Nilikuwa mfuasi wa Trump Kwa Muda Mrefu sana Ila Kwa Hili la Kusitisha Misaada na Ruzuku upande wa Afya Sikubaliani nalo, amekosea sana

Upumbavu Uko wapi Makonde plateu
Nimesema hali halisi iliyopo..

Mkuu Just imagine Ukija Hospitali Ukaambiwa Amoxicilne au Paracetamol bei yake Tsh 2000 Kwa Kidonge utajisikiaje..

Kuna wakati tuweke Siasa Pembeni Kifupi ni Kuwa Tanzania Bila Utegemezi hatutobi hata Kidogo maan Hata Bajeti ya Madawa yote hayo kwa Mwaka Inazidi Bajeti ya Tanzania Kwa Ujumla
Hivi for more than 60 year tuantegemea misaada tu? Sisi ni watu wa namna gani?
 
Umeongea na kueleza vema
Nchi za Afrika Zote haziwezi kutoboa kwa Disease Burden Iliyopo Ngoja Twende statistically..

  • Riport ya mwaka jana Tanzania Kwa sasa Ina WAVIU- 1.7Milion na waviu wanaotumia ARV ni 1.4 Milion
  • Waliokuwa wana Ugonjwa wa Malaria walikuwa ni zaidi ya Milion 1
  • Watoto waliopatiwa Chanjo ni zaidi ya Milion 1
  • Watu waliotumia Njia za Uzazi wa Mpango ni zaidi ya Milions
  • Wagonjwa wa TB kwa mwaka Jana walikuwa zaidi ya Laki mbili
Hakuna Nchi narudia tena Hakuna nchi wala Chama Kinachoweza Kubeba Hiyo burden Bila Kuhitaji Msaada..
unajua Chanjo moja ni Bei gani? Unajua ARV Drugs Ni Tsh ngapi Kopo Moja? Unajua Uzazi wa Mpango Hata Kidonge tu Circle mpja Ni Tsh ngapi??
umeongea na umetoa maelezo vema sana nazan sasa ni wakat wa viongozi wa afrika kukaa na rafiki zao china na russia waone ni jinsi gan watatusaidia

Maana kila sku waafrika wananchi na viongozi wanaiponda marekan na kuisifia china na russia so ni muda wao sasa kutusaidia

Lakin pia kila mtu anapotoa pesa huwa anaitaji heshima na kuthaminiwa sasa amerika anatoa pesa ila WHO haieshimu wala haithamini
 
Hii iwe wake-up call kwa Africa. Nchi nyingi za Afrika zimepata uhuru kwa zaidi ya miaka 50+ lakini wameshindwa kufungua viwanda vya kutengeneza dawa hata za malaria, nazo tusubiri kusaidiwa wakati tunaishi katika malaria ridden areas? Tumebaki kusifiana kwa kuupiga mwingi !
 
Trump anaipambania USA, hawezi kufanya kazi kwa maslahi ya nchi zingine hivyo uwe supporter wake au usiwe sidhani kama itapunguza au kuongeza chochote huko Marekani.

Hata hivyo hii ni alert kwa nchi kama Tanzania, tuna mengi ya kujifunza kupitia hii executive order ya POTUS, tuishi kwa uwezo wetu, tuna matumizi makubwa sana kama serikali, tunafuja fedha za misaada na mikopo. Hakuna donor anafurahi kuona misaada inayotolewa haifiki kwa walengwa.

Nadhani ushawahi kusikia, America is for the Americans...kule urusi huo msemo upo sana, Russia for the Russians. Tujipqmbanie, sio kusubiri wengine watupe vya bure. JPM aliyasema haya tukampuuza.

Wakati Magufuli akisema Tanzania haina mjomba wa kumtegemea, alipokufa wakasema "watu wema hawafi..."

Jambo la muhimu Donald Trump anatekeleza sera ya America for Americans
 
Siku ya Januari 20, 2025, Rais wa Marekani Donald Trump alisaini agizo la rais (executive order) lililosimamisha kwa muda wa siku 90 utoaji wa misaada nje ya Nchi, ikiwemo programu muhimu za afya kama Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI. "President's Emergency Plan for AIDS Relief " (PEPFAR).

Kusitisha Huku Progran Hizo kutaathiti Dawa za Virusi vya UKIMWI (ARV), Dawa za kifua kikuu (TB), na Dawa za malaria na Dawa za Uzazi wa Mpango..

