Dabodaiga
JF-Expert Member
- Mar 20, 2023
- 441
- 706
[emoji23][emoji23]Kwa jinsi alivyomalizia kuna ujumbe ameufikisha tuliosoma cuba tumeelewa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23]Kwa jinsi alivyomalizia kuna ujumbe ameufikisha tuliosoma cuba tumeelewa.
[emoji23][emoji23]asali ya pole[emoji23]Mnataka mumlambishe nini dada wa watu?????[emoji3]
Niliachana na aliyekuwa mume wangu miaka 5 imepita, kuachana kwetu kulikuwa kubaya sana kwa mambo mabaya yaliyopita katikati yetu. Sipendi kuyaeleza maana ni mabaya ila nilishayasahau na kuyaacha yapite.
Baada ya kuachana (aliondoka bila kuniaga na kodi ikiwa tunadaiwa miezi 5 bila kulipa) nilibaki na watoto huku nikiwa sina pa kuishi kwani mwezi 1 baadaye mwenye nyumba alinitaka kumuachia vyumba vyake, sina kazi, sina hata kitu kimoja kwa kuwa aliondoka na kila kitu hadi nguo zangu na za watoto na kwenda kusikojulikana alihama nikiwa sipo.
Kabla ya yeye kuondoka nilikuwa sijui kama tunadaiwa kodi, kwa kuwa kodi ya mwanzo ilipoisha alinambia kuwa kodi imeisha na yeye hana pesa kwa kuwa kazini kwake wamepata hasara analipwa nusu ya mshahara ambao ndio tunatumia kujikimu nyumbani.
Tukashauriana nikope pesa kwa ndugu yangu ambaye amekuwa akitusaidia kutukopesha pale tunapokwama na tunamlipa kidogokidogo, nikamtafuta na akatukopesha, nikamkabidhi 1,200,000 ambayo ndio ilikuwa kodi ya miezi 6 nikajua kalipa kumbe kampa mwenye nyumba kodi ya mwezi 1 tu na nyingine sijui alikopeleka hadi leo.
Sasa alipoondoka ndio mwenye nyumba kunitafuta kuwa nadaiwa miezi 5 hadi siku ile na nimeshaanza mwezi wa 6 ivyo ananipa wiki 1 nimuachie nyumba yake, kumbuka hapo nalala chini mimi na watoto kwa kuwa kila kitu kilishaondoka na yeye. Na nafanya kazi ndogondogo kupata chakula cha watoto.
Nikawaza kurudi nyumbani, Kilichonishangaza ni kuona ndugu zangu wote hawapokei simu zangu na wakipokea wananilaumu tu kuwa nimeyatafuta mwenyewe na nisiwasumbue na wanakata simu. Nikawaza nimeyataka yapi? Nimekosea nini? Mbona changamoto zangu pande zote wanazijua kulikoni nalaumiwa leo, nikajaribu upande wa aliyekuwa mume wangu ndio balaa zito.
Mtu 1 akaniambia unajua kuwa Unatuhumiwa kuzaa nje ya ndoa? Nikahamaki, akaendelea kusema baba fulani amewaambia ndugu zako na zake kuwa mtoto huyo mdogo sio wa kwake na ndio maana kaondoka. Nikamwambia hapana haiwezi kuwa kweli kwa kuwa sijawahi kutoka nje ya ndoa hata siku moja. Na kama kasema hayo basi ana lake jambo huenda kaamua kuficha mambo yake kwa kunitwisha mzigo maana tayari alikuwa hana pa kukwepea kutokana na mambo yake.
Basi nikatuma ujumbe mfupi kwa ndugu zangu kuwa, nashukuru kwa kuwa nimejua sababu ya nyie kunichukia ila nawaambia siyo kweli na sijawahi kufanya uchafu huo ila nipo tayari wakapime DNA nchi yoyote na ikibainika ni kweli basi wanihukumu nikazima simu ili nipate muda wa kuwa peke yangu kuwaza nini cha kufanya, nikaanza kuwaza cha kufanya nalia peke yangu.
Nikaanza safari ya kutafuta chumba japo sijui nalipa nini, nikapata mama mmoja nikamweleza hali yangu akanambia nakupa chumba ila utakuwa unanilipa mwezi mmoja mmoja sh. 60000 na mwezi huu nakupa ukae bure utaanza kunilipa mwezi ujao, nikaona chumba ni gharama ila kwangu ilikuwa ahueni maana nina mwezi mmoja wa kuanza maisha kutafuta kodi ya watu.
Nikahamia hapo, na wanangu tukaanza maisha, mwezi mmoja baadae nikapata kazi japo haina mshahara mzuri ila inaniwezesha kupata chakula na kulipa kodi ya 60000 kila mwezi, nikaanza kujibana na kununua vyombo, godoro, kitanda, nguo za watoto nk.
Miezi 7 baadaye nikaja kujua alikokwenda yule mwanaume, na kwamba alipohama alihama na mwanamke mmoja ambaye alikuwa mchepuko wake wa siku nyingi wakaanza maisha yao, nilikutana na ndugu wa huyo mwanamke ndiye aliyenipa taarifa hizo.
Baada ya miaka 2, mwanaume huyo alinipigia simu, akidai anataka kuniona kanikumbuka, nikamwambia huwezi kuniona na wala hutakaa ujue naishi wapi, kwa kuwa sikutaka hata waliokuwa wanatufahamu wajue naishi wapi pia, baada ya kumjibu ivyo akasema kwa kuwa hutaki nikuone basi nilichotaka kusema sitasema, japo nilikuwa na lengo la kuonana na wewe ili nianze kukupa hela ya matumizi ya watoto kwa kuwa umekataa na mimi sihudumii hao watoto, nikamwambia kama wameishi miaka 2 bila huduma yako, basi wataishi tu.
