Nilijikuta naishi maisha ambayo sikuyategemea ila sina jinsi

Nilijikuta naishi maisha ambayo sikuyategemea ila sina jinsi

Jamiiforum wangeweka utaratibu wa wao kudhibitisha identify ya mtu, kisha wanaoguswa wakaweza kumsaport mtu kwa account ya jamiiforum, wengi wanapitia magumu ambayo kwa kidogo mtu alichonacho kingeleta relief.

All in all pole sana dada angu.
@Moderator
 
Khaa yani kuna watu vitu mnaandika hadi unajiuliza huyu mtu anatumia kiungo gani kufikiri, kwahiyo huyo mume alipokuwa anawakimbia hao watoto na kusema kuwa mmoja siyo wake alitegemea nini, kwanini wanaume mnakuwa ni watu wa kutaka kufanya makosa, halafu wanawake wachukulie poa tu kana kwamba hakuna kilichotokea, hivi ushenzi wenu huwa mnaona ni mdogo siyo
Mwambie aelezee chanzo Cha mgogoro, kuna yule alihojiwa na VOA mumewe alimkata mkono wa kulia, akatoa kiganja kabisa, alipohojiwa dada alisema chanzo ni wivu wa kimapenzi na simu ndio iliyopelekea yeye kukatwa kiganja Cha mkono na kupigwa nusura kuuawa, sasa mwambie mleta mada aseme chanzo Cha mgogoro uliomfanya jamaa kumkimbia na kuepusha Shari ni nini ? Maana angebaki uenda tungekua tunazungumza story nyingine mda huu,
 
Ndio ueleze chanzo Sasa Cha jamaa kukukimbia ni nini ? Maelezo mengine sawa tumeyapokea okay turudi nyuma chanzo ni nini hadi akafikia maamuzi ya kukukimbia ? Huwezi ukasema hujui maana najua unajua Ila hupendi kusema ukweli, na hautaki ukweli ujulikane Ila picha mbaya ya wanaume kukimbiwa wanawake na watoto ndio unayotaka ionekane, Jambo ambalo sio sahahi kwa kuangalia kwa upana na kwa kina
Vipi kama chanzo ni kibaya zaidi ya kukimbia?
 
Issue sio kusikiliza upande wa Pili, issue ni source ya mgogoro wao ni nini ? Story yake ipo vizuri Ila kwenye source kaficha code na hataki ujue we unamwelewaje amelenga nini hapo sasa km sio kutaka wanaume waonekane wote wanakimbia wanawake bila sababu, aeleze chanzo ni nini na hicho chanzo hajakieleza na kasema wazi hatokieleza sasa ndio nini ? Ina maana gani ?
Sasa mtu ameshakuambia hajawahi kumcheat mume wake wala hana tabia za hovyo ila wewe ndio unamlisha maneno na kumlazimisha aseme anazo, wewe unataka kuonesha kwamba wanaume wote ni watakatifu hakuna mwanaume anayeweza kukimbia ndoa hivi hivi lazima chanzo kiwe ni mwanamke, labda mtuambie kwanini wanaume mnapenda kujiona innocent sana na uniambie hii story ingekuwa ni mwanaume ndio kaleta kumshutumu mke wake ungeandika kama ulivyoandika hapa
 
Wanawake huwa mnachekesha sana...yaani ugombane na mzazi mwenzako then ugomvi uuhamishie kwa watoto!! Kwanini umzuie baba watoto wako haki ya kuonana na kuhudumia wanawe??

Ni wazi ushawalisha sumu za kutosha hao watoto kuwa baba yao ni mbwa tu. Unawanyima watoto wako haki ya kumjua hata baba yao. Wanawake mnahukumu mambo kwa mihemko pasi na kutumia hekima na busara.


Kwanini usingemruhusu huyo aliyekuwa mumeo awahudumie watoro wake?
Pole sana, kama ndio uelewa wako uko ivyo pole
 
Sihukumu ila wanawake acheni kuolewa nawanaume wanaopanga , hawana guarantee kuwa watakuwa nawewe siku zote za maisha Yako .

Kama hauna mwanaume ambaye hajajenga wewe kuwa single tu .

Maana anaweza kimbia usimwone na walio nanyumba angalieni kama kweli hizo nyumba nizao na mzae Kwa akili.
Maisha sio marahisi maisha ni magumu ila usijiongezee shida .

Maana niwewe tu watoto wanawajua sio baba kingine katika maisha Yako yote usilegee tafuta maisha Yako .

Tofauti na wanaume hii inasaidia kutoaibika unatakiwa uwe na second plan always sio unajisahau.
 
Pole sana dada!

