Kwa nini ufe na kitu rohoni, hivi ungemwambia huna bajeti ya rafiki yake unadhani ungeonekana masikini au unadhani ungekuwa umejishusha?
Back in the days nimewahi kuwa katika mazingira ambayo mkitoka kila mtu analipia chake, au anakuambia kabisa you'll take care of drinks na mimi vyakula. Hakuna kupeana stress wakati mmetoka kufurahia. Najua kwa maisha yetu ni ngumu japo wapo wachache wanajitahidi, ila usiletewe mzigo wa kundi la watu uwalishe na kuwanywesha in the name of outing, unless of course mlipanga kutoka as a group.
Principle iko hivi, ukiniita manake una budget yangu, nikikuita manake nina budget yako.