Ukiachana na Kuathiri Upatikanaji wa Dawa Taarifa ya USAID kuhusu Kupunguza kusitisha Misaada ya Viti hivyo Kumeanza Kuleta Effect kwa Baadhi ya NGOs Mashirika Mengi..

Yanayohusika na Utoaji wa Dawa za ARV,Kifua kukuu na Ukoma,Uzazi wa Mpango,na malaria yameanza Kuyumba na wote wameanza Kutoa Notice kwa wafanyakazi wao kusubiri na Kuangalia kama Marekani itarudisha Panga kwenye ala bhasi watarudi kazini...

Takribani Wafanyakazi wa Mashirika Tanzania 2900s Wanaenda Kupoteza Kazi kutokana Na upuuzi na Ego ya Trump..

Poleni Afya, Poleni Wafanyakazj wenzangu na Mostly Poleni wagonjwa ambao mnaenda Kuathiriki kwa Order hii Isiyo na Mashiko..
Kama kweli ungekuwa mfuasi wa trump usingeshangazwa na hili na mengineyo yafananayo na hayo, "he is the proud white,and he is there for Americans",leave it or love it.
 
Moderator huyu apigwe ban.
Miaka 64 ya uhuru mtu analilia misaada kama vile ni haki yake.
Watanzania Mnachekesha Sana!

Mnasahau hata aliyeleta Misaada kwa Wajawazito kutibiwa na Kupewa Huduma Bure ni USA..
Juzi mkuu wa Mkoa kajaribu Kugusa Switch mmekuja Juu!

Watanzania Hamueleweki Mnatka Nini Mfanyiwe na Nini msifanyiwe Sasa Nyuzi tutawakazia ili tusikie milio
 
Nchi imejaza viongozi wengi wasio na tija kwa taifa mfano RC, DC, RAS, DAS, Wabunge na utitiri kama huo, hao wote wana mishahara mikubwa , posho, nyumba za bure wanazolipiwa na serikali, magari ya anasa n.k. Gharama za kuhudumia hawa wote ni kubwa sana kubebwa na nchi masikini kama Tanzania
 
Siku ya Januari 20, 2025, Rais wa Marekani Donald Trump alisaini agizo la rais (executive order) lililosimamisha kwa muda wa siku 90 utoaji wa misaada nje ya Nchi, ikiwemo programu muhimu za afya kama Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI. "President's Emergency Plan for AIDS Relief " (PEPFAR).

Kusitisha Huku Progran Hizo kutaathiti Dawa za Virusi vya UKIMWI (ARV), Dawa za kifua kikuu (TB), na Dawa za malaria na Dawa za Uzazi wa Mpango..

Ukiachana na Kuathiri Upatikanaji wa Dawa Taarifa ya USAID kuhusu Kupunguza kusitisha Misaada ya Viti hivyo Kumeanza Kuleta Effect kwa Baadhi ya NGOs Mashirika Mengi..

Yanayohusika na Utoaji wa Dawa za ARV,Kifua kukuu na Ukoma,Uzazi wa Mpango,na malaria yameanza Kuyumba na wote wameanza Kutoa Notice kwa wafanyakazi wao kusubiri na Kuangalia kama Marekani itarudisha Panga kwenye ala bhasi watarudi kazini...

Takribani Wafanyakazi wa Mashirika Tanzania 2900s Wanaenda Kupoteza Kazi kutokana Na upuuzi na Ego ya Trump..

Poleni Afya, Poleni Wafanyakazj wenzangu na Mostly Poleni wagonjwa ambao mnaenda Kuathiriki kwa Order hii Isiyo na Mashiko..
_____________________________________

Waafrika Tujitegemee:
Uhuru kenyata

View: https://youtu.be/wYpSNxTxXE0

Trump ni Chizi....

Wafuasi wake wengi humu wanasukumwa na mihemko tu
 
Nchi za Afrika Zote haziwezi kutoboa kwa Disease Burden Iliyopo Ngoja Twende statistically..