Ninaomba kukushauri. Kama mume wako amekutafuta na ametaka mzungumze, msikilize.

Kwa uelewa wangu, kukataa kumsikiliza unafanya kosa, kosa zaidi. Kwa kusema hauwezi kuonana nae unaharibu akili yako; unajiadhibu mwenyewe.

Kwa hiyo, kwa msimamo huu, kama ndio dhamira yako, unashiriki kwenye makosa yaleyale; nawe unakuwa mkosaji hata kama haukuwa na kosa.

Msamaha sio kusema nimekusamehe au nimesahau nilitendewa au kutenda, bali hali hiyo ni lazima uifanye iwe vitendo au matendo.

Dada, msamaha ni mlango wa mema yote, ni nguvu ya kupata chochote; ni pia uponyaji.

Anae samehe anamkaribisha Mungu ndani yake.
Aisee ...Mungu ?!?!
POLE sanaa lakini yule bwana alikosea sana pia nadhani ni hasira tokana na yale maneno shukuru Mungu aliondoka tu maana wengine wanafikia hatua ya kuwaua watoto. Aliporudi ungemsikiliza anachotaka kusema maana kitendo cha kuondoka mpaka na vitu ina maana aliamini kabisa HAO WATOTO SIO WAKE maana wanaume huwa tunaondoka na nguo tu kama mtu unaona umeshindwana nae mali watatumia watoto may angekupa support ya maishaa maana kama miaka 5 imepita bado una changamoto hata ya kodi jishushe ila kama akileta story za kifala na sio support achana nae jumlaa. pole sana
Kwa maelezo yake...kama amesema kweli ! Huyo mwanaume ni mpumbavu ..dada anastahili!
Kuambiwa mtoto sio wako Ndio uondokeniinyama hivo!?
 
Sihukumu ila wanawake acheni kuolewa nawanaume wanaopanga , hawana guarantee kuwa watakuwa nawewe siku zote za maisha Yako .

Kama hauna mwanaume ambaye hajajenga wewe kuwa single tu .

Maana anaweza kimbia usimwone na walio nanyumba angalieni kama kweli hizo nyumba nizao na mzae Kwa akili.
Maisha sio marahisi maisha ni magumu ila usijiongezee shida .

Maana niwewe tu watoto wanawajua sio baba kingine katika maisha Yako yote usilegee tafuta maisha Yako .

Tofauti na wanaume hii inasaidia kutoaibika unatakiwa uwe na second plan always sio unajisahau.
Asilimia kubwa ya wanandoa wamepanaga bado labda umshauri awe na kipato chake maana hata mwanaume anaefurahia mke kuwa nyumbani bila kazi basi malengo ya maisha ni ngumu kufikia hasa kwa sisi wa vipato vya chini
 
Hapana hicho sio chanzo hio ni hearsay akisikia kwa watu wakisema nataka aseme chanzo na anakijua Ila hataki kusema ukweli na ukisoma huko juu amesema hatoniambia au hatotuambia chanzo au source ya huyo Mwanaume kumkimbia ukiondoa hio hearsay aliyoisikia kwa watu wakisema, yeye chanzo halisi anakijua
Unaleta ubishi usiokua na maana1[emoji706]
 
Umeshikiwa akili nini ? Hio ni hearsay huelewi maana ya hearsay, hearsay evidence is not admissible (tho there are some exceptions) unaelewa maana yake ?
Mm nina mtoto ambae ninatoa gharama za ada tuu lakini huduma nyingine sitoi na hata hio ada nitakuja kusitisha hio huduma kutokana na tabia za mama yake kiburi na matusi,so usione namtetea huyu ukahisi labda sielewi hizi mambo,wanawake huwa wanazingua sana lkn hata baadhi ya wanaume huwa wanazingua balaa tena mwanaume ni mgeni k ndio balaa kabsa
 
Wewe unajitambua nini hapo ulipo ? Nini unachojitambua kulishwa maneno ya uongo na yenye kupandikiza chuki kwa wanaume bila kueleza ukweli kwa kina ndio unaona umejitambua ?
Wewe itakua umekimbia kuhudumia huko sio bure
 
Mwambie aelezee chanzo Cha mgogoro, kuna yule alihojiwa na VOA mumewe alimkata mkono wa kulia, akatoa kiganja kabisa, alipohojiwa dada alisema chanzo ni wivu wa kimapenzi na simu ndio iliyopelekea yeye kukatwa kiganja Cha mkono na kupigwa nusura kuuawa, sasa mwambie mleta mada aseme chanzo Cha mgogoro uliomfanya jamaa kumkimbia na kuepusha Shari ni nini ? Maana angebaki uenda tungekua tunazungumza story nyingine mda huu,
Okay,let's say mwanamke ndio mwenye makosa,kama mwanaume ndio ubebe mpaka nguo za watoto na za mke wako uondoke nazo[emoji2369], hapo mm ndio namuona huyo mwanaume hana akili
 
