Nilivunja urafiki na kumshushia heshima Mjomba wangu baada ya kugundua ni mtu mwenye tabia ya kuingilia faragha yangu

Nilivunja urafiki na kumshushia heshima Mjomba wangu baada ya kugundua ni mtu mwenye tabia ya kuingilia faragha yangu

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,235
Reaction score
4,252
Ndugu zangu kuishi Afrika lazima uweze kuvumilia kero za watu lasivyo patakushinda
Kero kubwa ya Afrika ni watu kutaka kujua siri zako na mambo binafsi yanayohusiana na faragha

Labda nianze kwa kujielezea kiasi, mimi ni baba wa watoto wawili wa kwanza ana miaka mitano wa pili miaka miwili ninaishi kwangu na mke na watoto

Mimi ni mtu ninayependa sana faragha na ni mtu ninayeheshimu kila mtu lakini kwa sharti moja, huwa sipotezi muda na siheshimu mtu yeyote asiyeniheshimu

Mimi ni mtu nisiyependa uchokozi wa aina yeyote na huwa sipendi kuchokozwa inapotokea reaction yangu inakuwa mbaya sana na mtu huyo anaweza kujuta kwa uamuzi nitakaochukua

Maisha yangu yapo katika faragha na huwa sipendi kabisa umbea kuwa na urafiki na mtu mwenye kidomodomo, mtu wa kusema mambo, kaulimbiu yangu utakachokiona hapa kiishie hapa hapa nisisikie kwa mtu

Baada ya kugundua tabia mbaya za ndugu zangu za midomo mirefu wamekuwa ni watu wasiofahamu maisha yangu kwao imekuwa ni fumbo

Mimi nina wajomba wanne, hawa wajomba wanne nawaheshimu sana tangu nazaliwa, hawa watatu kila mmoja ana maisha yake natangu niwafahamu hawajawahi kunikwaza wala sijawahi kuwakwaza

Huyu mmoja ana familia kijijini lakini anaishi mjini kwa dada yake
Kwa dada yake yupo yeye na mama yao ambaye ni bibi yangu pamoja na yeye. Dada yake alimpeleka kwake ili afanye kazi ana kama miaka 50

Huwa mara kwa mara ninapotembelea huo mkoa lazima nimsalimie dada yake ambaye ni mama mdogo wangu kwenye hiyo familia yao

Tangu zamani nikienda kwenye hiyo familia na chochote mkononi wanafurahi sana isipokuwa yeye anaishia kunikata jicho la wivu

Safari mbili za mwisho kwenda pale alinitazama vibaya sana kwa macho ya wivu
Nilipoondoka akathubutu kunipigia simu akiniuliza kama nimeoa,
Sikumjibu chochote kwasababu sipendi umbea nachukia sana maswali ya kimbea

Safari ya mwisho kwenda pale baada ya kuondoka akanipigia simu akanambia nizae watoto kwasababu dunia ya leo imeharibika sana wanaume wanaolewa
Baada ya maneno hayo machafu sikujibu

Nilipokata simu nikajiuliza huyu mtu mbona kama amekuwa wa hasidi katika maisha yangu?
Watu kuharibika inahusiana nini na maisha yangu?
Mke wangu ninayemuoa mimi kwa faida zangu anamhusu nini yeye?
Anayetunza mke wangu ni mimi au yeye?
Watoto wangu wanamuhusu nini mtu mwingine?
Mbona ni maisha yangu binafsi?
Mbona wanaume hatuna tabia za chokochoko?

Nikagundua huyu ni mtu wa chokochoko

Baada ya hapo nikamlima Block ya nguvu naendeleza urafiki na wale tunaoheshimiana
 
Ni vile umelichukulia negative kwan mjomba nae si mama si ajue tu kama una mke au la yaan kua na mke imekua faragha wakat umemuoa kaka? Au kua na watoto ni faragha kwa mjomba wako? Me nkadhan anakuuliza mnafikishaga shemej au unapigaga vingap? Umeyakuza tu mambo hakuna aliekuingulia faragha. Kwanza inabidi uelimishwe nini maan ya faragha
 
Hii ni changamoto sana kwa sisi watu weusi. Mwingine anakuuliza unaoa lini. Surely? Inakera sana. Usipochora mstari mwekundu wa NO GO ZONE, watu watataka kujua hadi unakunya mavi mafungu mangapi.
 
mtoa mada nimemwelewa. Hiyo hali ya kufuatiliwa mpaka mambo binafsi watu haswa ndugu wanayo sana.
 
Hii ni changamoto sana kwa sisi watu weusi. Mwingine anakuuliza unaoa lini. Surely? Inakera sana. Usipochora mstari mwekundu wa NO GO ZONE, watu watataka kujua hadi unakunya mavi mafungu mangapi.
Serios inakata sana, siku ukikutana na mke mbaya akianza kukuangusha huwa hawaji kukusaidia wanafurahi
 
Mjomba anauliza kama umeona utakasirika eti ni faragha. Sio dalili za ushoga kweli hizo?

Sasa kuna faida gani kuwa sehemu ya ndugu na jamaa kama huwezi hata kushauriwa kwenye masuala common tu. Si umweleze sababu za wewe kutofanya hivyo?
 
Ni vile umelichukulia negative kwan mjomba nae si mama si ajue tu kama una mke au la yaan kua na mke imekua faragha wakat umemuoa kaka? Au kua na watoto ni faragha kwa mjomba wako? Me nkadhan anakuuliza mnafikishaga shemej au unapigaga vingap? Umeyakuza tu mambo hakuna aliekuingulia faragha. Kwanza inabidi uelimishwe nini maan ya faragha
NAKAZIA

Huenda huyu jamaa anaonekama delicious
 
Ni vile umelichukulia negative kwan mjomba nae si mama si ajue tu kama una mke au la yaan kua na mke imekua faragha wakat umemuoa kaka? Au kua na watoto ni faragha kwa mjomba wako? Me nkadhan anakuuliza mnafikishaga shemej au unapigaga vingap? Umeyakuza tu mambo hakuna aliekuingulia faragha. Kwanza inabidi uelimishwe nini maan ya faragha
Huyu atakuwa na shida kubwa kama sio ushoga
 
Back
Top Bottom