mbele yao na hawajotoa msaada wowote wa maana, sana sana mwizi wa kura ambao hata wao wanaujua ukweli huo, akaapishiwa kambini kwao.
 
Msaliti wa Watanganyika!
Screenshot_20251126-192538~2.png
 
Jana mida ya saa tisa hivi mchana. Wapasua matofali wakawa wanafanya doria na helikopta yao moja hivi. Wanapita kwa chini chini mpaka wanaonekana makomandoo wao wamekaa milangoni na mabunduki yao makubwa makubwa...

Ilikuwa ni maeneo ya soko; na watu wakawa wametoka nje ya soko wakawa wanawaangalia. Mara watu wakaanza kuzomea. Tena wengine akina mama watu wazima. Hamtutishi kwa lo lote! Wapuuzi nyie. Kama kweli wanaume shukeni hapa wasaliti wakubwa nyinyi.... Vijana ndiyo kabisasaa. Wakawa wanaporomosha matusi. Helikopta ikaendelea kuzunguka!

Nilipoingia barabarani mara paap nikakutana na mtiti wa CDF nadhani. Landcruisers 4 zina namba za JW vioo tinted vimulimuli kama vyote na bendera zinapepea. Mbele na nyuma kuna open Defenders wamekaa wajeda wamevaa full kivita mpaka nyuso wamefunika. Na penyewe mambo yakawa ni yale yale. Watu wakaanza kupiga miluzi na kuzomea. Haooo wakatokomea zao.

Nilitoka pale nikiwa na mawazo tele. Watanzania hawa wamekuwaje hawa? Ina maana hawaogopi tena? Kwa nini uhusiano kati ya raia na wapasua matofali umezorota namna hii? Wanetu wapendwa hawa. Walinzi wa mipaka na uhai wetu. Mashujaa wetu. Majuzi tu hapa walikuwa admired na kupendwa sana lakini sasa wakipita huku mitaani watu ni kusonya tu na kutema mate. Je, D9 watasimama katika zamu yao kama walinzi wa amani na raia au watawatelekeza tena raia wauwawe kama kondoo pamoja na kuahidi maandamano ya amani?

Naam! Mambo yamebadilika . Hawa ni Watanzania wapya . Hawaogopi tena wala hawatishwi na nywi nywi nywi wala nywa nywa nywa. Viongozi wetu inabidi walitambue hili na watumie dialogue na ushawishi badala ya vitisho na maguvu tu. Kwa hakika hizi ni zama mpya!
Sasa ukiwa na helicopter si unaons wahalifu vizuri ata ukichapa shaba unatarget vizuri kabisa
 
Ile heshima walikuwa nayo imeingia doa

They know wame side na upande dhalimu. They are part of the gang now
 
Back
Top Bottom