Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mil 10 kwa mil 17Hii itakuwa ni bayport ingekuwa bank Kama Nmb au crdb ingekuja kwenye 17
Hesabu zinakataa mkopo wa 10m kurejesha 24m hata kwa miaka tisa, kwa riba zetu 16% Sasa sijui wewe ulikopa benki gani na kwa miaka mingapi?Acha kabisa aisee!
Nikiwa nimepagawa na changamoto iliyokuwa inanikabili bila kujua la kufanya, nikakimbilia benki moja kuomba mkopo. Kufika pale nikamuambia afisa mikopo kuwa nahitaji m15, akaniambia m10 ni utapata lakini si hizo ulizotaka. Nikaona kheri tu itaokoa kitu tena kwa kiasi kikubwa sana tu.
Wakati huo, simu inapigwa kila baada ya sekunde 20 kutoka huko kwenye changamoto iliyonifanya niende kukopa, nilipagawa sana. Wakati afisa mikopo ananieleza habari za makato n.k mimi hata sikuwa nasikia chochote.
Akili ilikuwa kwenye kupata pesa tu nikamalize tatizo. Siku kadhaa mbele nikafanikiwa na tatizo likaisha na akili ikarudi katika utulivu wa kawaida.
Siku zinavyoenda haraka, mwisho wa mwezi ukafika bwana! Aisee, ile naiangalia salary slip sikuamini nilichokiona. Milioni 24 nahitajika kulipa. 24M!!
Kwanza nilihisi baridi, halafu ganzi; baadae nikahisi uono wangu kama hauko sawa. Nikajiuliza imekuaje mbona sioni vizuri? Kwakuwa nilikuwa chumbani, nikasogea kwenye kioo kujiangalia. Dah, si ndo nakuta jicho moja la upande wa kushoto limejifunga, kope haitaki kupanda juu ('kukupila' watu wa pwani ya kusini wanasema).
Nikajaribu kulifunua kwa mkono, wapi! Nikiliacha linajifunga tena. Hali iliendelea hivyo kama dakika 40 au saa moja hivi. Baadae sana ndo likarejea katika hali ya kawaida. Nilishapagawa, nilijua limeparalyse!
Mikopo!!!! Ukiweza kuachana nayo iache ndg'angu!
Chai vipi?Wala siyo kweli. Ina maana hukujaza Mkataba mpaka usubirie slip? Maana mkataba huainisha kiasi chote unachopaswa kulipa.
Na hakuna benki Tanzania inayotoza riba ya zaidi ya asilimia 100. Hakuna.
Hii ni Chai.
Hesabu ulisoma mwisho darasa la ngapi?Mil 10 kwa mil 17
sikopi
Fatilia kwanza kwa niliyemquote.Hesabu ulisoma mwisho darasa la ngapi?
Kwamba riba ya 17% ndio 10mil kwa 17mil??
Ulilipaje mkuu naomba mbinu...me bado linaninyonya damuMi nililipa kwa miaka miwili tu..
Unafanya kazi benki ganiWakuu eleweni kitu kimoja, naona wengi wetu tunachangia kwa kujiamini afu tunachangia uongo.
Benki haitumii hizi hesabu zetu za madukani kwamba ukiambiwa riba ni 17% kwa mwaka maana yake kwa miaka mitano utachukua tu 17% × 5 upate 85%, hizi ni hesabu za form one simple interest[emoji2]
Kumaliza utata mtoa mada aseme alikopa benki gani, kwa riba gani na muda gani.
Halafu nilifanya kazi kama miaka miwili kwenda mitatu bila ya makato mpaka nikawafuata ndio wakaanza kukata ndani ya miaka miwili nimemaliza.Ulilipaje mkuu naomba mbinu...me bado linaninyonya damu
Haukuwa na mkopo wa 100% enheHalafu nilifanya kazi kama miaka miwili kwenda mitatu bila ya makato mpaka nikawafuata ndio wakaanza kukata ndani ya miaka miwili nimemaliza.
Upo sahihi Mkuu.Hesabu za benki haziko hivyo. Ni kweli riba inategemea muda ila calculations siyo hizo za simple interest, ukiambiwa benki riba ni 17% unaweza kukuta ni 9.5% kwa hesabu za kawaida.
Benki nyingi zinatumia Non Reducing Calculator na makanuni mengine ya kiuchumi.
Kwa mfano mimi nilikopa nmb 6,100,000 kwa riba ya 17%, kwa miaka 3 ningetakiwa nilipe 9.2M ila nlilipa 7.8M, sasa piga hesabu uone.
Ndio ilikuwa kama na asilimia 80 na kituHaukuwa na mkopo wa 100% enhe
Una bahati ila pia itakuwa salary yako imeshiba kidogo Akina siye huku bado nadaiwa kitu kama 4mNdio ilikuwa kama na asilimia 80 na kitu
Hawa jamaa kama umemaliza ,wataendelea kukata kama hautoenda kule kwao na refund ni kipengele.Una bahati ila pia itakuwa salary yako imeshiba kidogo Akina siye huku bado nadaiwa kitu kama 4m