  • Riport ya mwaka jana Tanzania Kwa sasa Ina WAVIU- 1.7Milion na waviu wanaotumia ARV ni 1.4 Milion
  • Waliokuwa wana Ugonjwa wa Malaria walikuwa ni zaidi ya Milion 1
  • Watoto waliopatiwa Chanjo ni zaidi ya Milion 1
  • Watu waliotumia Njia za Uzazi wa Mpango ni zaidi ya Milions
  • Wagonjwa wa TB kwa mwaka Jana walikuwa zaidi ya Laki mbili
Hakuna Nchi narudia tena Hakuna nchi wala Chama Kinachoweza Kubeba Hiyo burden Bila Kuhitaji Msaada..
unajua Chanjo moja ni Bei gani? Unajua ARV Drugs Ni Tsh ngapi Kopo Moja? Unajua Uzazi wa Mpango Hata Kidonge tu Circle mpja Ni Tsh ngapi??
Unayosema ni kweli gharama za hizo chanjo na drugs ni kubwa.
Ila most of African countries zina zaidi ya miaka60 tangu zipate uhuru,na still hazijawekeza kwenye science na research. Nchi tangu zianze kujitawala bado hazijaweza kuzalisha wataalamu wa madawa,bado hazina uwezo wakutengeneza vyandarua mpaka wapewe msada.
Ila nchi hizohizo zimeweka nguvu kubwa kwenye mambo yasiyo na tija au yenye mchango mdogo kwa ustawi wa jamii. Kwamfano Afrika kusini kuhost world cup2010 ilitumia a lot of money kana kwamba wanachi wake hawanashida katika upatikanaji wa huduma za kijamii.
Serikali za Afrika zimewekeza kwenye;
•mpira
•muziki
•siasa zisizo na mashiko
Hawawekezi kwenye kupromote gunduzi za kisayansi.
 
Trump ni Chizi....

Wafuasi wake wengi humu wanasukumwa na mihemko tu
Kama tunacheza ngoma ya chizi na sisi akina nani? Tukubali ,tukatae nchi zetu za Afrika zimejisahau sàna. Na kuna mtego wa GMO, tukiuingia ndio tumekwisha. Tahadhari nyingi zimetolewa lkn mwisho wa siku viongozi wetu watajaa na kuruhusu matumizi ya mbegu za GMO. kumbuka ukivuna mhindi wa GMO huwezi kupukuchua ukapanda uote ni lazima ununue mbegu kutoka kwao.
 
Siku ya Januari 20, 2025, Rais wa Marekani Donald Trump alisaini agizo la rais (executive order) lililosimamisha kwa muda wa siku 90 utoaji wa misaada nje ya Nchi, ikiwemo programu muhimu za afya kama Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI. "President's Emergency Plan for AIDS Relief " (PEPFAR).

Kusitisha Huku Progran Hizo kutaathiti Dawa za Virusi vya UKIMWI (ARV), Dawa za kifua kikuu (TB), na Dawa za malaria na Dawa za Uzazi wa Mpango..

Ukiachana na Kuathiri Upatikanaji wa Dawa Taarifa ya USAID kuhusu Kupunguza kusitisha Misaada ya Viti hivyo Kumeanza Kuleta Effect kwa Baadhi ya NGOs Mashirika Mengi..

Yanayohusika na Utoaji wa Dawa za ARV,Kifua kukuu na Ukoma,Uzazi wa Mpango,na malaria yameanza Kuyumba na wote wameanza Kutoa Notice kwa wafanyakazi wao kusubiri na Kuangalia kama Marekani itarudisha Panga kwenye ala bhasi watarudi kazini...

Takribani Wafanyakazi wa Mashirika Tanzania 2900s Wanaenda Kupoteza Kazi kutokana Na upuuzi na Ego ya Trump..

Poleni Afya, Poleni Wafanyakazj wenzangu na Mostly Poleni wagonjwa ambao mnaenda Kuathiriki kwa Order hii Isiyo na Mashiko..
_____________________________________

Waafrika Tujitegemee:
Uhuru kenyata

View: https://youtu.be/wYpSNxTxXE0

Bado mtasema tu, mlikuwa mnaomba duwa nzito nzito Trump apite,Kamala mkasema asichaguliwe kisa mwanamama kama samia,kwa kifupi Mungu kajibu duwa zenu,sasa subirini muanze kuanguka kama kuku wa kideri kwa vituo vya daladala, na mpoteze ajira,

Trump ni shetani ibilisi,
 
China, Russia wamepiga kimya kama hawajasikia vile!!
Kwani wao wanahusikaje kwenye hilo hayo ni masula ya ndani ya taifa la Marekani sasa China na Russia yanawahusuje?

Unataka Russia na China waingile internal affairs na policies za sovereign state Marekani?

Always China never meddles in other countries’ domestic affairs. Hiyo nii miongoni mwa foreign policies zao
 
Back
Top Bottom