Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 6,944
- 14,351
- Thread starter
- #61
Ushamba unakujaje sasa mkuu. mi naona ni ustaarabu tuJapo kushukurushukru sana ni ushamba
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ushamba unakujaje sasa mkuu. mi naona ni ustaarabu tuJapo kushukurushukru sana ni ushamba
Watu wanadhambi sanakuna mtu kasoma hadi aya ya mwisho akitafuta mahali umeandika umemnyandua huyo mama 🤣

Asante sana kwa uzi mkuu🤣Wakuu Ikumbukwe hakuna formula.Usiige na tusiigane.
Niliwahi pendwa sana na muuza duka jinsia ya kike asee kisa na mkasa nilikuwa na tabia ya kusema ahsante sana kila anapo nihudumia.
Ni umri wa makamo kiasi kwamba anaweza kuwa mama bila shaka kabisa. Huyu maza alinielewa sana akaona isiwe taabu akachukua hadi no za wazazi wangu kuwashukuru namna walivyo nilea.
Siku moja alinambia wewe ni mteja mzuri sana kwangu nikauliza kwanini mama akasema mimi ndo napaswa nikushukuru kuja kunichangia hapa na badala yake wewe ndo hushukuru kana kwamba umepewa bure ni nadra sana kuona watu kama wewe.
Hivyo kwa kupitia uteja huu akawa kama mama yangu pale kitaa hadi mmewe akajulishwa. Siku moja ilikuwa imekaribia Xmass mara yule mmewe akanipigia simu na sikuwa na no yake baada ya kujitambulisha tukafahamiana akaniomba niende kwake hapo ilikuwa saa11 jioni akanimbia nipite dukani then twende naye anipeleke.
Sikupoteza muda dk0 nikawa pale. Alikuwa na gari ya kuzugia sio kali tukapanda hatukuchelewa tukafika.
Jamaa alikuwa na bonge la mjengo kumbe lile duka la takataka lilikuwa na mke wake tu yeye ana maduka ya ELECTRONICS na pikipiki. nilishangaa ila ndo hivyo tena.
Baada ya kukaa wakaja mabinti 2 mmoja beki3 ndo mkubwa umri tunaendana ama naweza mzidi kama miaka2-3 hivi.
Akawaambia huyu ni kaka yenu wakanisalimu wakaondoka then akawauliza kuku mmewapa dawa?
Wakajibu ndio, nikamuuliza mzee unakuku? akasema ninao sasa wanaumwa siku ya3 na sijui ugonjwa gani.
Nikamwambia tunaweza kuwaona akasema kuwa huru hapa ni nyumbani kabisa nikazama nae bandani na kumwambia kuku wako wana kipindupindu hivyo mwambie mama aje na dawa hii.
Nikampa na ushauri kama wote. alifurahi sana yule father kitaa. Muda huo sijui nini nilichoitiwa pale na inaelekea saa1 hivi mara mama nae kafika.
Alipofika tu akaniuliza mimi akaja tukapiga story nae akawaita wale wadada2 akawaambia the same issue kama alivyofanya mzee. sijakaa sawq wakaja vijana 3 wanauza kwenye pikipiki na elect.
Mama akasema naishi hapa naomba uwe unakuja mwanangu wadogo zako wanasoma ila kesho watakuja kwa ajiri ya sikukuu maana walifunga wakaenda tuition tunakuomba siku ya Xmass ujumuike nasi hapa bila shaka ushapajua huhitaji kuuliza tena. Nikajibu nikweli mama na nina shukuru sana kupafahamu hapa.
Father kitaa akadakia umeleta ile dawa ya kuku sasa? Mama akakubali eee ipo father kitaa akasema huyu ndo mtaalamu sasa kawaangalia na kuniambia wanaumwa kipindupindu na dawa yake ni hii mimi nilkuwa sijui kama kuku nao wanauguaga kipindupindu.
INSHORT..
Father kitaa akanisindikiza hadi geto muda huo kaniuliza mishe zangu japo hata mama aliwahi niuliza.
Siku ya xmass ikafika nikatimba baada ya simu za mama kuzidi hatukuoni. Niliwakuta madogo wapo mmoja wa form1 mwingine advance huko.
Walinipa heshima kama kaka yao kweli na wakawa wanakuja hadi geto nikiwepo yaani full maupendo.
Nikawaomba niende nao kijijini kwetu wala hawakukatazwa niakenda nao wote 3 yaani yule dada na hawa 2 wakiume
Vitu tulivyo beba sukari kg50
ngano kg25
mafuta lita 10
sabuni ya unga mfuko1 sikumbuki kg ngapi
wax sijui ndo majava ama nini sijui yalikuwa pair kama 4 hivi na kitambaa cha mzee cha suti
hela cash 200k. na ndizi za kupika viazi mviringo nk
kwa kitendo hicho tulipofika kwetu kijijni nikiwa na boda 4 zimesheheni ilibidi majirani waje kwanza washuhudie ujio wangu.Huku nikiulizwa kazi ninayo fanya nk.
Uzuri mama alikuwa wakiwasiliana vyema kabisa na mama kitaa hivyo maandalizi hayakuwa haba
Walikula sana mbuzi ilichinjwa kuku zilichinjwa miwa ililiwa na vingine vingi vya kijijni na kwa sababu tumepakana na msitu na kuna ngedere mle basi madogo walitamani walale msituni kabisa washuhudie
ngedere analalaje juu ya mti bila kuanguka?
Madogo siku za kwenda skull zilifika lkn waligoma kabisa siyo wa kike maana ndo mkubwa yeye alikuwa college huko
Mimi mwenyewe ilibidi ni vumilie tu maana tulipitiliza siku za kurudi kwenye mishe zangu.
