geraldkowero1
JF-Expert Member
- Jul 5, 2014
- 1,838
- 646
Amani ya Mungu iwe nanyi wapendwa, naomba ushauri.
Ni mume niliempenda nilemuheshimu na kumfanyia kila kitu anachostahili mwanaume kufanyiwa kumfariji wakati wa magumu na kuwa nae wakati wa furaha, naye mwenyewe aliyakubali yote niliyokua nafanya.
Sasa juzi kachelewa kurudi nyumbani na sikumuuliza sababu akasema anaomba ale chakula ndipo aoge, nikapakua tukala kisha nikamuandaa akaoge ndipo nilipokuta kwenye nguo za ndani uchafu wa kutoka kujamiana na mwanamke.Nilipomuuliza akajibu fikiria utakachoamua kufikiri.
Naomben ushauri kwani hapa nasikia mwili wote unauma, kichwa kinataka kupasuka.
Ndio maana kakuambia fikiria utakavyoamini iwe juu yako mwenyewe. Wewe kwa hatua ya kwenda kukagua nguo yake ya ndani ulishamwazia mwenzio vibaya. Yeye mara ngapi ameshakagua nguo yako ya ndani unapofika tu nyumbani au ukienda kuoga? Si mnavulia huko huko bafuni? Hakupendezwa na tabia hiyo mpya ndio maana kakupa jibu hilo. Hata hivyo sio lazima awe ametembea nje ya ndoa kwani kuna wanaume wengine matamanio yakizidi wazungu hutoka tu. Hapo itakubidi usamehe bure tu nae aache ubwege awe anaingia bafuni na kyupi kwani haya mataulo yakiachia hujafika bafuni ni senema nyingine uswahilini.