Ina endeleeea!!!!@
Niliishia pale nilipopambana na wale wahuni,kweli ilikuwa hatari sana kwa mtu muoga kuwekwa kati na kundi la wahuni unawajua,matukio wanayofanya mtaani ya kihuni lazima upate waiwasi,sema kilichonisaidia ni mazoezi ya taekwondo,kama ningekuwa sina uwezo wa kujua ngumi nahisi pale wangenivunja vunja,maana jamaa walikuja kuniangamiza kabisa..
Baada ya fujo zile kupita,tulihairisha kwenda kwenye maporomoko ya maji,tukaona ni bora kurudi zetu home,maana wasi wasi ulitujia labda wameenda kukusanya kundi kubwa la wahuni.
Niliendelea na cheo changu cha kaka mkuu huku nikiudhuria vipindi vyote darasani,nilipunguza uhuni sana ,nikawa nakimbiza class,walimu walinipenda sana wakanipachika jina ""mwanakondoo wa bwana""😄😄😄
Hii siku sitakuja kusahau,arusha kuna tabia ya wanafunzi kwenda picnic,nakumbuka ilikuwa jumamosi tuliandaa kwenda picnic usa River arusha kulikuwa na club huko, jina limenitoka maana ni mda sasa. tulipendaga kwenda kwenye hiyo club kuenjoy maisha.
Siku hiyo nilijiandaa vinzuri,nilivaa kama cheguevara anavovaa..
Nilipiga jinsi yangu nyeusi kali iliyonibana kwa jina arusha inaitwa mnyonyo,chini nilivaa Travolta nyeusi,juu.nikavaa sharti langu la kaki la kiscout,juunkichwani nilivaa kofia aina ya baret ya kijani,ukiniona tu mwambaaa huyoo👌😜😜,nilibeba begi langu la janssport la kijani,ndani niliweka bapa la konyagi kubwa...
Niliondoka nyumbani saa 3 asubuhi nikiwa na yule msela angu wa kitaa,tulichukua hiace mpaka usa River,tukashuka,tukatembea kwa mguu mpaka kwenye hiyo club pana umbali kiasi,tulifika saa 6 hivi.
Baada ya kufika tulikutana na shanzi kubwa la wahuni wote washule za arusha,na mademu wale wajanja wajanja wa shule za chugah,kuna wengine niliwajua wengine ndo siku ya kwanza nakutana nao,pia kulikuwa na maraia ambao walikuwa sio wanafunzi,ni wahuni tu ambao wanapenda kuudhuria club ili kuwaibia wanafunzi..
Hii story ni ndefu sana,tena inautamu sana,mbeleni ndo patamu kinoma..
Itaendeleeeea.....