Nilimpiga Mwalimu akahama shule

Nilimpiga Mwalimu akahama shule

ukimaliza tuambie na maisha yako kwa sasa yapoje baada ya kujifanya mjanja sana kipindi unasoma bila kujua umuhimu wa kuzingatia masomo hata kama muda umeisha. wengi wa type zenu, hata hapa ukituambia umefanikiwa kimaisha huwa mnajifariji tu lakini moyoni mnatamani laiti mngerudi miaka ile mngekuwa na moyo wa kupiga kitabu. wewe sio mfano mzuri kwa watu wengine.

Binafsi nilizaliwa kijijini masikini kabisa, nikasoma kwa shida, sijawahi kusoma tuition tangu nizaliwe hadi form six, hata chuo, kwasababu sikuwa na pesa. cha ajabu, wenzangu waliokuwa wanaenda kusoma tuition walikuwa chini yangu, mimi kila siku wa kwanza tu. sio kwa masomo ya shule hiyo tu, hata mock na necta ambayo haijatungwa na shule hiyo niliongoza kwenye shule nilizopita. university Mungu alinisaidia kuchagua course niitakayo kwasababu nikiwa na BBB one point six ya miaka hiyo. kuna njemba moja ilitokaga DSM ilikuwa inajaziwa kila kitu na wazazi wake kuanzia vitamutamu, sukari, tanbond/blue band na pocket money ya kutosha kuturingishia, basi kuna siku nimekaa nikaona jina lake ameomba kazi ya udereva kwenye ofisi yetu. yaani alipoishia form four alifikiri wazazi wake wataendelea kuwepo, na hawezi kuendelea form six, akaishia kutafuta kazi ya udereva. nilimwonea huruma sana.

binafsi, wewe sio mfano mzuri wa kuigwa sio tu kwa watu wengine, bali hata kwa watoto wako. na usifikiri ni sifa.
Unajua nini nilichoandika hapa ni funzo nawapa madogo,sema mimi nilikuwa muhuni mjanja darasani nilikuwa si haba,pia nimesoma mkuu ngoja hadithi hiishe then utaelewa nina cheo gani hapa jamii
 
Ina endeleeea!!!!@

Niliishia pale nilipopambana na wale wahuni,kweli ilikuwa hatari sana kwa mtu muoga kuwekwa kati na kundi la wahuni unawajua,matukio wanayofanya mtaani ya kihuni lazima upate waiwasi,sema kilichonisaidia ni mazoezi ya taekwondo,kama ningekuwa sina uwezo wa kujua ngumi nahisi pale wangenivunja vunja,maana jamaa walikuja kuniangamiza kabisa..


Baada ya fujo zile kupita,tulihairisha kwenda kwenye maporomoko ya maji,tukaona ni bora kurudi zetu home,maana wasi wasi ulitujia labda wameenda kukusanya kundi kubwa la wahuni.

Niliendelea na cheo changu cha kaka mkuu huku nikiudhuria vipindi vyote darasani,nilipunguza uhuni sana ,nikawa nakimbiza class,walimu walinipenda sana wakanipachika jina ""mwanakondoo wa bwana""😄😄😄

Hii siku sitakuja kusahau,arusha kuna tabia ya wanafunzi kwenda picnic,nakumbuka ilikuwa jumamosi tuliandaa kwenda picnic usa River arusha kulikuwa na club huko, jina limenitoka maana ni mda sasa. tulipendaga kwenda kwenye hiyo club kuenjoy maisha.

Siku hiyo nilijiandaa vinzuri,nilivaa kama cheguevara anavovaa..
Nilipiga jinsi yangu nyeusi kali iliyonibana kwa jina arusha inaitwa mnyonyo,chini nilivaa Travolta nyeusi,juu.nikavaa sharti langu la kaki la kiscout,juunkichwani nilivaa kofia aina ya baret ya kijani,ukiniona tu mwambaaa huyoo👌😜😜,nilibeba begi langu la janssport la kijani,ndani niliweka bapa la konyagi kubwa...

Niliondoka nyumbani saa 3 asubuhi nikiwa na yule msela angu wa kitaa,tulichukua hiace mpaka usa River,tukashuka,tukatembea kwa mguu mpaka kwenye hiyo club pana umbali kiasi,tulifika saa 6 hivi.

Baada ya kufika tulikutana na shanzi kubwa la wahuni wote washule za arusha,na mademu wale wajanja wajanja wa shule za chugah,kuna wengine niliwajua wengine ndo siku ya kwanza nakutana nao,pia kulikuwa na maraia ambao walikuwa sio wanafunzi,ni wahuni tu ambao wanapenda kuudhuria club ili kuwaibia wanafunzi..


Hii story ni ndefu sana,tena inautamu sana,mbeleni ndo patamu kinoma..
Itaendeleeeea.....
 
Back
Top Bottom