Nilikopa milioni 10, siku naona salary slip yanipasa kulipa 24m jicho la upande wa kushoto lilijifunga kama dakika 40 hivi. Nilijua limeparalyse!

Nilikopa milioni 10, siku naona salary slip yanipasa kulipa 24m jicho la upande wa kushoto lilijifunga kama dakika 40 hivi. Nilijua limeparalyse!

Acha kabisa aisee!

Nikiwa nimepagawa na changamoto iliyokuwa inanikabili bila kujua la kufanya, nikakimbilia benki moja kuomba mkopo. Kufika pale nikamuambia afisa mikopo kuwa nahitaji m15, akaniambia m10 ni utapata lakini si hizo ulizotaka. Nikaona kheri tu itaokoa kitu tena kwa kiasi kikubwa sana tu.

Wakati huo, simu inapigwa kila baada ya sekunde 20 kutoka huko kwenye changamoto iliyonifanya niende kukopa, nilipagawa sana. Wakati afisa mikopo ananieleza habari za makato n.k mimi hata sikuwa nasikia chochote.

Akili ilikuwa kwenye kupata pesa tu nikamalize tatizo. Siku kadhaa mbele nikafanikiwa na tatizo likaisha na akili ikarudi katika utulivu wa kawaida.

Siku zinavyoenda haraka, mwisho wa mwezi ukafika bwana! Aisee, ile naiangalia salary slip sikuamini nilichokiona. Milioni 24 nahitajika kulipa. 24M!!

Kwanza nilihisi baridi, halafu ganzi; baadae nikahisi uono wangu kama hauko sawa. Nikajiuliza imekuaje mbona sioni vizuri? Kwakuwa nilikuwa chumbani, nikasogea kwenye kioo kujiangalia. Dah, si ndo nakuta jicho moja la upande wa kushoto limejifunga, kope haitaki kupanda juu ('kukupila' watu wa pwani ya kusini wanasema).

Nikajaribu kulifunua kwa mkono, wapi! Nikiliacha linajifunga tena. Hali iliendelea hivyo kama dakika 40 au saa moja hivi. Baadae sana ndo likarejea katika hali ya kawaida. Nilishapagawa, nilijua limeparalyse!

Mikopo!!!! Ukiweza kuachana nayo iache ndg'angu!
Hesabu zinakataa mkopo wa 10m kurejesha 24m hata kwa miaka tisa, kwa riba zetu 16% Sasa sijui wewe ulikopa benki gani na kwa miaka mingapi?
 
Wala siyo kweli. Ina maana hukujaza Mkataba mpaka usubirie slip? Maana mkataba huainisha kiasi chote unachopaswa kulipa.

Na hakuna benki Tanzania inayotoza riba ya zaidi ya asilimia 100. Hakuna.

Hii ni Chai.
Chai vipi?
What if kakopa kwa muda mrefu tuseme 5-8 years?
 
Mm nlikopa kijinga hivo hivo mil 30 nkatumpia kwa kilimo cha machungwa nkqlimq kisasa ekar 20 baada ya miaka 3 nkaanza vuna nkajisemea hebu nifute mkopo maana nlipata mteja wa kununua shamba mil 58.kwenda naambiwa bado nadaiwa mil 34 heeee yaan na kulipa 3 yrs kwa makato
 
Wakuu eleweni kitu kimoja, naona wengi wetu tunachangia kwa kujiamini afu tunachangia uongo.

Benki haitumii hizi hesabu zetu za madukani kwamba ukiambiwa riba ni 17% kwa mwaka maana yake kwa miaka mitano utachukua tu 17% × 5 upate 85%, hizi ni hesabu za form one simple interest[emoji2]

Kumaliza utata mtoa mada aseme alikopa benki gani, kwa riba gani na muda gani.
Unafanya kazi benki gani
 
U
Hesabu za benki haziko hivyo. Ni kweli riba inategemea muda ila calculations siyo hizo za simple interest, ukiambiwa benki riba ni 17% unaweza kukuta ni 9.5% kwa hesabu za kawaida.
Benki nyingi zinatumia Non Reducing Calculator na makanuni mengine ya kiuchumi.

Kwa mfano mimi nilikopa nmb 6,100,000 kwa riba ya 17%, kwa miaka 3 ningetakiwa nilipe 9.2M ila nlilipa 7.8M, sasa piga hesabu uone.
Upo sahihi Mkuu.

Ulipaswa ulipe jumla ya Tshs. 7,829,319.24.


Na makato Kwa Mwezi yalikuwa Tshs. 217,481.09.

Jumla ya Riba Kwa mkopo wote ni Tshs. 1,729,319.24.
 
Back
Top Bottom