Ndoa inatakiwa kulindwa kwa nguvu zote, mkivunja au mmoja kuvunja ndoa, madhara makubwa ni kwa watoto, ni shida na kilio, mimi niseme, mkiwa mnaishi ktk ndoa kuheshimiana, kuwa na utii, upendo, hekima, kuacha dharau, kuvumiliana sana, kujituma kujenga maisha ni lazima sio ombi. Sbb upendo au furaha au hekima haiji bure bure tu inajengwa na nyinyi katika ndoa.

Mkikosa heshima, hekima, uvumilivu na kuwa mkorofi au jeuri au kutojaliana, ndoa itakufa, na watoto wataumia bila sababu, sasa mara nyingi sio vema sana kutafuta kosa ni la nani hadi ndoa kuvunjika, kikubwa ni kuwasaidia watoto wasije pata mateso makubwa, sbb matatizo ya ndoa mengine ni ya ndani mno, yaliopelekea upendo na furaha kufa kabisa kwenye familia kwa sbb kadha wa kadha, sio jambo
rahisi kuongelea juu juu, ila ukweli mnaujua nyie wana ndoa, nini kimetokea hadi ndoa kuvunjika.
 
Sasa mtu ameshakuambia hajawahi kumcheat mume wake wala hana tabia za hovyo ila wewe ndio unamlisha maneno na kumlazimisha aseme anazo, wewe unataka kuonesha kwamba wanaume wote ni watakatifu hakuna mwanaume anayeweza kukimbia ndoa hivi hivi lazima chanzo kiwe ni mwanamke, labda mtuambie kwanini wanaume mnapenda kujiona innocent sana na uniambie hii story ingekuwa ni mwanaume ndio kaleta kumshutumu mke wake ungeandika kama ulivyoandika hapa
Hajawahi kumcheat wewe ulikuepo ? Aseme yeye chanzo sio wewe upike maneno ya kulishwa na yeye useme ndio chanzo, Kuna chanzo Cha ndani Cha mgogoro wao hataki kukiweka wazi na ameshasema hatoweka wazi chanzo hicho, ukiwa na akili ndogo huwezi kuelewa hilo
 
Okay,let's say mwanamke ndio mwenye makosa,kama mwanaume ndio ubebe mpaka nguo za watoto na za mke wako uondoke nazo[emoji2369], hapo mm ndio namuona huyo mwanaume hana akili
Kuna mengi yamesababisha yote hayo mwambie aelezee chanzo Cha mgogoro wao ndio utakapopata jibu, ukielezwa juu juu tu mwanaume ndie anaeonekana mbaya Ila akieleza chanzo nna uhakika asilimia 100 utaufyata mkia,
 
Niliachana na aliyekuwa mume wangu miaka 5 imepita, kuachana kwetu kulikuwa kubaya sana kwa mambo mabaya yaliyopita katikati yetu. Sipendi kuyaeleza maana ni mabaya ila nilishayasahau na kuyaacha yapite.

Baada ya kuachana (aliondoka bila kuniaga na kodi ikiwa tunadaiwa miezi 5 bila kulipa) nilibaki na watoto huku nikiwa sina pa kuishi kwani mwezi 1 baadaye mwenye nyumba alinitaka kumuachia vyumba vyake, sina kazi, sina hata kitu kimoja kwa kuwa aliondoka na kila kitu hadi nguo zangu na za watoto na kwenda kusikojulikana alihama nikiwa sipo.

Kabla ya yeye kuondoka nilikuwa sijui kama tunadaiwa kodi, kwa kuwa kodi ya mwanzo ilipoisha alinambia kuwa kodi imeisha na yeye hana pesa kwa kuwa kazini kwake wamepata hasara analipwa nusu ya mshahara ambao ndio tunatumia kujikimu nyumbani.

Tukashauriana nikope pesa kwa ndugu yangu ambaye amekuwa akitusaidia kutukopesha pale tunapokwama na tunamlipa kidogokidogo, nikamtafuta na akatukopesha, nikamkabidhi 1,200,000 ambayo ndio ilikuwa kodi ya miezi 6 nikajua kalipa kumbe kampa mwenye nyumba kodi ya mwezi 1 tu na nyingine sijui alikopeleka hadi leo.

