Nilitumia miaka mitano ya kujenga nyumba ya ndoto yangu, inawezekana vijana tusilale

Leo Kuna jambo ningependa kuwaeleza, lengo ni vijana kutokata tamaa magumu ni sehemu ya maisha. Kikubwa tuweke malengo na tupambane.

Angalizo: Kama una husda na wivu hii post usisome maana utashindwa kula leo.

Nilianza pilika za maisha mwaka 2011 soon after kugraduate, mambo yalikuwa mengi Sana Ila yalikuwa poa.

Ilipofika 2014 mwezi wa 3, nikanunua kiwanja goba njia nne kwa mil 18, ni kizuri na kikubwa. Hivyo jukumu lililokuwa mbele yangu ni kuanza kufikiria kujenga, japo pia nilikuwa na wazo la kuwa na hardware hukohuko goba kwa kuwa ujenzi kule ulikuwa na Kasi Sana.

Nilichofanya ni kuhakikishia kila mwezi naweka mil 1.8 ili mwisho wa mwaka nianze kidogo, na mwaka unaofuata mwishoni niendelee.
Mwaka wa kwanza yaani 2015 mwishoni nilikuwa nimekusanya jumla mil 21 hivyo nikaanza na foundation na kunyanyua boma. Nikalitelekeza.

Mwaka unaofuata 2016 nikaendelea na plan zangu zilezile na ilipofika December nikakusanya tena mil 21, hapa nikapiga bati kipindi hiki bati zile aina ya versatile zilishika chati jumla zilikuwa 145(zilibaki 6), pia niliiweka grills, mashimo ya choo, plumbing na wiring pesa yote ikaishia hapo.

Mwaka unaofuata 2017, vilevile nikakusanya mil 21 sikuacha lengo langu. Safari hii kazi ilikuwa kuzungusha ukuta, kupiga plasta, kununua gypsum, na tiles nikaziacha ndani humo.

Mwaka 2018 ulikuwa ni kwa ajili ya finishing, bahati mbaya sikufanikiwa kumaliza finishing Ila nikaapa 2019 lazima nimalizie.
Mwaka 2019 ulikuwa mwaka wa mwisho na ilipofika mwezi wa 7, kila kitu kilikuwa tayari na nikahakia hapo rasmi. Jumla ilitumika mil 78.

Kuhusu hardware, Sasa hivi ni moja ya inayofanya vizuri goba kwa kuwa nilitumia ujanja wa kupita sites na kuongea na wenye nyumba na mafundi, nawapunguzia Bei kidogo wananipa kazi. SoMo kubwa usipende Sana faida kubwa, watu watakuja kwako.

Wito kile unachofanya fanya zaidi na zaidi, weka plan zako.vizuri, na Kama bado mambo hayajakaa sawa tafuta zaidi weka pembeni kidogo starehe.
Naogopa picha kwa kuwa pale najulikana sababu ya biashara zangu(gen supplies, kampuni ya mfukoni ya construction na hardware)
Haya ndiyo mawazo yanayotakiwa hapa mwanangu. Kongole
 
Weka picha ya huo mjengo
 
Hardware inalipa Sana Kama una mzunguko mzuri, pale goba kumaliza lori mbili za cement za Tani 30 kwa mwezi ni kitu Cha kawaida sana. Hapo ni cement tu, hujauza vingine
Wacha watu waendelee kushangaa
Mkuu unatakiwa uwe na Budget Kiasi Gani kuwa na Kihardware tu cha Kawaida.
 
Ukisave kila mwezi 50000 end of yr una 3m mkuu ukiidumbukiza kwa biashara kila wiki una uhakika wa kulaza faida ya 100k..kwa mwez hukos 300k as faida..ss hizo 300k tumia 70 tu 230 fungulia akaunti..end of yr unaenda nunua kiwanja...na sio lazima wote tununua viwanja vya 18m..kuna had 400k

Mkuu 350,000/= ni familia nitasave vipi elfu 50? Yaani kwa siku niwe natumia elfu 10? natumiaje tena? Nauli ya kwenda kazini? na mchana,asubuhi kula kazini? Hela ya kuacha nyumbani ya kula familia? Ndio elfu 10 kwa siku itatosha?

Elfu 50 kwa mwezi maana kwa mwaka ni laki 6 ili niweze kupata kiwanja nje ya mji cha mil 1.8 inababidi nisave ndani ya miaka 2.5 baada ya hapo kupata mil 3 ya kuinua banda la chumba na sebule itanichukua tena miaka mi3.

Na hapo sio nyumba ya ndoto.
 
Tuishi kulingana na vipato vyetu mkuu mengine mwembwe
 
Mkuu tuwe realistic kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake ,kuna wenye kusave elfu moja kwa mwezi ,mwingine 20k ,mwingine 1m ,wewe 1.8m ,mwingine 10m etc.

Huyo anayesave 50k kwa mwezi ina maana ndani ya miaka mi5 ndio ana 3m ambayo haitoshi hata kukamilisha tofali za nyumba achilia mbali kununua kiwanja.

Hapo ndipo Inspirantional speaker wanapofeli,kitu kilichowork kwako kinaweza kisifanye kazi kwa mwingine.
A)Save kidogo ili ufanye investment
B)Invest ili u save kikubwa
C)Save kikubwa ili ujenge

wewe upo level A hapo usifosi Level C aliyopo mtoa mada.
 
Tuishi kulingana na vipato vyetu mkuu mengine mwembwe

Mkuu kuna vitu hauwezi kujibana kwa mfano mchele au unga kilo ni kuanzia 1200 hadi 2500 huko ,nauli ya daladala mijini ni 400 ,Chakula cha mama ntilie ugali ni buku hadi 1500 ,wali 1500 hadi 2000 ,maji ya kunywa ni 500 kwa lita.

Mkaa kibaba kimoja ni buku ,nyanya moja ths 100 hadi 200 ,kitunguu 100 hadi 200 ,mafuta ya kupikia kipimo komoja 200 ,lita elfu 4500 ,mafuta ya taa kibaba 300 lita 2500 hadi 3000...Dumu la maji 100 .

Kubana matumizi ni badala ya kununua mchele wa 2500 utanunua wa 1200,badala ya kununua mafuta ya Alizeti utanunua ya kawaida(ya karanga) etc kwenye maisha huwa sikubaliani na hawa mainspirational speaker wengi story zao CD zina scratch sana na kurukaruka.

Yeye anakwambia tu anasave 1.8m lakini hakwambii anaingiza ngapi kwa mwezi.
 
usipende Sana faida kubwa, watu watakuja kwako.

Kwenye huu uzi wako,ninapopaweza ni hapo tu na nimepaelewa sana
Kuna kipindi wengine walikuwa wanauza cement 14500, Mimi nilikuwa nauza 14000
 
A)Save kidogo ili ufanye investment
B)Invest ili u save kikubwa
C)Save kikubwa ili ujenge

wewe upo level A hapo usifosi Level C aliyopo mtoa mada.

Hapo sawa mkuu, hawa inspirational speakers wanadhani watu wote tunaingiza mamilioni kama wao.
 
Back
Top Bottom