Nilitaka kumuoa binti wa Dini tofauti na yangu vita kubwa ikaibuka. Kuna kitu gani kati ya hizi dini mbili?

Nilitaka kumuoa binti wa Dini tofauti na yangu vita kubwa ikaibuka. Kuna kitu gani kati ya hizi dini mbili?

Unawezaje kumuamini Mungu bila yeye kukupa muongozo ? Alikuwa anamuamini vipi Mungu ?

Siyo tu Ibrahimu bali mpaka nabii Nuhu ambaye alikuwa kabla yake alikuwa Muislamu. Anasema Allah mtukufu :

71. Wasomee khabari za Nuhu alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu!Ikiwa kukaa kwangu nanyi na kukumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu kunakutieni mashaka basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Nanyi tengezeni mambo yenu pamoja na washirika wenu, na wala mambo yenu yasifichikane kwenu.Kisha nihukumuni, wala msinipe muhula.

72. Lakini mkigeuka, basi mimi sikukuombeni ujira. Ujira wangu hauko ila kwa Mwenyezi Mungu. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu. (Yunus : 71-72)

Akasema tena kuhusu Ibrahiim ;

130. Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema.

131. Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote.

132. Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu. (al-Baqarah : 130-132)

Kwa ufupi hakuna nabii wala mtume ambaye hakuwa Muislamu.

Uislamu aliokuja nao mtume Muhammad umetofautiana na walio mtangulia katika sheria ila imani na itikadi zao ni sawa.
Kuamini Mungu hakumaanishi kuwa na dini.

Wote unaowataja hata kwenye biblia wapo.( Ukristo)
 
Allah nature yake ni physical being , kulingana na waislamu nguli wanasema Allah ana mguu ,mikono , USO, vidole n.k na waislamu wanasema pia mguu wake na umbo lake halifanani na kitu chochote


Allah pia anakazia anasema akitaka mke anachukua Malaika au hori ndio ujue ni mwanaume na Koran yote Allah anajiita he na sio she
Hivi we unajua unachokiandika kweli na pia ninawasiwasi na kujua kingereza kingereza chako ujui kwanini Allah au God inawasilishwa na he na si she au nyie kwenye ukiristo Mungu hua anawakilishwa na she!? Such a shame
 
Kama umeshaelewa utofauti wa Allah na Jehovah hapo sawa

Shida gani unapata Mungu akikwambia ata yupo mara 1000 ?
Unataka kumpangia kuwa unavyotaka wewe au?
Mungu ni mmoja na hana mshirika asa unaposema Mungu amegawanyika inamaanisha kwamba Mungu ana washirika kwa mujibu wako ama vip?
 
Dooh umesikia kwa muislamu gani ? maana kuna sura ktk Quran inaeleza Allah hafananishwi na chochote sasa unavyoniambia miguu mikono nashangaa sana na hayo mambo ya mke pia utakuwa Umesikia nilidhani umesoma mahali kwenye vitabu vyetu
Hana lolote uyo anaongea uzushi tu Mungu hafananishwi na lolote wala chochote wao ndo wanasema Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake
 
Hivi we unajua unachokiandika kweli na pia ninawasiwasi na kujua kingereza kingereza chako ujui kwanini Allah au God inawasilishwa na he na si she au nyie kwenye ukiristo Mungu hua anawakilishwa na she!? Such a shame
Ulitakiwa kujua mada ilipo anzia , sio unadandia tu
Sasa allah anaposema akitaka mke , maana yake nini
 
Sasa si ndiyo unatuonyesha na mtuambie hayo maandiko yenu kwanini yanapingana...?

Kingine hapa sijaleta ubishi ningekuwa mbishi ingekuwa ni kinyume chake.
Suratul iklaas

1.Kwa jina la Mwenyezi Mungu,
Mwingi wa rehema, Mwingi wa ukarimu.
2. Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni
Mmoja.
3. Mwenyezi Mungu Asiyehitaji,
Ambaye wote wanahitaji Kwake.
4. Hakuzaa wala Hakuzaliwa.
5. Wala Hana anayefanana naye hata
mmoja.
 
Ukiwa na hoja ya kujadiliana na mimi au kukosoa kielimu nilicho kiandika nijulishe ila sijadiliani na wajinga walio pea.

Kwani ujumbe ulio kuja toka kwa hao unao dai Waarabu uliwahusu Waarabu pekee, hakuna nabii aliyekuwa mzungu kijana.

Kingine naomba unipe sababu tano ambazo zinaonyesha ulazima wa uwepo nabii Muafrika ?

Mitume na manabii walikuwa wanapelekwa sehemu kwa sababu maalumu, nabii Musa alipelekwa kwenye jamii ambazo zilioza katika madhambi, kadhalika nabii Issa kadhalika nabii Muhammad alipelekwa kwa watu ambao maovu yao yalikuwa makubwa, sasa usifikiri unabii unapelekwa tu kiholela holela na kuna sababu nyingi hii nimekupa moja katika sababu nyingi.

Wasome Wana wa Israeli walivyokuwa waovu uovu ambao ulikuwa haupatikani sehemu yoyote,sasa sababu mnaendekeza urangi mtaendelea kuwa wajinga mpaka mnakufa.

Shida yenu nyinyi mnaleta uafrika bila kuangalia haja ya jambo husika, sasa elimu haiko hivyo, na mnayachukulia mambo juu juu. Wajinga sana nyinyi.
Mkuu Nabii Adam alipelekwa kwa watu gani waovu
 
Sijui hatima yangu itakua ipi kat yangu na mpenzi wangu Ester
 
Yeye akiwa ni Muislam na mie Mkristo;

Alikuwa pisi haswa, mtoto mkaree kila angle na anayajua mapenzi haswa, nikasema tabu za nini hasa ukizingatia binti mwenyewe ananitii kila nnalomwambia, sikuwa na upinzani wowote kwake, najipigia mwenyewe tu ki uhakika.

Sasa nilivyotangaza tu kumuoa na kuwaambia ndugu na jamaa kwamba kuna sehemu nimenasa na sasa nabeba jiko jumla hapo sasa ndio vita vikazuka, mwanzo nikaona ni mambo ya kawaida "jamaa wanaingilia maisha ya watu tena, hawa hawanijui hawa?" Lakini nikashangaa wazazi wote pande mbili wanapinga, wajomba wameshika mabango kwamba watu wa dini ile nyingine hakuna kabisa hawafai, nikasema eeh maji mazito kuliko damu ya mtume?

Binti alikuwa so so down, hana mzuka kabisa, mie nafosi bibie tulia wala usiwe na hofu dini tumeletewa na mabeberu tu, lakini ikamshinda nguvu maskini binti wa watu analia, maza ake nae kaja juu anasema kijana mkristo hakanyagi hapa kwangu, huba likakosa connection kabisa kimzaa mzaa tu, tukawa tunakulana tu na binti akawa anasema haoni future sa itakuaje? Nikamwambia basi tuzae tu wataelewa, akasisitiza mtume alishapinga kuzaa nje ya ndoa, basi ikaishia hivyo tu na sasa binti yupo na shekhe wake msoma visomo.

Hivi huwa kuna bifu la chini chini kati ya hizi dini mbili? Na raia huWa hawasemi au ni nini? Why wakule ni wakule na wa huku ni wa huku, hakuna kuingiliana?
Hahaa! Mi mama ni muislam baba ni mkatoliki but familia ipo na sasa na Mimi nimeoa muislam
 
Sahivi kuna mademu ukionesha interest nae tu especially wa kiislam anakuuliza "we dini gani"?
 
Kuna shida gani kama amegawanyika?
Ostaz Mokiti hebu nyoosha maelezo acha kuwa mkali.

Maana haya ndio mambo ambayo waislamu hawayaelewi na sio uislamu wao kama ambavyo huwa unawasingizia.

Sasa hebu mfafanulie ndugu yangu hapo
Kwamba inakuwaje nafsi 1=3 ?
Na kuna ubayagani kusema ni 1 na kuacha kusema 3, ikiwa hizi 3 ni 1?
Na kwanini iabudiwe nafsi 1katika 3, ikiwa zinakamilishwa na 3?
 
Mkuu Nabii Adam alipelekwa kwa watu gani waovu
Kwanza nikupe faida katika hili, wanachuoni wamegawanyika sehemu mbili juu ya hili la baba yetu Adamu, wapo wanao sema ni nabii kwa sababu alipewa muongozo wa kuishi na watu wake yaani familia yake, mke na watoto wake na wapo wanao sema hakuwa nabii, na mimi msimamo wangu huu wa wanazuoni wa pili kwamba hakuwa nabii, na nabii wa kwanza alikuwa ni Nuhu na hii ni baada ya kudhihiri USHIRIKINA.
 
Ostaz Mokiti hebu nyoosha maelezo acha kuwa mkali.

Maana haya ndio mambo ambayo waislamu hawayaelewi na sio uislamu wao kama ambavyo huwa unawasingizia.

Sasa hebu mfafanulie ndugu yangu hapo
Kwamba inakuwaje nafsi 1=3 ?
Na kuna ubayagani kusema ni 1 na kuacha kusema 3, ikiwa hizi 3 ni 1?
Na kwanini iabudiwe nafsi 1katika 3, ikiwa zinakamilishwa na 3?
Huo ni utaratibu wake Mungu muweza wa yote kajiwekea , hakuna linalomshinda
 
Habari ndugu Kisai
, inaonekana una elimu na ujuzi kuhusu dini yako kwani majibu yako yamejikita zaidi kutoka kwenye chanzo rasmi yaani kitabu chako.Pia unatumia zaidi uhalisia na siyo hisia katika majibu yako. Nina maswali yafutayo:

  1. Hizi alama za mwezi na nyota kwenye nyumba zenu za ibada zilitoka wapi?? Historia yake ikoje??.
  2. Je, uwepo wake ni sahihi kwa mujibu wa kitabu unachokiamini??
  3. Zilikuwepo enzi ya Mtume au baada yake??
  4. Je, Mtume mwenyewe amewahi kuzilezea uwepo wa hizi alama??.
Mwisho: Unawezaje kutenganisha dini na utamaduni?? Mfano utamaduni wa Kiarabu na Uislamu. Au Utamaduni wa Kimagharibi na Ukristo. Utamaduni wa Kiyahudi na Uyahudi.Utamaduni wa Kihindi na Uhindu.Utamduni wa nchi nyingi za Asia na Ubuda (Buddhist )

Samahani sana
kwa kuchukua muda wako na kama nitakuwa nimekukera nimeleta kejeli na kukuudhi. Ahsante.
 
Tupo kwenye boti moja chief, hata mimi nataka kuoa muislam kindaki ndaki tatizo dini yao hairuhusu kuolewa na mtu wa dini nyingine. Japo mwanaume wa kiislam anaruhusiwa kuoa mwanamke wa kikristo na kiyahudi.

Ulichokosea ni kutomtia mimba huyo mrembo, ilitakiwa ucheze faulo tu kibabe basi upinzani ungekosa nguvu. Wangu is a doctor hata kufunga offside goal ya mimba ni ngumu.

Maajabu ni kwamba mtu akiongezewa damu hospitali haulizi kama hii ni ya mkristo au muislam. Hizi dini za kigeni zina tutenganisha kijamii badala ya kutuunganisha.
aise umeongea kitu hadi nimefurahi.Ni kweli ukiongezewa damu huwa hakuna damu ya mkristo na Muislam.Watu hawajui tu dini ni mapito tu au tuseme ni njia mbali mbali kumtafuta mungu.
 
Back
Top Bottom