Englishlady
JF-Expert Member
- Apr 11, 2013
- 2,736
- 3,644
Kuamini Mungu hakumaanishi kuwa na dini.Unawezaje kumuamini Mungu bila yeye kukupa muongozo ? Alikuwa anamuamini vipi Mungu ?
Siyo tu Ibrahimu bali mpaka nabii Nuhu ambaye alikuwa kabla yake alikuwa Muislamu. Anasema Allah mtukufu :
71. Wasomee khabari za Nuhu alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu!Ikiwa kukaa kwangu nanyi na kukumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu kunakutieni mashaka basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Nanyi tengezeni mambo yenu pamoja na washirika wenu, na wala mambo yenu yasifichikane kwenu.Kisha nihukumuni, wala msinipe muhula.
72. Lakini mkigeuka, basi mimi sikukuombeni ujira. Ujira wangu hauko ila kwa Mwenyezi Mungu. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu. (Yunus : 71-72)
Akasema tena kuhusu Ibrahiim ;
130. Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema.
131. Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote.
132. Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu. (al-Baqarah : 130-132)
Kwa ufupi hakuna nabii wala mtume ambaye hakuwa Muislamu.
Uislamu aliokuja nao mtume Muhammad umetofautiana na walio mtangulia katika sheria ila imani na itikadi zao ni sawa.
Wote unaowataja hata kwenye biblia wapo.( Ukristo)