Nilitumia miaka mitano ya kujenga nyumba ya ndoto yangu, inawezekana vijana tusilale

Nilitumia miaka mitano ya kujenga nyumba ya ndoto yangu, inawezekana vijana tusilale

Kwanza ongera sna kwa kutimiza NYUMBA ya ndoto yako.maneno bila kapicha bado hakajanoga.itapendeza picha za msingi hadi finishing najua utakuwa nazo ili kutufanya tuwe na wivu ktk maendeleo.ila pia 1.8m kuweka kipindi kilichopendwa uko vzuri
 
Hongera sana mkuu.
Hii ni inspiration nzuri kwa vijana wanaotamani kajenga. Wajue inawezekana.
Ila mkuu jiandae kupokea matusi, kebehi, kejeli na kila kitu. Humu wamejaa ma-negative thinkers wanaopendelea kuona habari za kukatisha tamaa, matatizo, kulia njaa, na zinazofanana na hizo; Wasikufanye uvunjike moyo ku-share mafanikio yako humu JF. Hongera sana kwa mara nyingine mkuu!!
Ndio tatizo la watu humu mkuu, Ila tunaenda sawa
 
Sio lazima iwe mil 1.8, inaweza kuwa hata 50k

Mkuu tuwe realistic kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake ,kuna wenye kusave elfu moja kwa mwezi ,mwingine 20k ,mwingine 1m ,wewe 1.8m ,mwingine 10m etc.

Huyo anayesave 50k kwa mwezi ina maana ndani ya miaka mi5 ndio ana 3m ambayo haitoshi hata kukamilisha tofali za nyumba achilia mbali kununua kiwanja.

Hapo ndipo Inspirantional speaker wanapofeli,kitu kilichowork kwako kinaweza kisifanye kazi kwa mwingine.
 
Huu uzi haufai kabisa unazungumzia 1.8m wakati watu kuipta 1500000 kwa mwezi ni ngumu
Kifupi hatujajifunza kitu sana sana unaturingishia upigaji wako katika nchi yetu
Ni biashara gana au kazi gani uifanye ulipwe hela nyingi kwa mwezi hadi uwe na reseve ya 1.8m baada ya kila kitu
ÑAPENDEKEZA UZI UFUTWE MARAMOJA NA MODS HATUJAJIFUNZA CHOCHOTE
Nilitoa angalizo hapo juu kuwa Kama una wivu na husda huu uzi usiusome
 
Mkuu tuwe realistic kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake ,kuna wenye kusave elfu moja kwa mwezi ,mwingine 20k ,mwingine 1m ,wewe 1.8m ,mwingine 10m etc.

Huyo anayesave 50k kwa mwezi ina maana ndani ya miaka mi5 ndio ana 3m ambayo haitoshi hata kukamilisha tofali za nyumba achilia mbali kununua kiwanja.

Hapo ndipo Inspirantional speaker wanapofeli,kitu kilichowork kwako kinaweza kisifanye kazi kwa mwingine.


Lakini sidhan kama ni lazima wote tujenge nadhqn kupunguza makali ya maisha unaweza save then ukainvest
 
Kaka mmoja ana miaka 39 yeye kasema hawezi kuoa kisa eti mali zake katafuta mwenyewe alafu mke aje kukaa bure?

Tukamuuliza una mali gani hizo?
- Kasema amejenga nyumba ya mil 150 mwenyewe
-Ana gari mbili ya kazini na ya starehe

Hoja yake anasema eti yeye kaangaika mwenyewe, afu kirahisi mwanamke aje na mabegi tu alale aishi bure?

Huyu kaka mbinafsi kweli

Swali kwa mleta uzi na wanaume wengine hivi mama zenu walivyoolewa kwa baba zenu si walikuja tu na mabegi? sasa nyie mnaumizwa nini tukija na mabegi?[emoji23][emoji23][emoji23]

Btw hongera sana kujenga umetutia moyo.hata sisi wadada tunapambana kujenga.
Ahsante Ila Mimi sipo Kama huyo, Nina mke na Watoto wawili. Naheshimu Sana wanawake
 
Leo Kuna jambo ningependa kuwaeleza, lengo ni vijana kutokata tamaa magumu ni sehemu ya maisha. Kikubwa tuweke malengo na tupambane.

Angalizo: Kama una husda na wivu hii post usisome maana utashindwa kula leo.

Nilianza pilika za maisha mwaka 2011 soon after kugraduate, mambo yalikuwa mengi Sana Ila yalikuwa poa.