Sasa alipoondoka ndio mwenye nyumba kunitafuta kuwa nadaiwa miezi 5 hadi siku ile na nimeshaanza mwezi wa 6 ivyo ananipa wiki 1 nimuachie nyumba yake, kumbuka hapo nalala chini mimi na watoto kwa kuwa kila kitu kilishaondoka na yeye. Na nafanya kazi ndogondogo kupata chakula cha watoto.

Nikawaza kurudi nyumbani, Kilichonishangaza ni kuona ndugu zangu wote hawapokei simu zangu na wakipokea wananilaumu tu kuwa nimeyatafuta mwenyewe na nisiwasumbue na wanakata simu. Nikawaza nimeyataka yapi? Nimekosea nini? Mbona changamoto zangu pande zote wanazijua kulikoni nalaumiwa leo, nikajaribu upande wa aliyekuwa mume wangu ndio balaa zito.

Mtu 1 akaniambia unajua kuwa Unatuhumiwa kuzaa nje ya ndoa? Nikahamaki, akaendelea kusema baba fulani amewaambia ndugu zako na zake kuwa mtoto huyo mdogo sio wa kwake na ndio maana kaondoka. Nikamwambia hapana haiwezi kuwa kweli kwa kuwa sijawahi kutoka nje ya ndoa hata siku moja. Na kama kasema hayo basi ana lake jambo huenda kaamua kuficha mambo yake kwa kunitwisha mzigo maana tayari alikuwa hana pa kukwepea kutokana na mambo yake.

Basi nikatuma ujumbe mfupi kwa ndugu zangu kuwa, nashukuru kwa kuwa nimejua sababu ya nyie kunichukia ila nawaambia siyo kweli na sijawahi kufanya uchafu huo ila nipo tayari wakapime DNA nchi yoyote na ikibainika ni kweli basi wanihukumu nikazima simu ili nipate muda wa kuwa peke yangu kuwaza nini cha kufanya, nikaanza kuwaza cha kufanya nalia peke yangu.

Nikaanza safari ya kutafuta chumba japo sijui nalipa nini, nikapata mama mmoja nikamweleza hali yangu akanambia nakupa chumba ila utakuwa unanilipa mwezi mmoja mmoja sh. 60000 na mwezi huu nakupa ukae bure utaanza kunilipa mwezi ujao, nikaona chumba ni gharama ila kwangu ilikuwa ahueni maana nina mwezi mmoja wa kuanza maisha kutafuta kodi ya watu.

Nikahamia hapo, na wanangu tukaanza maisha, mwezi mmoja baadae nikapata kazi japo haina mshahara mzuri ila inaniwezesha kupata chakula na kulipa kodi ya 60000 kila mwezi, nikaanza kujibana na kununua vyombo, godoro, kitanda, nguo za watoto nk.

Miezi 7 baadaye nikaja kujua alikokwenda yule mwanaume, na kwamba alipohama alihama na mwanamke mmoja ambaye alikuwa mchepuko wake wa siku nyingi wakaanza maisha yao, nilikutana na ndugu wa huyo mwanamke ndiye aliyenipa taarifa hizo.

Baada ya miaka 2, mwanaume huyo alinipigia simu, akidai anataka kuniona kanikumbuka, nikamwambia huwezi kuniona na wala hutakaa ujue naishi wapi, kwa kuwa sikutaka hata waliokuwa wanatufahamu wajue naishi wapi pia, baada ya kumjibu ivyo akasema kwa kuwa hutaki nikuone basi nilichotaka kusema sitasema, japo nilikuwa na lengo la kuonana na wewe ili nianze kukupa hela ya matumizi ya watoto kwa kuwa umekataa na mimi sihudumii hao watoto, nikamwambia kama wameishi miaka 2 bila huduma yako, basi wataishi tu.

Akawa anaendelea kunitafuta kwa namba mbalimbali huku akifoka na kuniita nina kiburi, jeuri, sina adabu kwake, nitakuwa nimepata mwanaume ananipa kiburi nk, mara aseme nitakuwa nimewalisha watoto sumu kuwa yeye mbaya ila yeye sio mbaya anataka kuwatunza ila mimi ndio nazuia. Mwisho alikata tamaa na sasa imepita miaka 5 nikiwa naishi na wanangu.

Inaniuma sana kuishi na wanangu wakubwa sasa ndani ya chumba 1 kikiwa ndio chumba na ndio sebule kwa kuwa sina uwezo wa kulipia zaidi ya chumba 1 ukizingatia ni wa kiume ila sina jinsi najipa moyo kuna siku nitapata nafasi ya kupata walau vyumba 2 wanangu wakalala tofauti na mimi mama yao.

Nimejitahidi kuandika matukio machache kwa kuyakata sana ili nisiwacoshe
Pole Sana dada
Mtu akihitaji kukusaidia anafanyaje?

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom