Siku ya Januari 20, 2025, Rais wa Marekani Donald Trump alisaini agizo la rais (executive order) lililosimamisha kwa muda wa siku 90 utoaji wa misaada nje ya Nchi, ikiwemo programu muhimu za afya kama Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI. "President's Emergency Plan for AIDS Relief " (PEPFAR).
Kusitisha Huku Progran Hizo kutaathiti Dawa za Virusi vya UKIMWI (ARV), Dawa za kifua kikuu (TB), na Dawa za malaria na Dawa za Uzazi wa Mpango..
Ukiachana na Kuathiri Upatikanaji wa Dawa Taarifa ya USAID kuhusu Kupunguza kusitisha Misaada ya Viti hivyo Kumeanza Kuleta Effect kwa Baadhi ya NGOs Mashirika Mengi..
Yanayohusika na Utoaji wa Dawa za ARV,Kifua kukuu na Ukoma,Uzazi wa Mpango,na malaria yameanza Kuyumba na wote wameanza Kutoa Notice kwa wafanyakazi wao kusubiri na Kuangalia kama Marekani itarudisha Panga kwenye ala bhasi watarudi kazini...
Takribani Wafanyakazi wa Mashirika Tanzania 2900s Wanaenda Kupoteza Kazi kutokana Na upuuzi na Ego ya Trump..
Poleni Afya, Poleni Wafanyakazj wenzangu na Mostly Poleni wagonjwa ambao mnaenda Kuathiriki kwa Order hii Isiyo na Mashiko..
Yaani kodi za wamarekani ndio tunawanunulia Watu wetu dawa halafu Kodi zetu ni za safari na kula Bata na magari ya kifahari .
Hivi mtu kama Mwigulu anashindwa kununua gari lake mwenyewe la Kifahari kama alivyokua Marehemu Prof . Maji Marefu Mb. wakati huo?
Kwa nini tunashindwa kujitegemea kwa miaka yote ya uhuru . Wazungu wanafanya biashara zao wanalipa kodi sisi huku Wafanyabiashara wakubwa wanakwepa kodi na kusamehewa kodi . Yaani ujinga mtupu. Kwa nini pawe na misaada kwenye nchi yenye mabilionea wengi kama Tanzania lakini wanakwepa kodi na hakina jitihada za kuziba mianya ya kukwepa kodi zaidi ya kuzidi kupeana mianya ya kukwepa kodi na kujilimbikizia mali.
Kuna taasisis kama EWURA inaingiza mabilioni ya pesa kupitia mafuta ,maji na umeme .Je ,wanalipa kodi au PAE ni kwa wafanyakazi wenye vimishahara vya kuweka kwenye pochi ya mfukoni basi. ?
Kuna mahoteli huko Serengeti ,Mikumi na Loliondo yanainguza mabilioni ya pesa kwa siku . Je,wanalipa kodi inavyotakiwa au ni rushwa na tozo huko juu kwa juu .
Mo, ana Malaki ya ekari za ardhi . Je, anazilipia ipasavyo au anazitumia kwenye mikopo yake bila kuyaendeleza ? Mkonge unauzwa nje kwa maelfu ya Tani ,Je, kodi inalipwa ipasavyo.?
Mafuta yanayoingizwa nchini ,mitandao ya simu, TANESCO, gesi , Makaa ya mawe yanayosafririshwa nje kwa mamilioni ya tani tena kwa kutumia magari ya wakubwa .Je, yanalipiwa kodi inavyotakiwa ?
Madini ya dhahabu,nikeli , Tanzanite ,Almasi ,rubi ,viwanda vya maji yanayouzwa kwa bei inayokaribiana na mafuta toka Urusi je wanalipa kodi kwa mauzo ya kila sekunde mpaka vijijini , viwanda vya sementi ,Viwanda vya pombe vyenye wateja wengi sana je vinalipa kodi ipasavyo , viwanda vya sukari ,ngombe zinazochinjwa kwa maelfu kila siku ,je,zinalipiwa kodi ipasavyo au ni rushwa na kukwepesha kodi kisa Marekani watatoa misaada kwa kuwapigia magoti shingoni ukiwa umevaa mkufu wa dhahabu na kidani cha green safaya.?
Tatizo ni nchi maskini au ni viongozi wasio na kitu kichwani lakini mifuko imefurika kwa mapesa ya ujanja ujanja ?
Soko la ndani kubwa sana ukilinganisha na nchi kama Kenya Uganda na Rwanda lakini bado kodi inakua ni ya wachache na tozo zinaishia mifukoni mwa Wazabuni na wakurugenzi wanaowapa tenda hizo .Jioni mabaa yamejaa watu walioshiba vidonge vya ARV wakiwa wanakula Bata na mademu bia tamu na nyimbo nyingine kama vile ,"kama umenipenda basi nitongoze "
Ni vyema tukawakataa viongozi wasio faa na wabunge wao ili nchi ipige hatua na kuachana na misaada yenye masharti . Huu uwe ni wakati wa kujipanga kwani Trump ametikisa kiberiti tukadhani kimejaa kumbe hakina njiti.