Mr Why
JF-Expert Member
- Nov 27, 2019
- 2,235
- 4,252
Ndugu zangu kuishi Afrika lazima uweze kuvumilia kero za watu lasivyo patakushinda
Kero kubwa ya Afrika ni watu kutaka kujua siri zako na mambo binafsi yanayohusiana na faragha
Labda nianze kwa kujielezea kiasi, mimi ni baba wa watoto wawili wa kwanza ana miaka mitano wa pili miaka miwili ninaishi kwangu na mke na watoto
Mimi ni mtu ninayependa sana faragha na ni mtu ninayeheshimu kila mtu lakini kwa sharti moja, huwa sipotezi muda na siheshimu mtu yeyote asiyeniheshimu
Mimi ni mtu nisiyependa uchokozi wa aina yeyote na huwa sipendi kuchokozwa inapotokea reaction yangu inakuwa mbaya sana na mtu huyo anaweza kujuta kwa uamuzi nitakaochukua
Maisha yangu yapo katika faragha na huwa sipendi kabisa umbea kuwa na urafiki na mtu mwenye kidomodomo, mtu wa kusema mambo, kaulimbiu yangu utakachokiona hapa kiishie hapa hapa nisisikie kwa mtu
Baada ya kugundua tabia mbaya za ndugu zangu za midomo mirefu wamekuwa ni watu wasiofahamu maisha yangu kwao imekuwa ni fumbo
Mimi nina wajomba wanne, hawa wajomba wanne nawaheshimu sana tangu nazaliwa, hawa watatu kila mmoja ana maisha yake natangu niwafahamu hawajawahi kunikwaza wala sijawahi kuwakwaza
Huyu mmoja ana familia kijijini lakini anaishi mjini kwa dada yake
Kwa dada yake yupo yeye na mama yao ambaye ni bibi yangu pamoja na yeye. Dada yake alimpeleka kwake ili afanye kazi ana kama miaka 50
Huwa mara kwa mara ninapotembelea huo mkoa lazima nimsalimie dada yake ambaye ni mama mdogo wangu kwenye hiyo familia yao
Tangu zamani nikienda kwenye hiyo familia na chochote mkononi wanafurahi sana isipokuwa yeye anaishia kunikata jicho la wivu
Safari mbili za mwisho kwenda pale alinitazama vibaya sana kwa macho ya wivu
Nilipoondoka akathubutu kunipigia simu akiniuliza kama nimeoa,
Sikumjibu chochote kwasababu sipendi umbea nachukia sana maswali ya kimbea
Safari ya mwisho kwenda pale baada ya kuondoka akanipigia simu akanambia nizae watoto kwasababu dunia ya leo imeharibika sana wanaume wanaolewa
Baada ya maneno hayo machafu sikujibu
Nilipokata simu nikajiuliza huyu mtu mbona kama amekuwa wa hasidi katika maisha yangu?
Watu kuharibika inahusiana nini na maisha yangu?
Mke wangu ninayemuoa mimi kwa faida zangu anamhusu nini yeye?
Anayetunza mke wangu ni mimi au yeye?
Watoto wangu wanamuhusu nini mtu mwingine?
Mbona ni maisha yangu binafsi?
Mbona wanaume hatuna tabia za chokochoko?
Nikagundua huyu ni mtu wa chokochoko
Baada ya hapo nikamlima Block ya nguvu naendeleza urafiki na wale tunaoheshimiana