Father kitaa aliwachimba mkwara hatimae tukarudi wakiwa na gunia la mchele uliokobolewa na nyama iliyobanikwa kama nusu mbuzi maana zilifika mbuzi 2 zikihatarisha maisha kwa ujio wa madogo.
Kupitia mama yule tulitengeneza udungu wa karibu sana. Nilitoka kule nakuendelea kujitafuta huku tukiwasiliana
kiana kama mjuavyo fimbo ya mbali haiuwi nyoka.Bado hadi sasa mawasiliano yapo lkn sio kivile.
Niliugua nikalazwa yule mama alikuwa msaada mkubwa sana kwangu sikuwa na bima lakini gharama alitoa yeye mama mzazi alikuja kuniona alifikia pale na kulala kama siku2 akarudi.
Huyu mama kitaa alikuwa ladhi afunge duka aje anione na sikuwahi kumfanyia chochote cha maana tofauti na kusema AHSANTE kila ninapo nunua mahitaji kwakwe. Sijui Father kitaa aliambiwa nini hadi nae akanikubali vilevile!
Bado naitumia sana hii AHSANTE lakini bado sijawahi kukubaliwa tena namna hii
Ila haya mambo ya kuwaambia watoto waseme asante kwa chakula kama kuwaonea hivi?chakula si haki yao ya msingi jamani?Rafiki nikweli ni malezi na mazoea pia. mfano ikitokea nikala chakula halafu nisiseme ahsante hata kwa wife daah huwa najisikia sijatenda haki na ili nibaki normal lazima nimwambie ahsante kwa chakula nilikuwa na mawazo muda huo
Awali ya yote nipende kumshukuru mama😂Japo kushukurushukru sana ni ushamba
Hamia KenyaYaani ninunue halafu niseme asante?alooooh watu mmelelewa malezi bora sana
Kitu ambacho kizito kwangu ni shikamoo. I have no issues na asante na samahani.Ni wachache sana wenye moyo wa kushukuru na kusema asante, wenye misingi ya malezi mema tangu utotoni, lakini wengi wetu tunaishi kimjini mjini kusema asante au kushukuru tu midomo ni mizito sana.
Yaani watanzania tunapenda sana kutia huruma😁Hamia Kenya
Ni haki ila hakijajileta chenyewe. Ndio maana hata wakubwa tunapaswa kukiombea chakula na kushukuru kwa riziki.Ila haya mambo ya kuwaambia watoto waseme asante kwa chakula kama kuwaonea hivi?chakula si haki yao ya msingi jamani?
Nimesema Mimi ndo Huwa Nashukuru Kwa aliyepika (wife) Watoto wawili wakubwa Huwa hawashukuru isipokuwa yule mdogo wao yeye lazima ashukuru. Sioni kama ni kosa na sijawahi washikia fimbo kuwalazimisha kumshukuruIla haya mambo ya kuwaambia watoto waseme asante kwa chakula kama kuwaonea hivi?chakula si haki yao ya msingi jamani?
Sawa,mi nawafundishaga kumshukuru Mungu kwa riziki yeyote tunayopata wasiposema asante kwangu sionagi kama ni big deal...sema naona wakienda kula ugenini ndio itakuwa patashikaNi haki ila hakijajileta chenyewe. Ndio maana hata wakubwa tunapaswa kukiombea chakula na kushukuru kwa riziki.
Excellent.Nimesema Mimi ndo Huwa Nashukuru Kwa aliyepika (wife) Watoto wawili wakubwa Huwa hawashukuru isipokuwa yule mdogo wao yeye lazima ashukuru. Sioni kama ni kosa na sijawahi washikia fimbo kuwalazimisha kumshukuru
Utaonekana huna maadili ya kuleaSawa,mi nawafundishaga kumshukuru Mungu kwa riziki yeyote tunayopata wasiposema asante kwangu sionagi kama ni big deal...sema naona wakienda kula ugenini ndio itakuwa patashika
Hapo sasa tatizo... nilivyo mama mkuda hapo tu ndio siwabani sanaUtaonekana huna maadili ya kulea
😀Watengeneze watoto ili wafit katika familia yeyote hata ukiwa haupo hawatateseka. Kuna aina ya malezi ni ku spoil watotoHapo sasa tatizo... nilivyo mama mkuda hapo tu ndio siwabani sana
Sawa baba mdogo,ngoja niite kikao cha dharula hapa niwapige somo😀Watengeneze watoto ili wafit katika familia yeyote hata ukiwa haupo hawatateseka. Kuna aina ya malezi ni ku spoil watoto
Yeah, siku wataishi na mdogo wako au dadaako then wata feel wananyanyasika. Sababu ile special treatment hawaipati.Sawa baba mdogo,ngoja niite kikao cha dharula hapa niwapige somo
Nimekupata vyema kabisa...nalifanyia kaziYeah, siku wataishi na mdogo wako au dadaako then wata feel wananyanyasika. Sababu ile special treatment hawaipati.
Ila haya mambo ya kuwaambia watoto waseme asante kwa chakula kama kuwaonea hivi?chakula si haki yao ya msingi jamani
Hee yaani wapigwe waseme asante?aisee mi silei mtoto kizembe!tena nishawaambia mtu akikupiga pambana usikae kizembe,ila usichokoze wenzio na kuwapiga bila sababu...Hata wakipigwa kiboko au kuwa mistreatment waambie waseme Asante itawafanya wawe na Ukomavu wa akili na hisia
Asante ni dua ya kuondoa mabaya yote na kutengeneza utulivu mkubwa wa Akili na hisia .
Chakula wanabidi kabla hawajaanza kula washukuru na wakimaliza washukuru