Nilitaka kumuoa binti wa Dini tofauti na yangu vita kubwa ikaibuka. Kuna kitu gani kati ya hizi dini mbili?

Kuamini Mungu hakumaanishi kuwa na dini.

Wote unaowataja hata kwenye biblia wapo.( Ukristo)
 
Hivi we unajua unachokiandika kweli na pia ninawasiwasi na kujua kingereza kingereza chako ujui kwanini Allah au God inawasilishwa na he na si she au nyie kwenye ukiristo Mungu hua anawakilishwa na she!? Such a shame
 
Kama umeshaelewa utofauti wa Allah na Jehovah hapo sawa

Shida gani unapata Mungu akikwambia ata yupo mara 1000 ?
Unataka kumpangia kuwa unavyotaka wewe au?
Mungu ni mmoja na hana mshirika asa unaposema Mungu amegawanyika inamaanisha kwamba Mungu ana washirika kwa mujibu wako ama vip?
 
Dooh umesikia kwa muislamu gani ? maana kuna sura ktk Quran inaeleza Allah hafananishwi na chochote sasa unavyoniambia miguu mikono nashangaa sana na hayo mambo ya mke pia utakuwa Umesikia nilidhani umesoma mahali kwenye vitabu vyetu
Hana lolote uyo anaongea uzushi tu Mungu hafananishwi na lolote wala chochote wao ndo wanasema Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake
 
Hivi we unajua unachokiandika kweli na pia ninawasiwasi na kujua kingereza kingereza chako ujui kwanini Allah au God inawasilishwa na he na si she au nyie kwenye ukiristo Mungu hua anawakilishwa na she!? Such a shame
Ulitakiwa kujua mada ilipo anzia , sio unadandia tu
Sasa allah anaposema akitaka mke , maana yake nini
 
Sasa si ndiyo unatuonyesha na mtuambie hayo maandiko yenu kwanini yanapingana...?

Kingine hapa sijaleta ubishi ningekuwa mbishi ingekuwa ni kinyume chake.
Suratul iklaas

1.Kwa jina la Mwenyezi Mungu,
Mwingi wa rehema, Mwingi wa ukarimu.
2. Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni
Mmoja.
3. Mwenyezi Mungu Asiyehitaji,
Ambaye wote wanahitaji Kwake.
4. Hakuzaa wala Hakuzaliwa.
5. Wala Hana anayefanana naye hata
mmoja.
 
Mkuu Nabii Adam alipelekwa kwa watu gani waovu
 
Sijui hatima yangu itakua ipi kat yangu na mpenzi wangu Ester
 
Hahaa! Mi mama ni muislam baba ni mkatoliki but familia ipo na sasa na Mimi nimeoa muislam
 
Sahivi kuna mademu ukionesha interest nae tu especially wa kiislam anakuuliza "we dini gani"?
 
Kuna shida gani kama amegawanyika?
Ostaz Mokiti hebu nyoosha maelezo acha kuwa mkali.

Maana haya ndio mambo ambayo waislamu hawayaelewi na sio uislamu wao kama ambavyo huwa unawasingizia.

Sasa hebu mfafanulie ndugu yangu hapo
Kwamba inakuwaje nafsi 1=3 ?
Na kuna ubayagani kusema ni 1 na kuacha kusema 3, ikiwa hizi 3 ni 1?
Na kwanini iabudiwe nafsi 1katika 3, ikiwa zinakamilishwa na 3?
 
Mkuu Nabii Adam alipelekwa kwa watu gani waovu
Kwanza nikupe faida katika hili, wanachuoni wamegawanyika sehemu mbili juu ya hili la baba yetu Adamu, wapo wanao sema ni nabii kwa sababu alipewa muongozo wa kuishi na watu wake yaani familia yake, mke na watoto wake na wapo wanao sema hakuwa nabii, na mimi msimamo wangu huu wa wanazuoni wa pili kwamba hakuwa nabii, na nabii wa kwanza alikuwa ni Nuhu na hii ni baada ya kudhihiri USHIRIKINA.
 
Huo ni utaratibu wake Mungu muweza wa yote kajiwekea , hakuna linalomshinda
 
Habari ndugu Kisai
, inaonekana una elimu na ujuzi kuhusu dini yako kwani majibu yako yamejikita zaidi kutoka kwenye chanzo rasmi yaani kitabu chako.Pia unatumia zaidi uhalisia na siyo hisia katika majibu yako. Nina maswali yafutayo:

  1. Hizi alama za mwezi na nyota kwenye nyumba zenu za ibada zilitoka wapi?? Historia yake ikoje??.
  2. Je, uwepo wake ni sahihi kwa mujibu wa kitabu unachokiamini??
  3. Zilikuwepo enzi ya Mtume au baada yake??
  4. Je, Mtume mwenyewe amewahi kuzilezea uwepo wa hizi alama??.
Mwisho: Unawezaje kutenganisha dini na utamaduni?? Mfano utamaduni wa Kiarabu na Uislamu. Au Utamaduni wa Kimagharibi na Ukristo. Utamaduni wa Kiyahudi na Uyahudi.Utamaduni wa Kihindi na Uhindu.Utamduni wa nchi nyingi za Asia na Ubuda (Buddhist )

Samahani sana
kwa kuchukua muda wako na kama nitakuwa nimekukera nimeleta kejeli na kukuudhi. Ahsante.
 
aise umeongea kitu hadi nimefurahi.Ni kweli ukiongezewa damu huwa hakuna damu ya mkristo na Muislam.Watu hawajui tu dini ni mapito tu au tuseme ni njia mbali mbali kumtafuta mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…