Sheikh mbona huulizi Qurani ina vitabu vingapi na kwanini baadhi ya aya ziliondolewa ebu tupe hapo elimu na Sisi tuelimike.
Hili la vitabu vingapi. Inabidi ulielezee wewe, kwangu jipya hili. Huo ujinga kwetu haupo, Qur'aan ni kitabu kimoja pweke.
Ukisoma kwenye fani ya Qur'aan kuna somo la "Nasikh wa al Mansukh" yaani linaelezea aya zilizo futa na zilizofutwa. Huu ulikuwa ni utaratibu wa Allah katika kuwalea waja wake,analeta aya fulani kwa muda fulani kisha lengo likitimia anaifuta kwa kuleta nyingine, haya yote aliyafanya mtume kwa amri toka kwa Allah.
Vipi kuhusu Salman Rashad aliyetoa siri za uozo wa qurani kwenye kitabu chake cha satanic verses.
Sasa huyu Salman Rushd huyu alipotosha juu ya aya za shetani maana alisema kuna aya za shetani jambo ambalo si kweli. Laiti mngekuwa mnasoma hii Qur'aan hata nyinyi mngemshangaa Mtu huyo.
Quran si mnasema ina aya 114 mbona ziko nyingi tu zingine za hovyo na zikafichwa kwa sababu ni za hovyo zaidi ya uhovyo ulizonazo hizi mnazosomeshwa sasa.
Haya ndiyo matatizo ya kutokusoma. Nani amekwambia Qur'aan ina aya 114 ? Qur'aan ina sura 114 siyo aya 114. Rekebisha hapo.
Hizo nyingi ziko wapi ?
Biblia ina vitabu 73,kuna vingine sio vitabu vya biblia na havikubaliki kama sehemu ya biblia kama vile kitabu cha enoch kwa sababu kipo kama sehemu ya wasumeria na hadithi zao na hakina uvuvio wa roho Mtakatifu.
Biblia haijaandikwa na mtu mmoja au sio taasisi moja ndio imekaa na kutunga ila na mkusanyiko wa matukio ya tangu kuumbwa kwa ulimwengu mpaka wakati wa Yesu na baada ya Yesu(Ufunuo)
Sasa ilikuwaje vikawa 73 kwa muda wote huo na mkaja kuvipunguza mpaka kufikia 66 ? Hicho kitabu cha kina ujumbe gani mpaka mkakitoa ? Kilitolewa na nani ?
Sifa ya kitu kuwa na uvuvio wa roho mtakatifu ni ipi ?
Hapo kwenye waandishi wengi ndiyo kumezua uongo na uchafuzi wengi, sababu wote hao hawakumuona Yesu wala wanafunzi wake, hao waandishi haya maandiko walikuwa wanayatoa wapi ?
Swali dogo kwako, Biblia ya kwanza iliandikwa lini ?
Qurani haijaandikwa na muhamad yeye alikuwa anaweka watu waandike yale anayoyasema na kuna historia zipo maandiko mengine yalipotea na kwa sehemu kubwa mengi alikuwa anayasema watu wake aidha wanaandika na wengine kukariri sasa hapo mnasemaje kitabu chenu kimekamilika.
Safi gani andiko gali lilipotea ?
Sasa kama walikuwa wanaandika na wengine wanakariri, vipi yapotee wakati waandishi walikuwa wengi na walio kariri walikuwa wengi ? Maana hifadhi ya kuandika huwa ni yenye kudumu. Sasa unaweza kuniambia au kunipa ushahidi wa kuonyesha wanafunzi wa Yesu walikuwa wakiyaandika mafundisho ya Yesu ? Kama hawakuwa wakiyaandika, haya ya leo mmeyapata wapi ?
Na baadhi ya waandishi wake wala hawakuwa waislamu walifanya tu kazi ya kuandika.Lakini mara zote
Hapa unatakiwa uweke ushahidi, hakuna muandishi ambaye hakuwa muislamu. Kwanza aisyekuwa muislamu angeanzaje kuandika ?
Maandiko ya biblia wewe huyaelewi au unajitoa ufahamu kwa sababu unajua utashindwa hoja na ukishindwa hoja utaona aibu kusalia kwenye uislamu.
Sasa kama siyaelewi si mnanielewesha ? Wenyewe maandiko yenu mnayakimbia hamyatetei zaidi ya kutoa maelezo ya jumla na yasiyo jibu hoja zangu. Nilichokiona ni kuwa nyinyi Biblia yenu hamuisomi.
Kuhusu hoja kama tungekuwa tunashindana, hamna hona ya kunishinda mimi, wala sihofii kushindwa kadhalika.