Nilijikuta naishi maisha ambayo sikuyategemea ila sina jinsi

Mpe nafasi ya kumsikiliza, kama anataka kulea watoto nakushauri ukubali tu....

Maana nakuhakikishia, hao watoto watakuja kumtafuta baba yao.. na hapo itakuuma zaidi
 
Mimi nilikimbia mwanamke nilimuacha na watoto wawili mmoja wa kwake umri miaka mitano na mwingine miaka miwili ndio Morgan wangu huyo.

Sababu zilizofanya nimkimbie.

1. Toka mwanzo naanza naye mahusiano nilishamuweka wazi kuwa nipo mkoa ule sina furaha na kazi nayofanya na at anytime naweza kurudi nyumbani kwetu Namtumbo hapo tupo Kagera so akaamua kubeba mimba kama kunishawishi niendelee kubaki ile mimba iliharibika ilipofikisha umri wa miezi 7 tukaendelea na mahusiano kumbe kabeba mimba nyingine ndio Morgan huyo.

2. Morgan akazaliwa tukawa tunaishi lakini mimi roho yangu ilikuwa inaniuma kuona kama amenilaghai kwa gia ya mtoto ili nisiweze kurudi kwetu Namtumbo mnaweza kuhoji kwa nini nisirudi naye Namtumbo jibu ni kuwa sikuwa tayari kuwa na mwanamke pia financial sikuwa vizuri kwenda kuanza maisha Namtumbo nikiwa na familia.

3. Nilikuwa na madeni ambayo nilikataa kuyalipa nilimripoti mdeni wangu Takukuru akanambia nitakuonesha mimi na wewe nani mjanja alikuwa mtu wa Mara Chacha nikaona kabisa hapa mapanga yananihusu usalama wangu mdogo.

4. Kuongeza viugomvi vya ndani ya nyumba na stress za kuingia kwenye maisha ya ndoa bila ya kutarajia na ugumu wa maisha nikaona wakati sahihi wa kutoroka familia umewadia.

Kwa kipindi cha miaka miwili wazo nililokuwa nalo kichwani ni kurudi nyumbani nikimuangalia Morgan zile stage zake za ukuaji kama kutambaa, kutembea naona nikomae tu na huyu mwanamke lakini bado wazo la kurudi nyumbani liliponizidi nguvu.

Ilikuwa hivi siku nimerudi jioni nikamwambia nimeomba likizo naenda nyumbani jioni hii akafikiri utani akaleta chakula nikala nikachukua bag dogo nikaweka vyeti vyangu suruali kadhaa na tisheti nikamuachia hela ya matumizi nikachukua bodaboda huyo nikaanza safari ya kuitafuta Namtumbo.

Nipeni Maua yangu nimalizie hii true story.
 
Mpe nafasi ya kumsikiliza, kama anataka kulea watoto nakushauri ukubali tu....

Maana nakuhakikishia, hao watoto watakuja kumtafuta baba yao.. na hapo itakuuma zaidi
Sio baba yake tu, kuna member alifungua uzi humu majuzi ana zaidi ya miaka 50 anawatafuta ndugu zake upande wa mama na upande wa baba, scenario yake inafanana kidogo na ya huyu mama tofauti yake ni kidogo, walipofiwa na mama yao hawakuwajua ndugu zao mpaka leo, yaan mtu mpaka anafika 50 yrs old hajui ndugu upande wa mama Wala upande wa baba
 
Wakati mwingine hizi story ukikurupuka unaweza kumlaani huyo mwanamme.
 
Mwenye watoto ameshakuambia anataka ahudumie watoto wake wewe unaweka kiburi halafu unaanza kulia lia, pambana
 
We malizia tu maua yatakuja muda sio mrefu,
 
Swali la kizushi kwahiyo miaka yote iyo ujawahi toa mbususu kwa mtu yoyote hadi kesho?
 
