Nilijikuta napendwa sana kisa kusema ahsante kila ninunuapo bidhaa kwake

Asante sana kwa uzi mkuu🤣
 
Rafiki nikweli ni malezi na mazoea pia. mfano ikitokea nikala chakula halafu nisiseme ahsante hata kwa wife daah huwa najisikia sijatenda haki na ili nibaki normal lazima nimwambie ahsante kwa chakula nilikuwa na mawazo muda huo
Ila haya mambo ya kuwaambia watoto waseme asante kwa chakula kama kuwaonea hivi?chakula si haki yao ya msingi jamani?
 
Ni wachache sana wenye moyo wa kushukuru na kusema asante, wenye misingi ya malezi mema tangu utotoni, lakini wengi wetu tunaishi kimjini mjini kusema asante au kushukuru tu midomo ni mizito sana.
Kitu ambacho kizito kwangu ni shikamoo. I have no issues na asante na samahani.
 
Ila haya mambo ya kuwaambia watoto waseme asante kwa chakula kama kuwaonea hivi?chakula si haki yao ya msingi jamani?
Nimesema Mimi ndo Huwa Nashukuru Kwa aliyepika (wife) Watoto wawili wakubwa Huwa hawashukuru isipokuwa yule mdogo wao yeye lazima ashukuru. Sioni kama ni kosa na sijawahi washikia fimbo kuwalazimisha kumshukuru
 
Ni haki ila hakijajileta chenyewe. Ndio maana hata wakubwa tunapaswa kukiombea chakula na kushukuru kwa riziki.
Sawa,mi nawafundishaga kumshukuru Mungu kwa riziki yeyote tunayopata wasiposema asante kwangu sionagi kama ni big deal...sema naona wakienda kula ugenini ndio itakuwa patashika
 
Hata wakipigwa kiboko au kuwa mistreatment waambie waseme Asante itawafanya wawe na Ukomavu wa akili na hisia

Asante ni dua ya kuondoa mabaya yote na kutengeneza utulivu mkubwa wa Akili na hisia .

Chakula wanabidi kabla hawajaanza kula washukuru na wakimaliza washukuru
Ila haya mambo ya kuwaambia watoto waseme asante kwa chakula kama kuwaonea hivi?chakula si haki yao ya msingi jamani
 
Hee yaani wapigwe waseme asante?aisee mi silei mtoto kizembe!tena nishawaambia mtu akikupiga pambana usikae kizembe,ila usichokoze wenzio na kuwapiga bila sababu...
Hapo kwenye kushukuru wako vizuri sana kwenye kumshukuru Mungu ila baada ya chakula nawasikiaga mara waseme asante mara wasiseme asante..nitawakazania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…