Nilitahadharisha hapa kuwa 'Kesi' imemkalia vibaya 'Mwamba' na hachomoki kirahisi nikaishia Kushambuliwa

Ukweli ndio huo.... Mbowe atakuwa mshindi either way.

Makosa anayoshitakiwa nayo kama akitiwa hatiani atakwenda jela sio chini ya miaka 15. Jamhuri haina huo ubavu wa kumuweka Mbowe gerezani kwa miaka 15. Na kama wakijaribu, hawataweza ku-sustain hiyo state.
 
Pia itapendeza zaidi kama utakuja kukanusha haya hapo baadae huo utakuwa ni uungwana zaidi sio kujipa sifa kwa jambo ambalo liko wazi mno kwa asiyependa haki.
 
Mkuu bahati nzuri unafahamu kuwa ni kesi ya Kimkakati.Maana yake sheria siyo kipaumbele kwao.Jana imedhibitisha hivyo.Kwa hiyo, ushauri au maoni yako yasingesaidia chochote kwa kuwa wenye nia OVU tayari wanamaamuzi yao.
Lakini imeandikwa,mshahara wa dhambi NI MAUTI,walipaswa wawe wamejifunza.
 
Yaani kwa Upuuzi wako huu naamini kuna 'Majuha' kadhaa hapa watakuamini na kujipa Moto.

Endelea tu Kuwadanganya na Kujidanganya ila wenye Akili tumejua 'Mwamba' yameshamkuta.
Endelea kuamini unachoamini lakini nakuhakikishia hakuna kesi hapo na Mbowe atatoka bila matatizo
 
Kwa hiyo kaonewa sio?
 
Akikutwa na hatia, hukumu ya Ugaidi akipona sana ni Life sentence au Kunyongwa hadi kufa kisheria. CHADEMA walichukulia hii case kiutani utani, sasa wanaona mtu karibia anaelekezwa kibra.
Ikiwa ndivyo, Mungu wetu ambaye tunamtumikia aweza kutuokoa katika tanuri ya moto mkali; tena atatuokoa mikononi mwako, ee mfalme. Danieli 3:17
 
Akikutwa na hatia, hukumu ya Ugaidi akipona sana ni Life sentence au Kunyongwa hadi kufa kisheria. CHADEMA walichukulia hii case kiutani utani, sasa wanaona mtu karibia anaelekezwa kibra.
Ikiwa ndivyo, Mungu wetu ambaye tunamtumikia aweza kutuokoa katika tanuri ya moto mkali; tena atatuokoa mikononi mwako, ee mfalme.
 
Kesi ya ugaidi hukumu ni kunyongwa hangaya asisite kutia wino
Ndugu furaha yako ya kishetani, umeianza mapema mno, nawe waweza kujikuta umeishia jangwani kama yule wa Burigi. AMEN
 
Haki inawekwa 'kapuni' kila kukicha!
Uongo na uzandiki umetamalaki!
Maneno ya kikatili yaliyojaa uongo nayo yametamalaki!
Watu wenye 'ndimi za moto' wameandaliwa kutoa ushuhuda wa 'yule mwovu'
Asiye na hatia yupo mikononi mwa mbwa mwitu waovu na makatili!
Haki itatamalaki kwa mkono wa Mwenyezi Mungu kupitia Malaika wake, time will tell
Ila watambue dhambi, kufuru na laana hizi zitaandamana nao hadi ktk lile Ziwa la Moto waliloandaliwa wao na vizazi vyao.
 
Tukiwaambia hawajui Kufikiri wananuna.
Sasa ww maamuma unajua kipi cha kufikiri.. kwakukusaudia ili uondoke na ujinga ulionao.. nenda youtube search maria space ya jana upate somo kutoka kwa adv matata na fatma karume naamini hatarudia tena kuwa mpuuuz kwenye mambo usiyo na upeo nayo.
 
Nilitukanwa sana hapa na Wafuasi wake wakati GENTAMYCINE nilikuwa na nia njema nae tu ili asaidiwe Kiushauri na Kimawazo na Wadau mpaka Wataalam wa Kisheria.

Sasa kuanzia leo tutaheshimiana vizuri.
Usipende jambo baya litokee kwa mtu fulani ili litimie ulilolisema au kuliota. Huo ni ushetani sawa na mashetani wengine tu tunaowaona wakiendeleza ushetani. Ukiota mtu X kafa ukaja hadharani ukasema "Jamani nimeota X kafa, naomba tumuombee asife". Wakajitokeza watu kukupinga, kwamba usituletee uchoro hapa, hafi mtu. Baada ya siku chache kupita yule uliyemuota akifa kweli usishangilie eti "mimi nilisema atakufa mkinibishia, sasa uneni nilichosema kimekuwa kweli, na kuanzia leo tutaheshimiana vizuri". Hapo utakuwa hutendi haki na ni ukosefu wa hekima wa hali ya juu kabisa. Wewe unakuwa siyo binadamu wa kawaida. Kwanza ukiota mtu kafa badala ya kwenda kujimwambafai kwamba wewe ni muotaji hodari, ni vema ukiota mtu kafa ingia kwenye maombi ili hilo uliloota lisitokee. Ni ajabu kushangilia ndoto yenye machungu kwa wengine kuwa kweli. Jifunze kuwa na ubinadamu ndugu yangu.
 
Usipende jambo baya litokee kwa mtu fulani ili litimie ulilolisema au kuliota. Huo ni ushetani sawa na mashetani wengine tu tunaowaona wakiendeleza ushetani. Ukiota mtu X kafa ukaja hadharani ukasema "Jamani nimeota X kafa, naomba tumuombee asife". Wakajitokeza watu kukupinga, kwamba usituletee uchoro hapa, hafi mtu. Baada ya siku chache kupita yule uliyemuota akifa kweli usishangilie eti "mimi nilisema atakufa mkinibishia, sasa oneni nilichosema kimekuwa kweli, na kuanzia leo tutaheshimiana vizuri". Hapo utakuwa hutendi haki na ni ukosefu wa hekima wa hali ya juu kabisa. Wewe unakuwa siyo binadamu wa kawaida. Kwanza ukiota mtu kafa badala ya kwenda kujimwambafai kwamba wewe ni muotaji hodari, ni vema ukiota mtu kafa ingia kwenye maombi ili hilo uliloota lisitokee. Ni ajabu kushangilia ndoto yenye machungu kwa wengine kuwa kweli. Jifunze kuwa na ubinadamu ndugu yangu.
 
Nilikuwa najidanganya kwamba gentamycine ni mtu smart kumbe nilikuwa naota, yaani hujui ni kwa nini uzi wako ulifutwa ?, pole sana na hao mafisiem wenzako, nyinyi na mahakama zenu mnaenda kuaibika mchana kweupe
 
nimekuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…