Nilikamatwa Morogoro stesheni ya SGR nikituhumiwa kusafirisha chupa ya mil.500 ya maji ya kunywa!

Sasa mkuu, treni imekuwa ndege? Alafu si wanafanya ukaguzi? Kama wameona ni maji ya kawaida tu shida iko wapi?
 
Ukitaka ujue Watanzania bado kiza ukipita Mtera dam utasikia msipige picha hapa na wanaopiga picha wanawasumbua wakati Dunia imezungukwa na satellite ambayo inaweza kuchukua picha hata ya sisimizi popote pale juu ya uso wa Dunia..
Google map inafanya kila kitu
 
Walikuona mlugaluga. Walitakiwa wakuambie uyaache tu hayo maji usipande nayo treni. Hao walinzi hawana common sense. Wao wako kama Bobby akiambiwa shika anashika.
Sasa mtu anatoka porini JKT halafu anapewa kazi ya ulinzi unatarajia afanye nini kama siyo matumizi ya mabavu kuliko akili?
 
M
Sasa mkuu, treni imekuwa ndege? Alafu si wanafanya ukaguzi? Kama wameona ni maji ya kawaida tu shida iko wapi?
Mkuu vimiminika vimekuwa issue kwenye ndege maana ni ngumu sana kutofautisha kati ya glycerin na vimiminika salama, ndio sababu ili isiwe shida vikawa banned
Unaweza ona chupa ya maji safi kumbe ndani mtu keshamix na smart gin anaenda kuleta fujo kwenye behewa.
Ndo mana kama unataka maji basi nunua maji yao ndani
 
Tanzania ina Askari wajinga sana.
 
Inaonesha haujawahi kusafiri kwa treni, ndani ya treni imo baa inauza pombe.
 
Tatizo haujawahi kupanda treni, kuna hoteli na baa.
 
Treni ya asibuhi saa 1:30 ikitokea Dodoma haikujaza abiria, dalili za mwanzo wa kifo. Stesheni ya sgr Moro iko mbali sana na hakuna daladala huku bodaboda sh 5,000/=! Barabara ni njia iliyotengenezwa na magurudumu ya malori wakati wa ujenzi ni vumbi na kokoto. Ukifika stesheni utaona wasafiri ni kundi la wenye uwezo.
 
Jamani iishie huko huko Dar sisi wasukuma lazima tupande na bata wetu sembuse maji
 
usipaki gari hapo wewe unapaki. Tusikukamate kweli?

usipite hapa kuna mbwa wakali, wewe unapita. Mbwa wakali watakuacha kweli?

Ni muhimu kua makini na kuuliza vitu vinavyokwenda maeneo mbalimbali nchini πŸ’
 
Wabongo wanapenda sana kulalamika. It's simple hununui wala kula chakula au maji yao. Trip ya masaa matatu na nusu usipokula au kunywa maji utakufa? Wakikutaza maji yako kunywa yaishe au yamwage uwakomoe 🀣🀣
Safari ya 2hrs mtu anataka ale ndio maana huwa tunashikwa na tumbo la kuhara,πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…