Nilichokiona mara ya kwanza baada ya kuagiza kitu ebay

Ebay!

Mzigo kama umeagiza USA, ama Ulaya kuna mingine utalipia pesa ya Posta na baada ya kulipia watakwambia subiria mtu wa TRA aje akufanyie makadirio ya kodiπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Na mzigo wako ulifanya kazi vizuri mpaka leo? Mana mm niliwahi kuagiza SSD kupitia kikuu ila haikufanya kazi.
Nimeagiza vitu kupitia kikuu mda sasa, nimegundua kuwa hizo SSD, flash na memory cards nyingi ni magumashi sana kutoka kikuu. So far ni flash moja tu ilifanya kazi, memory cards, baadhi ya flash na ssd hadi leo zipo hazifanyi kazi.
 
Ninachoona mimi mzigo ni afadhali upitie Posta ambayo iko nje ya mji wa Dar Es Salaam, nilipokuwa naagiza na mizigo ikipitia Dar Es Salaam ilikuwa ni lazima nilipie lakini tangu nimeanza kupitishia Posta ya huu mkoa ninaoishi sijawahi kulipia.
Mkuu unatuchomesha sasa
 
siku nyingine ni MARUFUKU kuagiza kwa kutumia soko mjinga la kuitwa Kikuu. we huoni jina lenyewe limekaa kidwanzi.
Sijawahi kukutana na changamoto yoyote kupitia kwao, labda kuchelewesha mzigo, nayo sio mara zote. Hawajawahi kunitapeli
 
Nimeagiza vitu kupitia kikuu mda sasa, nimegundua kuwa hizo SSD, flash na memory cards nyingi ni magumashi sana kutoka kikuu. So far ni flash moja tu ilifanya kazi, memory cards, baadhi ya flash na ssd hadi leo zipo hazifanyi kazi.
Kila nikichomeka SSD kwenye pc inanitaka nii-format nikaona ujinga huu nikampa dogo afanye kama rula shulen
 
Sijawahi kukutana na changamoto yoyote kupitia kwao, labda kuchelewesha mzigo, nayo sio mara zote. Hawajawahi kunitapeli
Labla ndo hvy inategemea unaagiza nn
 
Cha kwanza Kabisa wawe na account huko ebay na muhimu wewe na PayPal ndio tamu maana hizi kadi za tigo na voda mda mwingine zinaleta usumbufu sana

Duh Bora uagize za AliExpress au ebay mkuu
si mtumie MasterCard za bank tu mbona ni rahisi zaidi mpk mtapetape..πŸ˜…
 
Mzee wa Series naomba mwongozo jinsi ya kuanza kufanya manunuzi ebay
Cha kwanza kuwa na kadi za kulipia mtandaoni kama MasterCard za bank PayPal afu hapo fungua account hapo ebay

Cha pili
Nunua kwa muuzaji anayekubaliwa na weteja wengi.

Utajuaje kama muuzaji anakubalika sokoni na anauzoefu wa kuuza vitu kwenye mtandao? Rahisi! Kwa mfanounataka kununua saa Ebay au kitabu cha electrniki (PDF) kwenye Amazon, chini ya hiyo bidhaa iliyoichagua utaona maoni ya watu walionunua kabla yako

Cha tatu
Chagua namna ya kutumiwa mzigo wako.

Unatakiwa kuchagua namna kutumiwa mzigo wako ambayo itakuwa rahisi kwako kuupata. Gharama za kutuma mzigo zitaoneshwa pale kwenye mtandao na muda wa kufika kwa kila gharama.

Cha nne
Hakikisha muuzaji anahudumia eneo ulilopo.

Baadi ya wauzaji huchagua nchi au miji wanayoweza kutuma mizigo na wengine huuza dunia nzima. Taarifa hizi huwekwa chini ya bidhaa unayotaka kununua , hii itakusaidia kuokoa muda kuondoa usumbufu usio wa lazima.
 
Uoga ni pale ambapo unashindwa kuelewa hii ni og au feki kwa maana pale ni mwendo wa picha tu afu kuna bidhaa unakuta bei iko chinii mno mpk unahisi kama ni feki
 
Yaani sasa tupe elimu jinsi ya kuagiza bidhaa bila usumbufu. Mkuu sisi wengine bado tupo kwenye mfumo wa 'Pager' yaani kama vile VW Beetle, Ford Cortina, Morris Marina, n.k.
Okay, mimi nafahamu kuagiza bidhaa kwa kutumia mtandao wa ebay.