Akawa anaendelea kunitafuta kwa namba mbalimbali huku akifoka na kuniita nina kiburi, jeuri, sina adabu kwake, nitakuwa nimepata mwanaume ananipa kiburi nk, mara aseme nitakuwa nimewalisha watoto sumu kuwa yeye mbaya ila yeye sio mbaya anataka kuwatunza ila mimi ndio nazuia. Mwisho alikata tamaa na sasa imepita miaka 5 nikiwa naishi na wanangu.
Inaniuma sana kuishi na wanangu wakubwa sasa ndani ya chumba 1 kikiwa ndio chumba na ndio sebule kwa kuwa sina uwezo wa kulipia zaidi ya chumba 1 ukizingatia ni wa kiume ila sina jinsi najipa moyo kuna siku nitapata nafasi ya kupata walau vyumba 2 wanangu wakalala tofauti na mimi mama yao.
Nimejitahidi kuandika matukio machache kwa kuyakata sana ili nisiwacoshe
Hapaa kuna maharamiaa nawaonaaa...[emoji3][emoji3][emoji3][emoji23][emoji23]asali ya pole[emoji23]
Wanataka kula tunda kimasihara[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119]Hapaa kuna maharamiaa nawaonaaa...[emoji3][emoji3][emoji3]
Yanii machakaramuu sanaa yanakuwa kama mume wa huyo dada... genye zikimshikaa ndo anarudi mbiooo[emoji3][emoji3][emoji3]Wanataka kula tunda kimasihara[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119]
Acha kusafiria nyota ya mwenzako. Wengi wenu huwa haya yanawatokea baada ya kuzingua. Huyu amesema hajawahi kusaliti ndoa yake, na mwanamke haachwi kwasababu yoyote ile ila ya kusaliti na uchawi/ushirikina.Acha mama tuitwe mama jamani[emoji24][emoji24]
Mdada akaze hivo hivo,hakuna kuwapa maharamia nafasi[emoji23][emoji23]Yanii machakaramuu sanaa yanakuwa kama mume wa huyo dada... genye zikimshikaa ndo anarudi mbiooo[emoji3][emoji3][emoji3]
Mbona makasiriko tena!!?? Nimesafiria nyota yake kivipiAcha kusafiria nyota ya mwenzako. Wengi wenu huwa haya yanawatokea baada ya kuzingua. Huyu amesema hajawahi kusaliti ndoa yake, na mwanamke haachwi kwasababu yoyote ile ila ya kusaliti na uchawi/ushirikina.
Mm nashauri jamii forum itoe namba watu wachange. Huyu member akuchukue Kule mikocheni Kule ofisn kwaoJamiiforum wangeweka utaratibu wa wao kudhibitisha identify ya mtu, kisha wanaoguswa wakaweza kumsaport mtu kwa account ya jamiiforum, wengi wanapitia magumu ambayo kwa kidogo mtu alichonacho kingeleta relief.
All in all pole sana dada angu.
We cheka tu 😅[emoji23][emoji23]
Hatujapata story kabila ila so far bi dada anaonekana hakutendewa haki na huyu mwenzie.Wanawake ni wanafiki sana na mnapenda kutafuta huruma wakati nyie ndo mnaanzaga kuvuruga nyumba hadi mwanaume anaamua kutokomea kusikojulikana
Inshallah itapatikana, wewe fanya kutafuta kisha tuletee mrejesho hapa sisi tutajua la kufanya, this is Tanzania we are family. Nenda katafute kisha ukiviona njoo hapa tujue la kufanya.Tatizo linakuja wenye nyumba wanataka kodi ya miezi 6 kwa mkukupuo, hata nikipata vya 30000 sitaweza kulipa pesa yote kwa mkupuo hapa nalipa mwezi mmoja mmoja tu
Hivi unajua umewatag watu kwenye hii comment?!poleni sana,inaonekama Mumeo alikua Zee la hovyo sana
Tafuta Hela ulee wanao MunguniMungutu atakua nawe daima.
Ndio najua sana tu mkuu.Hivi unajua umewatag watu kwenye hii comment?!
Wewe mbona sasa kama unataka aanze kuwa mjinga tena. Huyo jamaa ni hana akili. Kama alikuwa ana nia ya kumsaidia kipindi anataka kusema angekaa nae kiutu uzima wayajenge na sio kuondoka kama nguruwe anatoka bandani.Pole sana dada!
Ninaomba kukushauri. Kama mume wako amekutafuta na ametaka mzungumze, msikilize.
Kwa uelewa wangu, kukataa kumsikiliza unafanya kosa, kosa zaidi. Kwa kusema hauwezi kuonana nae unaharibu akili yako; unajiadhibu mwenyewe.
Kwa hiyo, kwa msimamo huu, kama ndio dhamira yako, unashiriki kwenye makosa yaleyale; nawe unakuwa mkosaji hata kama haukuwa na kosa.
Msamaha sio kusema nimekusamehe au nimesahau nilitendewa au kutenda, bali hali hiyo ni lazima uifanye iwe vitendo au matendo.
Dada, msamaha ni mlango wa mema yote, ni nguvu ya kupata chochote; ni pia uponyaji.
Anae samehe anamkaribisha Mungu ndani yake.