Nilidhani ukiingia mbuga ya wanyama Unaona wanyama kirahisi kumbe napo tabu tupu

Sikuifurahia ile safari..... Nakumbuka kabisa. Nilijiona nimekwenda kuchoka zaidi.
 
Afadhali lakini ulipata hewa mpya huko
 
Saadani kule kwa wanaotaka kuona Twiga, Tembo na Ngiri hao wapo tele na vingedere. Pia kule mtoni kuna viboko na Mamba wanyama wengine ni shughuli kuwaona.
 
Mkuu labda ulikuwa na bahati mbaya tu siku hiyo... lakini kati ya mbuga zote nchi hii ngorongoro crater ndo mahala ambapo unapokwenda una uhakika kwa asilimia zaidi ya 90 wa kuona simba Tembo pamoja na faru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbuka unaenda kuangalia wanyama sio kumtembelea mtu ambaye atakaa kusubiri ujio wako kwa hiyo bajeti ya kutosha ni muhimu, sijui ni vyuma kukaza huko mbugani siku hizi ni ngumu kuwakuta wanyama wamejilaza tu wakisubiri watalii mje mpige picha
 
kweli Adventure is not for everyone ... usiende tena had ujue maana ya advnture

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…