Ilipofika 2014 mwezi wa 3, nikanunua kiwanja goba njia nne kwa mil 18, ni kizuri na kikubwa. Hivyo jukumu lililokuwa mbele yangu ni kuanza kufikiria kujenga, japo pia nilikuwa na wazo la kuwa na hardware hukohuko goba kwa kuwa ujenzi kule ulikuwa na Kasi Sana.

Nilichofanya ni kuhakikishia kila mwezi naweka mil 1.8 ili mwisho wa mwaka nianze kidogo, na mwaka unaofuata mwishoni niendelee.
Mwaka wa kwanza yaani 2015 mwishoni nilikuwa nimekusanya jumla mil 21 hivyo nikaanza na foundation na kunyanyua boma. Nikalitelekeza.

Mwaka unaofuata 2016 nikaendelea na plan zangu zilezile na ilipofika December nikakusanya tena mil 21, hapa nikapiga bati kipindi hiki bati zile aina ya versatile zilishika chati jumla zilikuwa 145(zilibaki 6), pia niliiweka grills, mashimo ya choo, plumbing na wiring pesa yote ikaishia hapo.

Mwaka unaofuata 2017, vilevile nikakusanya mil 21 sikuacha lengo langu. Safari hii kazi ilikuwa kuzungusha ukuta, kupiga plasta, kununua gypsum, na tiles nikaziacha ndani humo.

Mwaka 2018 ulikuwa ni kwa ajili ya finishing, bahati mbaya sikufanikiwa kumaliza finishing Ila nikaapa 2019 lazima nimalizie.
Mwaka 2019 ulikuwa mwaka wa mwisho na ilipofika mwezi wa 7, kila kitu kilikuwa tayari na nikahakia hapo rasmi. Jumla ilitumika mil 78.

Kuhusu hardware, Sasa hivi ni moja ya inayofanya vizuri goba kwa kuwa nilitumia ujanja wa kupita sites na kuongea na wenye nyumba na mafundi, nawapunguzia Bei kidogo wananipa kazi. SoMo kubwa usipende Sana faida kubwa, watu watakuja kwako.

Wito kile unachofanya fanya zaidi na zaidi, weka plan zako.vizuri, na Kama bado mambo hayajakaa sawa tafuta zaidi weka pembeni kidogo starehe.
Naogopa picha kwa kuwa pale najulikana sababu ya biashara zangu(gen supplies, kampuni ya mfukoni ya construction na hardware)

Nimepitia comments mbali mbali kwenye huu uzi na kujifunza humu kwenye jukwaa kuna too much negativity when it comes to maendeleo..it is as if vijana wengi wamekata tamaa sana na hawaamini inawezekana kabisa kufanya maendeleo bila ubadhirifu au wizi wa mali za umma kwao ni next to impossible ..guess what ? kuna vijana wengi tu wanafanya maendeleo kwa decent na passive income wanapata...yani savings ya 1.8M imeonekana ni jambo la ajabu kabisa lakini nionavyo mimi inawezekana na kuna watu kibao wanalipwa hela ya kutosha kabisa kuweza kusave 1.8M ingawa nikiri pia sio rahisi kwa hii mishahara yetu ya tia maji tia maji ya walio wengi lakini inawezekana kabisa na mifano ipo

Labda ombi kwa mleta uzi ungefungua macho ya vijana wengi kwa kuelezea njia unazotumia kufanya savings zako, mtaji wa kufungua hardware ulipataje ..ulikopa au ulidunduliza au ulishikwa mkono ? biashara zipi unaweza kushauri vijana wafanye kwa ajili ya kujipatia kipato na kujiendeleza na mbinu nyingine kadha wa kadha ...

Vijana wanakuwa na mahasira kwakua BOQ za ujenzi zimejaa chungu nzima mtandaoni utata ni jinsi ya kupata michongo ambayo itakuwezesha kujenga hiyo nyumba ...ukiweza kushauri utakuwa umesaidia vijana wengi zaidi kuliko kutoa empty numbers

"Kazi iendelee"
 
Hongera sana mkuu.
Hii ni inspiration nzuri kwa vijana wanaotamani kajenga. Wajue inawezekana.
Ila mkuu jiandae kupokea matusi, kebehi, kejeli na kila kitu. Humu wamejaa ma-negative thinkers wanaopendelea kuona habari za kukatisha tamaa, matatizo, kulia njaa, na zinazofanana na hizo; Wasikufanye uvunjike moyo ku-share mafanikio yako humu JF. Hongera sana kwa mara nyingine mkuu!!
Wajinga mnapeana pongezi
 
Back
Top Bottom