Hatua ya kwanza kabla haujaanza kuagiza bidhaa ebay, unatatakiwa ujiunge na mtandao wa ebay, yaani ufungue akaunti ili uweze kufanya manunuzi.
Utajisajili hapa kwenye hii link.
Security Measure

Hatua ya pili, baada ya kuwa umejisajili. Utatakiwa kuweka taarifa za mahali ambapo unahitaji mzigo utumwe endapo utafanya manunuzi.


Ukishakamilisha usajili utaingia kwenye akaunti yako, kisha utabonyeza hako kamshkaji nilikokazungushia duara.

Itakuletea hivi.

Ikikuletea hivi utabonyesha hapo palipoandikwa Account, nimezungushia duara nyekundu.
Ukibonyeza hapo, itakuleta hapa
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Hapa utajaza taarifa zako binafsi kama vile email na namba za simu, pia sehemu unapoishi na Zip Code, Zip Code utagoogle tu, kwa mfano kama unaishi Mtama, utaenda google utaandika "Mtama Zip Code" zitakuja zip code za Mtama, utachagua iliyosahihi kulingana na eneo unaloishi.
Ukishamaliza hiki kipengere, utarudi tena hapo kwenye kimtu, utabonyeza tena kwenye neno Account, kisha utabonyeza kwenye payments (duara nyekundu).
Yaani hapa πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Hapo utapewa njia za malipo, utaweka namba zako za kadi ya benki, kama unatumia Paypal unaweza pia kuweka taarifa zako za PayPal(email).
Ukikamilisha hivi vipengere vyote unakuwa upo tayari kununua bidhaa yoyote katika mtandao wa ebay.

Hatua ya pili, kutafuta vitu unavyotaka kununua.
Ebay homepage utakutana na hii sehemu iliyozungushiwa duara nyekundu.

Hapo andika kitu unachokitaka. Kwamfano tunaandika "laptop", kisha tunasearch.

Watatuletea matokeo ya "laptop" kama hivi. πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Ukiangalia hapo juu unaona kuna duara nyekundu nimezungusha, ina maneno All, Auction, Buy It Now. Yeah, uzuri wa ebay ni kuwa kuna vitu huwa vinauzwa kwa mnada, kwa hiyo kama unataka kuona laptops ambazo zinauzwa kwa njia ya mnada utabonyeza hapo palipoandikwa Auction, kama unataka vitu vinavyouzwa kawaida utabonyeza hapo palipoandikwa Buy It Now, kama unataka kuona vitu mchanganyiko utaacha hapo kwenye All.

Tufanye umechagua bidhaa ambayo inauzwa kawaida, sio mnada yaani Buy It Now.
Itakuleta hapa πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Utabonyeza hapo palipoandikwa Buy It Now.
Itakuleta kwenye sehemu inayoitwa Checkout, hapa utathibitisha mahali unapotaka mzigo utumwe, na njia unayotaka kutumia kufanya malipo utaithibitisha ama kuibadilisha hapa.
Itakuwa kama hivi πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Ukishakubaliana na hizo taarifa hapo juu, utabonyeza hapo palipoandikwa "confirm and pay"

Tufanye umechagua bidhaa ambayo inauzwa kwa njia ya Auction.
Itakuletea hivi πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡


Kama bidhaa umeipenda na unataka kuipigania, utabonyeza hapo palipoandikwa place bid. Ukishabonyeza hapo utaingiza kiasi ambacho upo tayari kutoa, lakini kumbuka kiasi utakachoingiza ni lazima kiwe kikubwa kuliko mtu wa mwisho. Nadhani unaelewa namna mnada unavyofanya kazi. Ukishinda mnada utatakiwa kuilipia bidhaa.

πŸ€”πŸ€”πŸ€”Pia bila kusahau, ebay wana kitu inaitwa eBay money back guarantee, yaani hapa mzee ikitokea umepokea mzigo na ukakuta upo tofauti na maelezo na picha za muuzaji, una uwezo wa kufungua madai na kurudishiwa pesa zako.

eBay Money Back Guarantee

Aisee, mkongwe nimejitahidi sana kukuelekeza japo kuna mambo mengi sana pia nimeyaacha, kuna mengine utajifunza kwa njia ya AAANHA KUMBE CONCEPT πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kama kuna sehemu haujaelewa utauliza swali, tutasaidiana na wadau wengine kukujibu.
 
Kamanda bila kupepesa macho nakupa 5🌟 umejitahidi saana na kupitia hii comment yako kuna watu wataanza kufanya manunuzi
 
Kamanda bila kupepesa macho nakupa 5🌟 umejitahidi saana na kupitia hii comment yako kuna watu wataanza kufanya manunuzi
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Hapo tumeacha masuala ya tracking number, na vitu vingine vidogo vidogo ambavyo ni rahisi kuvijua akishapita hizo hatua zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…