Nilichokiona mara ya kwanza baada ya kuagiza kitu ebay

Kuna watu wengi saana wanatamani kuagiza vitu ebay lakini wanakosa muongozo namna ya kuagiza mnaonaje wazoefu nkatoa muongozo japo kidgo tu.
Japo miongozo iliopo jf kama ni ya zamani kidgo na ukipitia pia kama ziko complicated saana
Cha kwanza Kabisa wawe na account huko ebay na muhimu wewe na PayPal ndio tamu maana hizi kadi za tigo na voda mda mwingine zinaleta usumbufu sana
Na mzigo wako ulifanya kazi vizuri mpaka leo? Mana mm niliwahi kuagiza SSD kupitia kikuu ila haikufanya kazi.
Duh Bora uagize za AliExpress au ebay mkuu
 
Ali express ndio bei rahisi na nyepesi zaidi,fungua account
 
AliExpress inanishinda kabisa, kuna wakati nikisearch bidhaa yanakuja makorokoro ambayo hata siyaelewi. Ila ebay utakachosearch ndio utakacholetewa.
Au kuna sehemu nakosea?
Haina shida mkuu iko sawa tu,halafu huko ebay unauziwa vifaa vingine kutoka hukohuko china kwa bei ya juu wakati aliexpress ungeipata kwa bei ya chini,mfano kaangalie bei ya frem ya miwani pure titunium kwa bei ya ebay na aliexpress with same quality utaona tofauti kubwa sana katika bei, pia shiping cost ebay iko juu compared to aliexp.pia alexp wana agent ambao unachukua mzigo free bila charger walio chini ya speedof wakati ebay lazima upitie posta na lazima posta wakucharge storage achilia mbali ishu ya kodi
 
Haina shida mkuu iko sawa tu,halafu huko ebay unauziwa vifaa vingine kutoka hukohuko china kwa bei ya juu wakati aliexpress ungeipata kwa bei ya chini
Sawa kiongozi, nisaidie kucheki hii kitu AliExpress halafu unipe link, nitashukuru sana ukinisaidia.



pia alexp wana agent ambao unachukua mzigo free bila charger walio chini ya speedof
Pia nitashukuru sana kama utanielekeza vizuri kuhusu hii ishu ya kuchukua mizigo kupitia Speedaf, unatumiwa mzigo popote ulipo?
Hawa Speedaf wana ofisi mikoa tofauti tofauti hapa Tanzania?
Pia nawezaje kujua kama muuzaji anamtumia huyo agent (speedaf)?
 
Kuna watu wengi saana wanatamani kuagiza vitu ebay lakini wanakosa muongozo namna ya kuagiza mnaonaje wazoefu nkatoa muongozo japo kidgo tu.
Japo miongozo iliopo jf kama ni ya zamani kidgo na ukipitia pia kama ziko complicated saana
Mimi nimewahi kuagiza simu zaidi ya mara nne, saa za mkononi mara tatu saa niliyovaa sasa hivi niliagiza online, niliwahi kuagiza smart watch, earpods nk.

Muongozo ni wewe kujisajili kwenye app husika kwa kuweka taarifa zako sahihi, mfano wa taarifa ni jina lako, address yako ya posta, namba ya simu nk.

Kuhusu namna ya kufanya malipo napo ni rahisi tu, mfano mimi nimewahi kufanya malipo kupitia MasterCard kwa maana ya kadi yangu ya NMB, sasa hii ya NMB inabidi uende kwenye branch ili waiwezeshe kufanya malipo online. Visa card ya CRDB yenyewe imeshawezwesha kufanya miamala online , uchaguzi ni wako.

Nimeona mdau amegusia swala mitandao kama tigo au voda,, huko sina utaalamu nako nazungumzia kile nimekiishi. Mtandao ambao nimeagiza bidhaa ni AliExpress huko eBay sijawahi kuagiza. Mwanzoni kutokana na uoga nilikuwa naagiza tuvitu tudogo tudogo na tunafika fresh tu, baadae nikaanza kuagiza items mpaka za 700K.

Ukizoea kuagiza online raha sana utajikuta hata soksi unaagiza online.. karibuni kwa swali au nyongeza ya maelezo ambapo hujaelewa. Kuagiza bidhaa inawezekana wala usihofu.


NB: Sio lazima uwe na sanduku la posta hata ukiandika la mtu mwingine au taasisi unayofanyia wewe andika physical address ya mahali ulipo mfano Bagamoyo, kumbuka mahali ulipo pawe na posta, kwisha habari
 
Okay so ni recommendable? Kuna bidhaa natamani kuagiza, ila sijapata app sahihi ya kutumia, kikuu walinicheleweshea bidhaa zangu nikakata tamaa kabisa ya kuagiza vitu online
Tena hao kikuu wala usirudie kuna jamaa aliagiza tairi za Alteza akaletewa kitu tofauti, wale ubabaishaji mwingi, kwanza hao kikiuu wanachukua bidhaa kwa kina AliExpress, eBay, hata Alibaba. Achana nao agizia AliExpress au hata eBay
 
kuna member humu anaitwa Ruble nilikua namlipa ananiagizia vitu mpaka maksoko ya Uingereza na vinafika salama. anajua sana hata hizo ebay na masoko mengine lakini mara ya mwisho namuunganisha na mtu akasema amewacha shughuli hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…