Nilisafiri kwa pikipiki Dar mpaka Tabora

Asante umenitoa woga, kesho naanza kwa kutoka Iringa hadi Tosamaganga, safari yangu ndefu ya kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini isijekuwa wale waenda mbio bila life assurance. Mi napenda kusafiri lakini sio kufa, kuna kikundi cha watu wa ajabu niliwahi kukutana nao Mkomazi wakiwa kwenye mwendo ambao sidhani kama dharura ikitokea uhai wako una guarantee. Ngoja niwacheki hawa ulioniambia, thanks!
 
Mzee aibu nami niliunge na kaTVS kangu hapo [emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu polepole ndio mwendo kuna siku utapata kama hizo.

Kama unapenda Adventure za pikipiki uwe unaenda Pale Tanganyika Packers Jumapili hata kubadilishana Mawazo na wadau kwenye michezo ya pikipiki.
Tatizo mimi nina TVS mkuu sasa hao jamaa mizigo yao wanaweza kuniacha njiani na kibaskeli changu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa wengi ni watu wazima tena wanaojitambua. Vijana wapo wachache sana, sisi vijana mwisho wa kucheza ni Tanganyika packers.
 
mkuu umetumia lita ngapi,na muda gani?
manake mimi luti za dar mwanza ni nyingi kama vp na mm nimenye boxer yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Mara ya kwanza jaribu route za umbali wa kawaida kama Dar kwenda Moro.

Njia yenye changamoto sana ni Dar-Morogoro-Iringa-Mbeya hii ina magari mengi sana na kuna madereva wengine hawajali hivyo unakuwa unaendesha kwa kujiami.
 
Dah hongera mkuu ,hii kitu naiogopea magari makubwa njiani namna yanavyokupita ,unaweza jikuta mtaroni na huwa hawathamini pikipiki ,

Vp hii changamoto ulikabiliana nayo vp ,maana ujanja wangu pikipiki mwisho mjini,
Una boxer upitwe na gari kubwa
 
Mkuu hongera sana kwa hiyo adventure I wish ningekujoin ila poa kuna siku na mimi ntasafiri umbali mrefu na mnyama wangu kiboko ya boxer (discover 4valve)

hua naiita the navigator wenye boxer hua wananikoma barabarani na hapa nna mpango niibomoe yote ili niifanyie overhaul

anayejua fundi mzuri kwa dar anifahamishe tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…