Okay, mimi nafahamu kuagiza bidhaa kwa kutumia mtandao wa ebay.
Hatua ya kwanza kabla haujaanza kuagiza bidhaa ebay, unatatakiwa ujiunge na mtandao wa ebay, yaani ufungue akaunti ili uweze kufanya manunuzi.
Utajisajili hapa kwenye hii link.
Security Measure
Hatua ya pili, baada ya kuwa umejisajili. Utatakiwa kuweka taarifa za mahali ambapo unahitaji mzigo utumwe endapo utafanya manunuzi.
View attachment 3101114
Ukishakamilisha usajili utaingia kwenye akaunti yako, kisha utabonyeza hako kamshkaji nilikokazungushia duara.
Itakuletea hivi.
View attachment 3101115
Ikikuletea hivi utabonyesha hapo palipoandikwa Account, nimezungushia duara nyekundu.
Ukibonyeza hapo, itakuleta hapa
👇👇👇
View attachment 3101118
Hapa utajaza taarifa zako binafsi kama vile email na namba za simu, pia sehemu unapoishi na Zip Code, Zip Code utagoogle tu, kwa mfano kama unaishi Mtama, utaenda google utaandika "Mtama Zip Code" zitakuja zip code za Mtama, utachagua iliyosahihi kulingana na eneo unaloishi.
Ukishamaliza hiki kipengere, utarudi tena hapo kwenye kimtu, utabonyeza tena kwenye neno Account, kisha utabonyeza kwenye payments (duara nyekundu).
Yaani hapa 👇👇👇
View attachment 3101121
Hapo utapewa njia za malipo, utaweka namba zako za kadi ya benki, kama unatumia Paypal unaweza pia kuweka taarifa zako za PayPal(email).
Ukikamilisha hivi vipengere vyote unakuwa upo tayari kununua bidhaa yoyote katika mtandao wa ebay.
Hatua ya pili, kutafuta vitu unavyotaka kununua.
Ebay homepage utakutana na hii sehemu iliyozungushiwa duara nyekundu.
View attachment 3101142
Hapo andika kitu unachokitaka. Kwamfano tunaandika "laptop", kisha tunasearch.
Watatuletea matokeo ya "laptop" kama hivi. 👇👇👇
View attachment 3101152
Ukiangalia hapo juu unaona kuna duara nyekundu nimezungusha, ina maneno All, Auction, Buy It Now. Yeah, uzuri wa ebay ni kuwa kuna vitu huwa vinauzwa kwa mnada, kwa hiyo kama unataka kuona laptops ambazo zinauzwa kwa njia ya mnada utabonyeza hapo palipoandikwa Auction, kama unataka vitu vinavyouzwa kawaida utabonyeza hapo palipoandikwa Buy It Now, kama unataka kuona vitu mchanganyiko utaacha hapo kwenye All.
Tufanye umechagua bidhaa ambayo inauzwa kawaida, sio mnada yaani Buy It Now.
Itakuleta hapa 👇👇👇
View attachment 3101173
Utabonyeza hapo palipoandikwa Buy It Now.
Itakuleta kwenye sehemu inayoitwa Checkout, hapa utathibitisha mahali unapotaka mzigo utumwe, na njia unayotaka kutumia kufanya malipo utaithibitisha ama kuibadilisha hapa.
Itakuwa kama hivi 👇👇👇
View attachment 3101174
Ukishakubaliana na hizo taarifa hapo juu, utabonyeza hapo palipoandikwa "confirm and pay"
Tufanye umechagua bidhaa ambayo inauzwa kwa njia ya Auction.
Itakuletea hivi 👇👇👇
View attachment 3101156
Kama bidhaa umeipenda na unataka kuipigania, utabonyeza hapo palipoandikwa place bid. Ukishabonyeza hapo utaingiza kiasi ambacho upo tayari kutoa, lakini kumbuka kiasi utakachoingiza ni lazima kiwe kikubwa kuliko mtu wa mwisho. Nadhani unaelewa namna mnada unavyofanya kazi. Ukishinda mnada utatakiwa kuilipia bidhaa.
🤔🤔🤔Pia bila kusahau, ebay wana kitu inaitwa eBay money back guarantee, yaani hapa mzee ikitokea umepokea mzigo na ukakuta upo tofauti na maelezo na picha za muuzaji, una uwezo wa kufungua madai na kurudishiwa pesa zako.
eBay Money Back Guarantee
Aisee, mkongwe nimejitahidi sana kukuelekeza japo kuna mambo mengi sana pia nimeyaacha, kuna mengine utajifunza kwa njia ya AAANHA KUMBE CONCEPT 😂😂😂
Kama kuna sehemu haujaelewa utauliza swali, tutasaidiana na wadau wengine kukujibu.