Nilichokiona mara ya kwanza baada ya kuagiza kitu ebay

Natumia NMB hiyo huduma ya Paypal unajiunga au?
 
Natumia NMB hiyo huduma ya Paypal unajiunga au?
Hao PayPal ni kama mtu wa kati kwenye kufanya malipo, wanasaidia kulinda taarifa zako za kibenki kupitia kadi yako.

Unachokifanya unajiunga na PayPal, halafu unawaruhusu wawe wanatoa pesa kwenye akaunti yako pale unapofanya malipo mtandaoni, kwahiyo badala ya kuandika taarifa za kadi yako unapofanya manunuzi unaandika email uliyotumia kujiandikisha Paypal.

Pia faida nyingine ya PayPal ni kuwa ikitokea umepokea mzigo wa ovyo, PayPal watabeba jukumu la kurudisha pesa yako kutoka kwa muuzaji aliyekufanyia uhuni.

Jisajili PayPal hapaπŸ‘‡πŸ‘‡
PayPal
 
Prices zimewekwa in US DOLLARS kama nini fedha in TSH inakuwaje hapo
 
Ebay!

Mzigo kama umeagiza USA, ama Ulaya kuna mingine utalipia pesa ya Posta na baada ya kulipia watakwambia subiria mtu wa TRA aje akufanyie makadirio ya kodiπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kwahiyo wakiona USA baby πŸ‡ΊπŸ‡ΈπŸ‡ΊπŸ‡ΈπŸ‡ΊπŸ‡Έ umekwisha!?
 
Tafuta bidhaa ukiiipenda angalia reviews za watu walionunua hiyo bidhaa kujiridhisha la sivyo baadhi ya bifhaa ambazo hakuna reviews ikikufikia unaweza ukajicheka mwenyewe.
Hakika, hili ni jambo la msingi sana, unakuta muuzaji hana review hata moja, halafu unaenda tu kichwakichwa unanunua bidhaa yake. Lazima ule za kichwa.

Pia kuna uhuni mwingine nimeuona eBay, unaweza kukuta iphone 14 Pro inauzwa. Kwenye picha limewekwa boksi la simu jipya kabisa. Ukiangalia bei ni kitonga mpaka macho yanakutoka.
Kichwa kimeshapagawa na Iphone ya bei chee, na uvivu wa kusoma maelezo unakurupuka unafanya malipo kumbe wahuni wamekuwekea boksi tupu, na kwenye maelezo ya bidhaa katikati au mwisho unakuta wamekuchomekea neno EMPTY BOX.
 
Very useful.
 
Asante mkuu!
 
Sio mbaya, ni kama Bi Mkubwa alivyosema, haizidi 10000.
Hii sio kodi ila ni gharama za usafirishaji za posta. Inawezekana wanapima uzito wa kitu ili kujua unatakiwa ulipie shilingi ngapi. Shirika la posta halisafirishi bidhaa bure. Ukiona hujalipa chochote posta basi ujue ni bahati tu unaipata.
Kuhusu kulipa kodi ya kitu ulichoagiza inategemea kama TRA wamehusishwa au la. Ikiwa wamehusishwa na posta ujue lazima ulipe kodi na usishangae au kuhuzunika maana ni kawaida. Tena unaweza walipa posta pesa yao na TRA pesa yao.
Kwa kuhitimisha tu ni kuwa kuna tofauti kubwa kati ya gharama za posta kukusafurishia mzigo wako toka posta makao makuu hadi posta yako wewe uliopo na kodi(TRA). Hivi ni vitu viwili na taasisi mbili tofauti.
 
Mkuu naona aliexpress vitu vingi ni kama fake tofauti na ebay
 
Ebay & Amazon via DHL huduma yao safi kabisa....nimeanza kutrade nao 2014.
 
Tafuta mtu pale awe anakutolea

Ila mingi kama sim ina makadirio ya kodi hadi laki 3 kitegemea na sim
 
Mkuu naona aliexpress vitu vingi ni kama fake tofauti na ebay
AliExpress ni Wachina!
Products za Wachina zinafahamika zilivyo. Ila ukiwa makini ninaamini unaweza kupata kitu kizuri.
Uzuri wa soko la China gharama za shipping ziko chini sana, nahisi serikali ya China inawasaidia wafanyabiashara wa China kwenye upande wa usafirishaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…