Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,600
- 35,158
Mimi nampongeza Trump, bora angesitisha misaada yote maana haiwezekani mpaka leo pamoja na kuwa na maprofesa na madokakta wenye PhD mpaka leo hakuna tafiti zozote za maana zinafanyika na mbaya zaidi hata kwenye bajeti ya serikali hamna hata fungu la maana linalotengwa kwa ajili ya tafiti!Siku ya Januari 20, 2025, Rais wa Marekani Donald Trump alisaini agizo la rais (executive order) lililosimamisha kwa muda wa siku 90 utoaji wa misaada nje ya Nchi, ikiwemo programu muhimu za afya kama Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI. "President's Emergency Plan for AIDS Relief " (PEPFAR).
Kusitisha Huku Progran Hizo kutaathiti Dawa za Virusi vya UKIMWI (ARV), Dawa za kifua kikuu (TB), na Dawa za malaria na Dawa za Uzazi wa Mpango..
Ukiachana na Kuathiri Upatikanaji wa Dawa Taarifa ya USAID kuhusu Kupunguza kusitisha Misaada ya Viti hivyo Kumeanza Kuleta Effect kwa Baadhi ya NGOs Mashirika Mengi..
Yanayohusika na Utoaji wa Dawa za ARV,Kifua kukuu na Ukoma,Uzazi wa Mpango,na malaria yameanza Kuyumba na wote wameanza Kutoa Notice kwa wafanyakazi wao kusubiri na Kuangalia kama Marekani itarudisha Panga kwenye ala bhasi watarudi kazini...
Takribani Wafanyakazi wa Mashirika Tanzania 2900s Wanaenda Kupoteza Kazi kutokana Na upuuzi na Ego ya Trump..
Poleni Afya, Poleni Wafanyakazj wenzangu na Mostly Poleni wagonjwa ambao mnaenda Kuathiriki kwa Order hii Isiyo na Mashiko..
Sasa wenzenu wanafanya tafiti kwankutumia maprofesa hao wao wenye PhD, wanaletea madawa tena ya misaada alafu unaanza kuwapangia?
Ni lini na sisi tutasimama wenyewe? Ni lini tutaacha lalamikia misaada na kuanza kutengeneza misingi ya kujitegemea wenyewe?