Nilidhani ukiingia mbuga ya wanyama Unaona wanyama kirahisi kumbe napo tabu tupu

Taratibu za kwenda Tarangire au Ngorongoro zikoje
Na kadirio ya gharama
 
Nusu tubutuliwe na Tembo hapo Tarangire sina hamu nako
Hapo kuna Tembo wakubwa sana mdogo wangu halafu hawapendi kelele kabisa. Kuna kijamaa kilikuja na gari yake sasa tembo anamfuata yeye anakaza atoki wacha tembo asinye sinye gari ..ilikuwa ni balaa mzee..
 
Kuna tukio la watoto wa tatu wa kimasai kuuliwa na simba juzi kati hapa walikuwa wanatoka shule.
 
Nipe connection ya kampuni hizo kubwa
 
Yale mambo ya discovery channel au chanal yoyote zikiwemo cnn aljazira bbc ni chanal ambazo zinarusha matokeo hamna kabisa tunaliwa pesa zetu na mfumo huu wa cable
 
Watanzania wenzangu tujifunze tofauti ya
Hifadhi za wanyama pori
Na
Bustani za wanyama..

Hifadhi za wanyana maana yake ni maeneo yakiotengwa na kuwaacha wanyama waishi katika asili yao bila kuingiliwa na binaadam.
Hivyo wanaishi mazingira yao ya asili..
wanyama wa maeneo haya huwa wanaishi wanavyotaka na wakitaka wao kwa asili zao wanakua wanajificha au kukaa maeneo ambayo sio rahisi kuonekana kwani ni mbali na mizunguko ya binaadam..

Bustani za wanyama ni sehemu wanyama wanahifadhiwa kwa ajili ya kwenda kuangaliwa hivyo hiwa rahisi kuwaona na mara nyingi huwa kwenye eneo dogo lililo wekwa uzio ..


So ukitaka uhakika wa kuona wanyama nenda kwenye bustani .. uwaone wanyama wanavyofugwa but ukitaka kuona wanyama wanaishije katika asili zao nenda Katika hifadhi za wanyama…
 
Asante kwa ushauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…