Natamani nisingezaliwa
Senior Member
- Sep 9, 2024
- 112
- 265
- Thread starter
- #141
Sio ndugu pekee wa nje hata wa ndani yaan kama kaka na mdogo wake pia umakini uwepo huwezi jua wametolea nje wanaenda kufundishana na wazazi hawajuiDah!
Nakumbuka mnamo mwaka 95 tulienda mahali kufanya shughuli Kwa kipindi Cha miezi kadhaa. Tulikua na mwenzangu akinizidi kama miaka miwili hivi. Siku moja usiku tumelala katika mazungumzo ya kutafuta usingizi baada ya shughuli za kutwa nzima, ghafla akasema tupigane kazi Kwa zamu, nimuanze yeye Kisha itafuatia zamu yangu. Mazungumzo yaliishia hapo. Nilichefukwa sana, kwanza hata mahusiano na mwanamke sikuwa nimewahi kujaribu. Pili, nilikua mtu wa ibada sana.
Ndio siku hizi natafakari huenda yule mwenzangu alikua ameshaanza haya mambo kitambo, alikua mziefu. Aliweka bayana kabisa nimuanze yeye. Inamaana hata kama ningekataa kusinfekua na tatizo lakini yeye alikua ameridhia.
Kutokana na hilo tukio, wazazi tuongeze umakini kwenye malezi ya watoto wetu, hasa wa kiume. Suala la kuwalaza na watu wengine iwe ni ndugu au wageni wa aina yoyote Ile, liepukwe kadri inavyowezekana.