Nilitaka kumuoa binti wa Dini tofauti na yangu vita kubwa ikaibuka. Kuna kitu gani kati ya hizi dini mbili?

Hajasema Allah sio Mungu bali Allah sio Yehovah.
 
MI dini kwangu sio kipaumbele watoto wenyewe walikua watachagua wenyewe .
 
Ibrahimu hakuwa na dini.

Alimwamini Mungu tu.

Dini zilikuja baadae sana.

Kwani uislamu si umeletwa na Muhammed? Sasa Ibrahim alikuja kuishi baadae?
Unawezaje kumuamini Mungu bila yeye kukupa muongozo ? Alikuwa anamuamini vipi Mungu ?

Siyo tu Ibrahimu bali mpaka nabii Nuhu ambaye alikuwa kabla yake alikuwa Muislamu. Anasema Allah mtukufu :

71. Wasomee khabari za Nuhu alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu!Ikiwa kukaa kwangu nanyi na kukumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu kunakutieni mashaka basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Nanyi tengezeni mambo yenu pamoja na washirika wenu, na wala mambo yenu yasifichikane kwenu.Kisha nihukumuni, wala msinipe muhula.

72. Lakini mkigeuka, basi mimi sikukuombeni ujira. Ujira wangu hauko ila kwa Mwenyezi Mungu. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu. (Yunus : 71-72)

Akasema tena kuhusu Ibrahiim ;

130. Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema.

131. Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote.

132. Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu. (al-Baqarah : 130-132)

Kwa ufupi hakuna nabii wala mtume ambaye hakuwa Muislamu.

Uislamu aliokuja nao mtume Muhammad umetofautiana na walio mtangulia katika sheria ila imani na itikadi zao ni sawa.
 
KWA HAPA TANZANIA TENA HAINA NGUVU KAMA HUKO MASHARIKI YA KATI, WAKATI MWINGINE KAMA MMEPENDANA INATAKIWA MCHUKUANE HIVYO HIVYO WAZAZI WATAWAELEWA TU!
 
Ukitaka kuharibu jamii basi ruhusu mahusiano ya kimapenzi baina ya imani mbili tofauti.

Ukiona mtu ana uhusiano wa kimapenzi na mtu wa imani nyingine huyo hajitambui au anajiendekeza. Huu ukweli mchungu.
Ukweli upi mkuu?
 

Na sie wanawake wa Kikristo tuna mahaba mno na wanaume wa Kiislam sasa sijui tufanyaje???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…