Utakua ni mmoja ya wazazi mnakimbia majukumu ya kifamilia, huyo dada alivyoteseka unaona kirahisi tu amsamehe?
Hakuna kisicho sameheka. Na msamaha hukaribisha Mungu rohoni.
Ukisamehe hata huwezi kuja kujieleza mtandaoni huku kwa sababu yalisha isha moyoni
 
Mkuu

Kama ulichosimulia ni kweli!

Bas ni ile mwendelezo wa wanaume wenzetu kufeli na kuumiza watoto!

Mimi nakuelewa sana ulichopitia kama ni kweli ulivoeleza!

Kumlea kijana HADI akajitamgua mwenyewe ni kazi ngumu SANA!!

Nakushauri UKIPATA nauli jaribu kwenda kwenye wilaya zilizo chamgamka na maisha ni nafuue hasa chakula na malazi!!

Using'ang'anie Miji mikubwa kama Dar na n.k!

Wilaya kama Tunduma, malinyi njombe hata makambako kuna shughuli za kilimo na vibarua ambavyo vitakuinua na ukatunza fedha ukajenga na kuishi na wanao!!!


Mungu hajawahi muacha mama mwenye WATOTO bila msaada hugeuka na kuwa baba halisi wa watoto hao na mume wa mama aliyetelekezwa!!

Mungu wabariki kina mama kama nyie!!!
 
Siwezi ruhusu kupasha kiporo ili watoto wapate matunzo, kama wa kuwatunza anewatunza bila kuhitaji kukutana na mimi. Mbona mnaona mwanamke mnaweza kumchezea tu mkitaka loh
Siamini kama kuna mwanaume ataweka condition ya kupasha kiporo ili ahudumie wanae.

Nachojua akitaka kupasha kiporo ataanza kuhudumia na kulipa bili zote plus zako binafsi e.g kununua nguo na zawadi za mara kwa mara bila kuombwa, na mwisho kiporo unakipeleja mwenyewe.

Maelezo yako umejiweka wewe ni safi sana jambo ambalo inaonesha wewe ndio mchafu zaidi.
Pole dada, uzuri maisha hayawezi kusimama iwe kwako au kwa huyo adui yako. Kwahiyo Take it easy.
 
Nimesoma uzi wako kwa umakini,
Ila nitakua mbaya kusikiliza upande mmoja,
Ila kuna namna pia wewe una tatizo sehem...

Hakuna mkamilifu, mwanaume alikukosea na hauwezi badilisha huo ndio ukweli...
Ameomba nafasi ya kulea wanae na una mkatalia..je unadhani umefanya hekima?
Angalau ungepata unafuu wa maisha,je unamkomoa nani?
Baba,watoto ama wewe mwenyewe?

Utajitesa kuwalea mwenyewe ila mwisho wa siku watoto wakikua watamtafuta baba yao, kama kuna todauti watazimaliza.
Lengo la kuandika huu uzi hapa ni nini ikiwa unakataa msaada wa mzazi mwenzio...je lengo tukuchangie watu baki angali baba wa watoto yupo?

Mpe mzazi mwenzio haki yake,
Hao ni watoto wake pia.
 
Hakuna kisicho sameheka. Na msamaha hukaribisha Mungu rohoni.
Ukisamehe hata huwezi kuja kujieleza mtandaoni huku kwa sababu yalisha isha moyoni
Ukiendelea na hio mitazamo una safari ndefu. Akishamsamehe atapata faida gani? Ndio wale wachungaji anapitisha donation church anunue gari ya kutembelea we ukitaka gari anakuombea.

Bro achana na hio mindset utatumika sana, kwani asipomsamehe ni dhambi? Binadamu kuna mambo usipomuonyesha hato kuheshimu.
 
Miaka mitano bado una kinyongo? Achilia na samehe, kutanisha watoto na baba yao, move on penda mtu mwingine, sahau yaliyokukuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…