Uchaguzi 2020 Nilikuwepo kwenye mkutano, sijapenda kuchangishwa fedha kinguvu

Uchaguzi 2020 Nilikuwepo kwenye mkutano, sijapenda kuchangishwa fedha kinguvu

Madaraka wanayataka wenyewe michango tuwachangie sisi na maandamano tuyafanyie sisi kipigo tupewe sisi . Kisha BATA wale wenyewe. Aaaa wazee hiyo haiwezekani kabisa
 
Unahangaika nini , nenda kwenye mkutano wa Jiwe yeye ana 1.5 tilioni kibindoni , bado ana voti namba ishirini isiokaguliwa , bado ana Kodi za walala hoi lukuki Pimbi kweli wewe.
 
Leo kama kawaida niliwahi mapema sana kwenye mkutano kusikiliza sera za mgombea wetu.

Mengi ameeleza vizuri sana japo kuna ambayo ameyarudia rudia sana...
Nenda kachangie kigodoro,huku waachie wenye mahaba na chama la wananchi
 
Kauli aliyotoa ilikuwa ya shuruti, anasema toa simu yako kisha bonyeza......hapo huoni katushurutisha?
Hii ni aibu kubwa sana kwa mtoto wa kiume kukaa unalialia ati umeshurutishwa kwa kauli hii.

Hivi wewe ukikutana na baunsa akakukazia kidogo tu si atakutatua marinda kilaini kwa mwendo huu?
 
Mkuu samahani unaweza kunisaidia namba ya kuchangia?maana mimi niko nanjilinji sikubahatika kufika huko,natanguliza shukrani zangu za dhati
Nilivyoona tunaambiwa toa simu yako ya mchina, mm sikutoa tukamwambia hakuna network
 
Kwahiyo umetoa mchango kwa nguvu! Wanekukaba au wamekupiga mtama? Je umeporwa sh ngapi kama mchango? Je umeripoti katika kituo gani cha polisi?
Kuna jamaa yangu alianza kufatisha ghafla akasikia chagua namna 4, kumbukumbu namba weka CDM2020, ghafla weka kiasi, ghafla password...... Jamaa akashtuka nkaona anaitia simu mfukoni
 
Hawajaacha ile tabia yao ya kuchangisha mafuta ya helikopta? Khalafu huwa hawalete mrejesho. Zilipatikana ngapi, zilitumika vipi, Watanzania kuweni makini na hawa matapeli wa kisiasa.

Wanawachangisha wafuasia wao baada ye wakati wanakula fedha walizo wachangisheni wanasema'kazi na bata' michango yenu ndivyo inavyo liwa hivyo kibata bata.
 
Back
Top Bottom